Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amegongwa na gari barabara ya zamani ya Dar es salaama jirani na stendi Katika Manispaa ya Morogoro na kuvunjika mguu wa kushoto. Wakizungumzia Ajali hiyo Mashuhuda wamesema dereva huyo wa boda boda Alikuta gari limesimama baranarani bila kujua ni kwanini gari la mbele yake limesimama alitanua na kulipita gari hiyo aiana ya Collora na ndipo kugongana uso kwa uso na gari hilo .
Kijana Huyo ambaye ndiye alikuwa akiendesha bodaboda ndipo alipopata Ajali mbaya iliyompelekea Kuvunjika Mguu wa Kushoto.
Muendesha Bodaboda Aliyejeruhiwa Vibaya katika Ajali hiyo akipakiwa katika gari kupelekwa Hospitali kwa Matibabu.