Uchunguzi wa shirikisho la soka la Italia umebaini kuwa mchezaji tineja wa Cameroun Joseph Minala ana umri wa miaka 17 wala sio 42 kama ilivyodhaniwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari.
Mnamo mwezi Februari mtandao mmoja wa michezo barani Afrika ulichapisha habari ambayo ilizua dukuduku iwapo kiungo huyo alikuwa amedanganya umri wake .
Mtandao huo ulichapisha habari za kuashiria kuwa hakuwa tineja bali mtu mwenye umri wa miaka 42.
Uchunguzi uliofwatia ulimlazimu kukatiza kwa muda mipango yake ya kucheza soka ya kulipwa hadi pale matokeo ya uchunguzi yangewekwa wazi na maafisa wa shirikisho la soka la Italia.
Minala alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Rome na hata alishiriki mchuano wa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 wa Viareggio mnamo mwezi wa Februari.
CHANZO: BBC SWAHILI