Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

UNA JAMBO UNATAKA KUAMUA MAISHANI? JIFUNZE NAMNA NZURI YA KUULIZA MASWALI MWENYEWE

$
0
0

Kuuliza maswali ni taaluma katika kuwasiliana na watu wengine, unahitaji kujua namna ya kuuliza maswali kulingana na mtu , wakati na sehemu uliyopo.

1. Swali zuri linahitaji ubunifu katika kufikiri
Huu ndio ukweli ninafikiri, unapotaka kuuliza swali zuri unahitaji kuwa mbunifu katika kufikiri kwako. Usiulize kwasababu ya kuuliza tu bali, fikiri atakayekuwa anakujibu atatakiwa kujibu nini? Kama unahitaji jibu sahihi unahitaji kuuliza swali sahihi na kwa ustadi mkubwa unapokuwa kazini unahitaji kuweka akili yote kwenye swali kwani jibu ni bidhaa unayohitaji.


2. Unapokua Umepotea sehemu fulani katika jambo, tafuta swali na sio jibu
Jinsi taaluma inavyokwenda kama unahitaji kuwa bora na mwenye kutegemewa katika utendaji wa kazi, unahitaji kuuliza maswali mazuri. Mara nyingi maswali yaliyozoeleka ni namna ya kubadilisha kazi. Unapotaka kubadilisha kazi jiulize au uliza maswali ya kukusaidia kufika kule unakotaka kufika.


ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


3. Fikiri mlengo wa taaluma yako kama swali la kitaaluma
Kama unahitaji kuwa mfugaji wa kuku, wengi tunafikiria mabanda mangapi , niyaweke wapi, chakula kitapatikana wapi na soko liko wapi? Tunafikilia mambo ya kawaida ambayo kila mtu hufikiria, unapaswa kujiuliza je nina msingi wa elimu ya ufugaji? ninajua nini kuhusu ufugaji kabla ya kuanza kufuga. Je nimejiandaa kiakili kufuga pamoja na changamoto zake?
Unatakiwa kuuliza maswali ya msingi ya kule unakotaka kwenda kabla ya kuunza kwenda. Wengi wanategemea wakistaafu wataanza kufuga au kulima mananasi kwasababu wameambiwa yanalipa. Jiulize leo, kabla miaka 20 ijayo ya kustaafu haijakufikia endapo utakuwa hai, unahitaji kujua nini sasa?

4. Kuuliza swali nzuri ni kazi nahiyo kazi unapaswa kuifanya mwenyewe
Usitegemee watu wengine wakuulizie maswali yako, ni kazi yako na maswali unapaswa kuuliza wewe. Wewe ndio kiongozi wa maisha yako mwenyewe kwa hiyo unapaswa kujua maswali ya kuuliza yanayohusu maisha yako , taaluma yako na familia yako.

5. Tafuta maswali ya watu wengine ujifunze kuuliza ya kwako.
tafuta watu wanaojua kujiuliza maswali halafu ujifunze kutoka kwao. Wanapoamua kufanya jambo huwa wanauliza maswali gani, wapi, kwa nani, na kwa wakati gani?Uwezo wako wa kuuliza maswali unaonyesha upeo wako wa kuelewa ni wa kiasi gani, hivyo unahitaji kupevuka namna unavyofikiri.
Usitafute kijifunza kutoka kwa watu ambao wanalalamika au upeo wao ni mdogo kuliko wa kwako. Ongeza ujuzi wa kufikiri kwa kuuliza maswali mazuri, kama huna uhakika na unachotaka kuuliza unashauliwa kutokuuliza. Usiende mwendo wa kisiasa, kwa kuuliza maswali ya kisiasa, utabeba porojo nyingi sana.
Hebu jikague namna gani wewe hupenda kuuliza maswali? Je maswali yako yameonesha ukomavu wako wa kufikiri?

na Bongo 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>