Kisukari,ni ugonjwa unaotokea katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, ambapo kiwango cha sukari rahisi(glucose) kinazidi katika damu.Kawaida, kiwango cha sukari katika damu kinarekebishwa na kemikali inayoitwa insulini inayotolewa nakongosho.
Sasa inapotokea kemikali ya insulini kutoka katika kongosho,utengenezaji wake ni duni au seli za mwili zinashindwa kuifanyia kazi kemikali hiyo kama inavyotakiwa,na hivyo kuruhusu sukari kuongezeka katika damu.
Kuna dalili kadhaa zinazotokea pale sukari inapokuwa imezidi katika damu:
1. Kupatwa na haja ndogo mara nyingi;
2. kiu kali ya maji;
3. kuhisi njaa kali.
AINA ZA KISUKARI:
1. KUTOTENGENEZWA KWA INSULINI
Mwili unashindwa kutengeneza kemikali ya insulini,kwahiyo mhusika huwa ana
hitaji la kujiwekea emikali hiyo mwilini.Aina hii inaweza kumpata mtu kabla hajafikisha miaka 40,sana sana ni kipindi cha ujana.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Asilimia 10 ya wagonjwa wa kisukari wanaugua aina hii ya kwanza.Mgonjwa atatakiwa ajichome sindano ya kemikali ya insulini katika maisha yake yote.Na mara nyingi huwawanatembea na kifaa maalumu cha kupimia kiwango cha sukari katika damu,mara anapoona imezidi anatakiwa ajichome sindano ya insulini ili kuipunguza katika kiwango maalumu.
2. KIWANGO KIDOGO CHA INSULINI
Katika aina hii mwili unashindwa kutengeneza kemikali ya insulini ya kutosha,au mwili unashindwa kuitumia kemikali hiyo.Asilimia 90 ya wagonjwa wa kisukari wanaugua aina hii ya pili.
Aina hii inaweza kuzuiwa kwa:
1.Kupunguza uzito;
2.Chakula kamili;
3.Mazoezi mengi;
4.Kufuatilia kiwango cha sukari katika damu.
Na ikiwa aina hii itashindwa kuzuiwa na mgonjwa,itampeleka katika hatua ya kujiwekea kemikali ya insulini sana sana kwa njia ya kunywa vidonge.
3. KISUKARI WAKATI WA UJAUZITO
Inawapata sana wakina mama wakati wakiwa wajawazito,na kuwafanya wawe na kiwango kikubwa sana cha sukari katika damu.
Inaweza kuzuiwa kwa mazoezi na chakula kamili.Inaposhindwa kuzuiwa kwa mama mjamzito inamsababishia matatizo wakati wa kujifungua,mwili wa mtoto unaweza kuwa mkubwa kuliko unavyopaswa kuwa.
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanawake wengi ambao lishe yao kabla hawajawa wajawazito ilikuwa na kiwango kikubwa cha mafuta ya wanyama na chenye kolesto wanakuwa katika hatari ya kupata aina hii ya kisukari.
Vitu gani vinaweza kusababisha ugonjwa huu wa kisukari:
1. UZITO KUPITILIZA
Unapokuwa na uzito mkubwa,unajiweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.Uzito wa mwili kupitiliza unaufanya mwili kutengeneza kemikali ambayo inaenda kuvuruga mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
2. KIWANGO KIDOGO CHA HOMONI ZA TESTOSTERONE
Ikiwa mtu atakuwa na kiwango kidogo cha utengenezwaji wa homoni hii kutoka katika korodani za mwanaume na ovari za mwanamke, basi kiwango chake katika damu kikishuka
kinamuweka mtu katika hatari ya kupata aina ya pili ya kisukari.
Ndio maana watu wenye umri mkubwahatari inakuwa kubwa kwasababu, kiwango cha utengezaji wa homoni hii unapungua kiasili,na kuzuia insulini isifanya kazi yake sawa sawa.
MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA IKIWA UTASHINDWA KUZUIA ONGEZEKO LA SUKARI KATIKA DAMU:
1. Matatizo ya MachoGlaucoma-kuharibika kwa mishipa kuona na inaweza kutibiwa kwa dawa ya matone ya macho.Cataracts-ukungu katika macho unazuia kuona vizuri ambao unawezakuondolewa kwa opareshenimaalumu ikiwa kuna ulazima.
2. Matatizo ya miguu
3. Matatizo ya ngozi
4. Matatizo ya moyo
5. Matatizo ya kusikia
6. Matatizo ya nguvu za kiume
7. Matatizo ya tumbo
8. Kiharusi
9. Michubuko kushindwa kupona haraka
10. Matatizo ya fizi za meno
HUO NDIO UGONJWA WA KISUKARI KWA UFUPI.