Licha ya kuwepo kwa madimbwi ya maji yaliyochanganyikana na maji taka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam , raia hao wa kigeni ambao hawakufahamika wanatoka taifa gani walinaswa na kamera ya mtandao wa habari za jamii.com wakipita maeneo ya posta mpya jirani na jengo la IPS wakiwa pekupeku jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja walikokuwa wakienda. Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya madhehebu kutoka nje ya nchi ambayo waumini wake hawavai viatu kutokana na imani zao. (Picha zote na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)