Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UPDATES: LORI LA MAFUTA LAANGUKA KIMARA MWISHO NA KUZIBA NJIA

$
0
0
Wananchi wengine waiona ajali hii kama 'neema' na kuanza kuchangamkia mafuta yaliyomwagika.
GARI lenye namba T748 ABJ lililokuwa limebeba mafuta ya diseli kutoka Dar es Salaam kwenda Singida, limeanguka leo asubuhi na kusababisha foleni ndefu maeneo ya Kimara-Darajani jijini Dar es Salaam.Dereva wa gari hilo aliyefahamika kwa jina moja la Juma, alikimbizwa hospitali.  Gari hilo lilikuwa na lita 34,000 za mafuta, mali ya Nassor Filling Station ya jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo wananchi wa maeneo hayo, badala ya kutoa msaada, walianza kuiba mafuta hayo kabla ya kutawanywa na polisi waliofyatua mabomu ya kutoa machozi na juhudi za kulitoa barabarani zikaanza mara moja.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Polisi wakipakia madumu ya mafuta waliyoyakamata kutoka kwa wananchi.
Polisi wakidumisha ulinzi eneo la ajali.
 Foleni iliyosababishwa na ajali hiyo eneo la Kimara, Dar.
Lori la mafuta baada ya kuanguka. 

 Kazi ya kuhamisha mafuta kutoka kwenye gari lililoanguka kwenda jingine ikifanyika.
Polisi wakitafuta mafuta yaliyoibiwa katika moja ya maduka ya jirani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>