Mb Dog, pichani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed, Mb Dog, amesema mashabiki wake wataanza kuona video ya wimbo wake wa Mbona Umenuna katika vituo vya luninga ndani ya wiki hii.
Video hiyo iliyoandaliwa kwa kiwango cha juu iliingizwa katika mitandao ya kijamii, huku kwenye luninga ikianza kusambazwa wiki hii ili kuwapa burudani mashabiki wake.Akizungumza leo mchana, Mb Dog alisema kwamba alianza kwanza kuingiza kwenye mitandao ya internet ili kuwapa nafasi watu wote, wakiwamo wan je ya nchi kuitazama video hiyo.
“Hii ni video nzuri ambayo iliingia kwanza kwenye mtandao na kuwapa fursa watu kuitazama, ambapo natarajia mashabiki wengine wataanza kuangalia luningani wiki hii.
"Naamini mashabiki wangu wote watapata burudani ya kutosha, ukizingatia kuwa nimefanya video nzuri inayoonyesha umahiri wangu kisanaa,” alisema.
Mb Dog ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wenye uwezo wa juu wa kutunga na kuimba, ambapo wimbo wake wa kwanza uliomuibua ni Latifa na nyinginezo.