↧
TID ALALA MAHABUSU YA OYSTERBAY
↧
WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MH. PROF. MAKAME MBARAWA (MB) AHITIMISHA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)
Katikati ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akisikiliza jambo wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.![]()
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa juu ya mkutano wa sikumbili wa maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akitoa hotuba yake ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 10 za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akizungumza Jambo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRAWaziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Prof. John Nkoma
Meneja wa Pangani FM Richard Charles Katuma Meneja msaidizi na Mhariri mkuu wa Radio hiyo ya Pangani akikabidhiwa Rasmi Reseni ya Uendeshaji wa Radio yao na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akiongea na wadau mbalimbali katika Secta ya Mawasiliano Tanzania
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akisikiliza maelekezo ndani ya Banda laMamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka katika Banda la CDS ambao wanahusika na usafirishaji wa Mizigo kwenda nje na ndani ya Nchi.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akipokea maelezo kutoka katika Banda la Shirika la Posta Tanzania
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Makame Mbarawa akipata Maelezo kutoka katika Banda la Stushi wanaohusika na Maswala ya ulinzi kutumia Teknolojia mpya.
Hawa ni wale Akina dada ambao walikuwa wakikaribisha wageni na kutoa maelezo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mkutano huo wa miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA
↧
↧
MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA MONDULI ASIMAMISHWA UONGOZI MARA MOJA
TAARIFA KWA UMMA
KUKOMA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA WILAYA YA MONDULI MCHUNGAJI AMANI SILANGA MOLLEL
Kwa niaba ya baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, napenda kuujulisha umma wote kwa ujumla kuwa mwenyekiti wa wilaya ya monduli Mchungaji Amani Silanga Mollel amekoma/amesimamishwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya monduli kuanzia tarehe 29 Novemba 2013 kufuatia tuhuma nzito za uvunjifu wa kanuni za maadili ya chama.
Hatua hii imefikiwa baada ya kuthibitika na yeyé mwenyewe kukiri mbele ya kikao cha kamati tendaji ya wilaya ya monduli kilichoketi tarehe 29 Novemba 2913 saa NNE asubuhi kuwa alitoa tamko batili akitumia wadhifa wa mwenyekiti wa wilaya bila ridhaa ya kamati tendaji na huku akidanganya kuwa ni tamko kwa niaba ya wilaya ya Monduli.
Katika tamko lake ametoa tuhuma dhidi ya wajumbe wa kamati kuu na viongozi wakuu wa kitaifa kwa maamuzi halali ya kikao cha kamati kuu huku akijua kuwa anavunja kanuni za chama kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka 2006 ya Kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (X) “Kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelezwa kwenye kanuni za chama”.
Sambamba na hilo, Mchungaji Amani Silanga ametoa tuhuma za uzushi, uongo na upotoshaji na kutaka kuaminisha jamii kuwa chadema ina makundi ya CHADEMA Asili na CHADEMA Family kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa na wa hatari kwa ustawi na umoja wa chama na kinyume na kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (VII), “Kiongozi anatakiwa kuwa mkweli na muwazi wakati wote hususani katika vikao halali na aachane na vikundi vya majungu, wadanganyifu (Rumour Mongers). Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi wa vikao halali”.
Kamati tendaji ya wilaya ilipomtaka aonyeshe CHADEMA asili ni kina nani na CHADEMA family ni kina nani alishindwa kutoa maelezo yoyote ya maana na kufikia hatua ya kutaka kuvuruga kikao kwa kuleta vijana wahuni wapatao 17 ndani ya kikao ambao wengi walijulikana kuwa sio WANACHADEMA. Katika utambulisho wake wa majigambo Mchungaji Amani SIlanga kwa kiburi na kejeli amejitambulisha na kukiri kuwa yeye yupo kambi ya Zito Kabwe na hakuna wa kumfanya kitu maana ni mjumbe wa baraza kuu la chama. Maneno yake yalidhihirisha kuwa Mchungaji Amani Silanga anashiriki mpango wa kuunda makundi yasiyo na tija ndani ya chama na hivyo kuwa kinyume na sura hiyo hiyo ya kumi ya kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10 (IX), “Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake”.
