Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Kessy akiwa bungeni.
BUNGE Maalum la Katiba limechafuka wakati wa Majadiliano ya Taarifa za Kamati baada ya Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Kessy kusema Serikali ya Zanzibar inatumia fedha za Tanzania Bara kuendesha mambo yake ikiwemo kulipwa mishahara.
Wajumbe kutoka Zanzibar wamemshambulia kwa maneno makali wakidai kawavunjia heshima hali iliyopelekea Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kuingilia kati katuliza mzozo huo.