Enzi ya Uhai wa Sakabenga
Mwanachuo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam amekutwa amefariki kwenye chumba ambacho alikuwa akikaa chuoni hapo. Kwa mujibu wa wenzake wanasema mwanachuo huyo alitoka kujisomea na alipofika chumbani hapo aliamua kujipumzisha, baada ya muda wenzake walianza kumwasha na hakuweza kuamka ndipo waliamua kupiga simu kwenye kituo cha afya kinachopatikana kwenye eneo la Chuo na walipofika walikuta ameishafariki. Mwili umepelekwa na gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mwili wa mwanachuo huyo ukitolewa kwenye hostel ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwili wa Sakabenga ukiwekwa kwenye gali la wagonjwa