Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MKUTANO WA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI KUFANYIKA DAR E S SALAAM SEPTEMBA 18-2014 UKUMBI WA MIKUTANO WA BENKI KUU YA TANZANIA BoT.

$
0
0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo. Kushoto ni Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (katikati), akiwa na viongozi wenzake wa bodi hiyo. Kutoka kulia ni Kaimu Msajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala, Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad, Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Mwanasheria wa Bodi, Ibrahim Mohamed.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo. 
 Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad akizungumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu mkutano huo.
 Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani, Ezekiel Stephen na Kaimu Nsajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale 

 BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi sasa imewafuta  wataalamu 86 na kampuni 36 kufanyakazi ya ujenzi baada ya kushindwa kufuata sheria. 

 Hayo yalielezwa na Msajili wa bodi hiyo Jehad Jehad wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi utakaofanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Septemba 18, 2014 jijini Dar es Salaam ambao uta wahusisha wadau wa  sekta ya ujenzi. 

 "Kazi yetu kubwa ni kutoa ushauri wa  shughuli za ujenzi na kama tukibaini kuna kampuni inakwenda kinyume tunaifuta " alisema Jehad. 

 Alisema lengo la mkutano huo wa Septemba 18 ni kuwanoa wataalamu wa fani hiyo ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknologia na kitaaluma katika sekta ya ujenzi, kubadilishana mawazo na kuboresha huduma za taaluma. 

 Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Ambwene Mwakyusa alisema Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla (Building Codes) itakayoweza kuwabana wajenzi ya maghorofa ambayo yanabomoka hapa nchini. Dk. Mwakyusa alisema sheria hiyo ingekuwepo ingewaongoza wataalamu wa majengo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi kwenye jengo husika tofauti na ilivyosasa.  
Dk.Mwakyusa alisema kutokana na sheria hiyo kutokuwepo wataalamu wa majengo wanapotumia vifaa vya ujenzi ambavyo havina kiwango na wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya majengo wanayojenga kuanguka wanakutwa hawana hatia. 

“Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla kama ikiwepo sheria itamuongoza mtaalamu wa majengo afuate sheria iliyopo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi mfano kama mbao au nondo zinatakiwa zitumike aina gani kwenye jengo husika ,”alisema Dk.Mwakyusa. Katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan Mwinyi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>