AZIMIO LA BARAZA LA UONGOZI LA MKOA WA ARUSHA:
Baraza la uongozi la mkoa lililoketi tarehe 29 Novemba 2013, limepokea mapendekezo ya kamati tendaji ya wilaya na kuzingatia hofu kubwa iliyoainishwa na kamati tendaji kufuatia matendo mengi yanayotia shaka ya uadilifu na uwezo wa kiuongozi wa Mchungaji Amani Silanga na hivyo baraza la uongozi la mkoa limeridhia kuwa amevunja kanuni za maadili ya chama sura ya KUMI ibara ya (VII) hadi (XII) na hivyo kupelekea ukomo wa yeye kuwa Mwenyekiti wa wilaya kuanzia tarehe 29 Novemba 2013. Baraza la mkoa likiwa mamlaka ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ibara ya 6.3.6 (a) (iv) limemjulisha tuhuma zake na hatua hii stahiki iliyochukuliwa. Kwa vile Mchungaji Amani Silanga alikiri kosa hili mbele ya kamati tendaji ya wilaya bila kulijutia au kuomba msamaha, baraza la mkoa limechukua hatua hii stahiki kwa maslahi ya chama na kuwa uchunguzi zaidi utafanyika ili kufikia maamuzi makubwa zaidi ya tuhuma nyingi kwa mujibu wa kanuni za hatua za kinidhamu.
Baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, linatoa onyo kwa wote ambao wapo katika mtandao huu mchafu, ama watoke wenyewe mapema maana hawatavumiliwa kamwe. Baraza la uongozi wa mkoa liliona kuwa Mchungaji Silanga amepotoka na hivyo yeyé kuendelea kuwepo ndani ya chama wakati wa uchunguzi wa tuhuma hizi nzito dhidi yake ni hatari zaidi kwa ustawi wa chama na hivyo baraza likaridhia kwa kuzingatia tafsiri ya katiba ya chama ibara ya 6.3.4 (c) wa yeyé kukoma uongozi na hivyo akae nje kwa muda na waliopotoka wenzake.
Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – Mkoa wa Arusha.
(Kwa niaba ya Baraza la Uongozi la Mkoa wa Arusha)
Tarehe 30 Novemba 2013
↧
AJALI YATOKEA IRINGA MJINI USIKU HUU
TAXI inayoegeshwa eneo la Posta mjini Iringa imegongwa vibaya eneo la Idara ya maji mjini Iringa usiku huu na watu kadhaa kunusurika kifo ajali hiyo imetokea mida ya saa 2.30 usiku huu hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Gapco mshindo kujeruhiwa
Hili ndilo gari lililosababisha ajali katika barabara kuu ya Iringa - Dodoma
CHANZO: FRANCIS GODWIN
↧
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DECEMBER 01, 2013
↧
↧
CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA
Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu Ali Omari. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;
Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama kuendelea.
Pili kuhusu suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;
1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.
Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanaCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa ndani ya chama, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo;
Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza
Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjar.o
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro.
Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama.
Hii ni kwa sababu maboresho yanayofanyika ndani ya chama, hadi sasa yanaendelea katika ngazi ya Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya, majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji.
Katika maboresho hayo, kwa nafasi za uteuzi, yanayoendelea sasa ambayo yanakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika.
Suala la maslahi ya watumishi wa CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na kisha kuridhiwa kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni.
Katika suala hili la maslahi ya watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu Chitanda amesema uongo mkubwa. Kusema kwamba Ofisa Mwandamizi anaweza kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika, ni uongo unaovuka mipaka.
Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; "800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs.6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=".
Pia si kweli kuwa kila mtumishi anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia chama na Watanzania kwa ujumla.
Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi na hata baada ya maboresho atapata posho kulingana na Mkurugenzi. Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji wa makusudi.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, restructuring inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika.
Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda. Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia.
Ndugu Chitanda anajichanganya sana katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kujaribu kuukana ukweli anaoujua moyoni. Tutatoa mfano mmoja;
Kupitia taarifa yake, anasema alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama kuna ubaguzi wa dini!
Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu.
Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza athibitishe kwa kutoa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu.
Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA.
Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini.
Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya CHADEMA ni msingi.
Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama, zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari.
Tungependa kumalizia ufafanuzi huu mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii yataandaliwa na kutolewa kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao.
Mathalani katika taarifa yake, Ndugu Ali Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi;
"Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda."
Aya hiyo pekee inayotumia lugha wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha uhalisia wa yeye mwenyewe (mtoa taarifa) alivyo.
Ni kauli za namna hii (kuwatisha na kutaka kuwatenganisha Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli.
Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
↧
EMMANUEL MSUYA ACHUKUA MILIONI 50 ZA EBSS YA 2013
Mashindano haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba, Makomando, Young Killer, Water Chilambo, Shaa, Kimbunga na Snura.
Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano ambao ni Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya, Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho.
Kinyanganyiro cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013 kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.
Katika round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana.
Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.
