Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

JE UWEZO WAKO WA KUSIKILIZA UKO SAWA?

$
0
0
Inawezekana wewe ni mfanyakazi mzuri na mwenye elimu nzuri lakini unapata shida!
Watu wengi hukazana kutazama elimu zao bila kuwa wasikilizaji wazuri. Mawasiliano ni kitu cha muhimu sana kwenye maisha yako na hata kwenye kazi na biashara. Kama hatuna ujuzi mzuri wa mawasiliano katika biashara na shughuli za kila siku dunia inaweza kusimama ghafla, mambo hayatakwenda.
Mawasiliano ni njia mbili, moja ni kwa mwongeaji na nyingine ni kwa msikilizaji. Kama msikilizaji hasikilizi vizuri au haelewi kinachozungumzwa huomba kurudia ili waulize maswali au kukubaliana na kinachozungumzwa. Usikivu yakinifu/makini ni kitu kinachohitajika sana kwenye mawasiliano yako na mtu mwingine. Hebu fikiri kwamba umezungumza mambo mengi na mtu unayezungumza naye inakuwa kana kwamba hakuna ulichozungumza, hakubaliani wala kuuliza swali na haonyeshi kama ameelewa au hajaelewa. Inawezekana ukawa na wakati mgumu wa kukabiliana na mtu huyo .
Meneja mwajiri huanza kukuchukulia kawaida kama akigundua wewe sio msikilizaji mzuri, hivyo ataelekeza nguvu kwenye mtu mwingine. Kama huwezi kusikiliza vizuri inamaanisha hata katika utendaji wako utawasumbua, na ni ngumu kumfanyia mafunzo mtu ambaye hasikilizi vizuri.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mawasiliano hasa katika kusikiliza kwa makini ni kitu kizuri ambacho kinafanya watu wakupende na kukwamini. Wanaweza kukufahamu na kukujua kwa kuwa unaongea sana ila hawatakupenda kwa sababu husikilizi mahitaji yao. Na vilevile hawana uhakika wakikwambia kitu utakitilia maanani kwakuwa husikilizi, hivyo hawakuhitaji kwenye kazi zao au kwenye maisha yao. Wakati wote unapokuwa unaongea na watu (kama hutoi maagizo) weka muda kuruhusu watu wakuulize maswali au kutoa michango yao. Fanya kazi na mtu atakayekuuliza maswali, hivyo jifunze kusikiliza kwa umakini usiwaburuze watu.
Kila unayeongea nae hakikisha anajua kuwa umemsikiliza na unafanyia kazi au utashukua hatua fulani kutokana na mazungumzo hayo. Unatakiwa uwe kwenye mazungumzo ya huyo mtu kama ni swali, au unaweza kulinyumbua kwa namna nyingine kujua kama ndivyo alivyomaanisha. Mfano “Unamaanisha kuwa hicho kitu kiko hivi au vile?” unamfanya anayeongea nawe kuwa na imani na wewe na kumfanya aje siku nyingine kuomba hata ushauri.
  • Usiongee mfululizo, achia nafasi watu wengine waongee.
  • Rudia swali lililoulizwa, hata kama unalo kichwani. Rudia kabla ya kuanza kujibu.
  • Ukimaliza kujibu uliza kama watu wameridhika na majibu yako au kunasehemu haijaeleweka.
  • Kama huna kumbukumbu nzuri , andika vitu vya msingi watu wengine wanapoongea ili wakati wa kuongea ionekane kwamba ulisikiliza kwa umakini na ukaelewa alichokiongea.
Inawezekana wewe ni mtu makini sana duniani na mwenye akili kama unavyojitizama, ila kama huwezi kuongea vizuri na kusikiliza vizuri na kwa umakini akili zako zinakuwa hazina faida sana. Hakikisha unasikiliza watu wengine na mawazo yao kwa umakini bila kuonyesha kwamba unajua zaidi ila kuwa kwenye picha ya muulizaji na uweze kumsaidia.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>