“Tanzania inaua zaidi ya 11,000 ekwa mwaka kwaajili ya biashara ya pembe za ndovu na Rais wake amefumbia macho ili Prince aje kushikana naye mikono?” limeandika gazeti la Daily Mail la Uingereza.
Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa wiki hii Rais Jakaya Kikwete, atakutana na Prince of Wales, Duke of Cambridge, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais mambo ya nje wa nchi hiyo, William Hague kwenye mkutano wa viongozi wa nchi 50 huku Tanzania ikiwa na sifa mbaya kwa mauaji ya Tembo.
Mkutano huo ni mahsusi kwaajili ya kuokoa viumbe hao wanaohatarishwa kupotea kutokana na kushamiri kwa mauaji.
Mkutano huo wa Alhamis hii utajaribu kufikia muafaka kuhusiana na muitikio wa kidunia dhidi ya biashara haramu ya pembe za ndovu yenye thamani ya paundi bilioni 6 kwa mwaka na ambayo hudhamini makundi ya kigaidi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Theluthi ya pembe zote za ndovu zinazokamatwa barani Asia hupitia Tanzania na kila siku tembo 30 huuliwa ambao ni sawa na tembo 11,000 kila mwaka.
“Tanzania is effectively a one-party state with a pervasive intelligence apparatus, and nobody seriously contends that this slaughter is happening without high-level complicity. Yet not a single kingpin has been charged and convicted. MPs, senior officials and businessmen are named in parliament and the media, but investigations fizzle out and little happens,” Daily Mail wameandika.
Katika gazeti la leo la MWANANCHI la nchiniTanzania limeandika habari hii kwa kina kwa ufupi linasema ‘Kwa jumla Tanzania inatawaliwa na chama kimoja ikiwa chini ya chombo kimoja cha intelijensia, hakuna mtu anayepinga kuwa hayo yanafanyika bila kuhusisha ngazi za juu. Lakini hakuna hata kigogo mmoja aliyekamatwa na kushtakiwa.” Inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.