TAARIFA ZILIZOTUFIKIA, ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.
GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA KUTOKANA NA GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM,WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW,KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA KWA MIPIRA MIWILI (MATAIRI) YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH.
AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.
NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU NANE AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.
TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.