Vijimambo kwa ushirikiano wa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Jumuiya ya Watanzania DMV wanapenda kukukaribisha kwenye sherehe ya miaka 4 ya Blog ya Vijimambo kwa kutangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani na kukemea ujangili wa mali asili wa nchi yetu siku ya September 13, 2014 itakayofanyika THE OXFORD EVENT CENTER 9700 Martin Luther King Jr HWY, Lanham, MD 20706. kutakua na burudani za kila aina kutoka nyumbani na hapa Marekani TEGA SIKIO MAMBO MENGI MAZURI YANAKUJA .
Mwenyekiti wa kamati ya Vijimambo Bwn. Baraka Daudi akitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku kamati ilipokutana na Ubalozi kwa kikao cha Maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ambayo mwaka huu mbiu yake ni kutangaza Utalii na kukemea ujangili kwa nguvu zote karibu tuungane pamoja katika siku hii maalumu ili wewe, mimi pamoja na yule wakiwemo watoto wetu wajifunze mengi kuhusu Utalii wa nchi yetu ukiwemo kukemea nguvu zote swala zima la ujangili mali asili za nchi yetu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kaimu Katibu wa kamati ya Vijimambo Bwn Julius Katanga akitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku kamati ya maandalizi ilipokutana na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo itakayofanyika September 13, 2014.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongoza kikao siku kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ilipokutana na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya maatayarisho ya mwanzo mwanzo ya sherehe hizo.
Wanakamati ya maandalizi kutoka kushoto Julius Katanga, Mayor Mlima na Baraka Daudi wakimsikiliza Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani