Huyu ndiye Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka na mtoto huyo kusiko julikana huku wasamalia wema wakitaka kutoa misaada.
Hatimaye Mama aliyetoroka na mtoto aliyeungua moto apatikana kupiga simu katika Chombo cha Mbeya yetu Blog kuwa yupo Njombe kwa baba mzazi wa mtoto huyo nakuomba radhi kuwa aliondoka bila kuaga kesho saa nane mchana atakuwa amerudi na mtoto huyo
Mama huyo amejitokeza baada ya mtandao wa Mbeya yetu kuandika mapema leo kwamba alikuwa ametoweka bila Taarifa zozote, Akiongea na Mbeya yetu amedai kwamba yeye aliondoka ili akashauriane na wazazi wa Mtoto huyo ili waone ni jinsi gani watamsaidia lakini alipo hojiwa amejikanyaga kanyaga na kuongea bila kuwa na uhakika na kile anacho zungumza.
Hata hivyo hapo kesho atafanyiwa mahojiano ya kina na kuona ukweli ukowapi kwa kuwa anatia mashaka na maelezo yake, Tunaendelea kusisitiza kuwa Kama kuna Mtu anahitaji kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo kasha onesha wasiwasi na kuondoa imani watu.
Habari zaidi zitakuja