↧
TAZAMA HAPA MATOKEO YA MECHI YA LIGI YA UINGEREZA ZILIZOCHEZWA JANA NOVEMBER 30, 2013
↧
MUIGIZAJI WA FAST AND FURIOUS, PAUL WALKER AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI
Muigizaji wa Marekani, Paul Walker aliyekuwa akiigiza kwenye filamu ya Fast & Furious amefariki dunia kwa ajali ya gari California.
Msemaji wake ametoa taarifa ya kifo chake kupitia Facebook kudai Walker, 40, alikuwa amebebwa kwenye gari ya rafiki yake iliyopata ajali Kaskazini mwa jiji Los Angeles. Alikuwa akienda kuhudhuria tukio la utoaji misaada.

Paul aliigiza kwenye series za filamu ya Fast and The Furious ambazo hadi sasa ni sita. Walker pia ameigiza kwenye filamu iitwayo Hours, ambayo itazinduliwa mwezi huu. Mamlaka zimesema waliikuta gari hiyo ikiwaka moto na watu wawili waliokutwa kwenye gari hiyo walikutwa wamekufa tayari.

Gari alilopata ajali Paul Walker

↧
↧
HAWA NDIO WASHINDI WA TUZO ZA CHANNEL O ZILIZOFANYIKA JANA HUKO AFRIKA YA KUSINI
Wizkid bags the Biggest Award for The Night – Music Video Of The Year.
![]()
Lizha James FT Anselmo Ralph – Vais Rochar
STL – Stella Stella Stella
Tiwa Savage ft Don Jazzy – Without My Heart
Toya Delazy – Heart
All The Winners:
Most Gifted Music Video Of the Year – Wizkid (Winner)
Most Gifted Duo/Group Featuring Video
ZONE FAM – Winner
Tear gas – Wake Up
Xtatic/Aka & Priddy Ugly -Hit Em Up
Mi Casa – Can't Get Enough
EME – Baddest Boy
Naeto C FT D'Banj – Tony Montana (Bad Pass) Remix
Xtatic/Aka & Priddy Ugly -Hit Em Up
Mi Casa – Can't Get Enough
EME – Baddest Boy
Naeto C FT D'Banj – Tony Montana (Bad Pass) Remix
Most Gifted Newcomer Video
Khaya Mthethwa – Move – Winner
Most Gifted Female Video
Zonke – Feelings – Winner
Zonke – Feelings – Winner

Lizha James FT Anselmo Ralph – Vais Rochar
STL – Stella Stella Stella
Tiwa Savage ft Don Jazzy – Without My Heart
Toya Delazy – Heart
Most Gifted Male Video
Donald – Over The Moon
Zeus FT AKA & TUMI – #DatsWasup – Winner
Wizkid – Azonto
AY/Marco Chali – Party Zone
Iyanya – Flavour
Donald – Over The Moon
Zeus FT AKA & TUMI – #DatsWasup – Winner
Wizkid – Azonto
AY/Marco Chali – Party Zone
Iyanya – Flavour
Most Gifted Ragga/Dancehall Video
Buffalo Souljah – Basawine
Kaakie – Too Much
Jesse Jagz – Murder Dem
P-Unit FT Collo – You Guy (Dat Dendai) – Winner
Radio and Weasel – Can't Let You Go
Buffalo Souljah – Basawine
Kaakie – Too Much
Jesse Jagz – Murder Dem
P-Unit FT Collo – You Guy (Dat Dendai) – Winner
Radio and Weasel – Can't Let You Go
Most Gifted Hip Hop Video
Aka – Jealousy – Winner
Jayso & Sarkodie – Pizza & Burger
Reason – Do It Like I Can
Ifani ft Blaksuga – Chocolate Vanilla
EL/M.anifest – Hallelujah
Aka – Jealousy – Winner
Jayso & Sarkodie – Pizza & Burger
Reason – Do It Like I Can
Ifani ft Blaksuga – Chocolate Vanilla
EL/M.anifest – Hallelujah
Most Gifted R&B Video
Banky W – Yes/No – Winner
Anselmo Ralph – Curticao
Danny K – Brown Eyes
Chase – Lonely
Victoria Kimani/M.I – Oya
Banky W – Yes/No – Winner
Anselmo Ralph – Curticao
Danny K – Brown Eyes
Chase – Lonely
Victoria Kimani/M.I – Oya
Most Gifted Afro Pop Video
The Soil ft Zakwe – Linkomo – Winner
Sauti Sol – Money Lover
2Face Idibia – Ihe Ne Me
The Muffinz – Umsebenzi Wendoda
Davido – Gobe
The Soil ft Zakwe – Linkomo – Winner
Sauti Sol – Money Lover
2Face Idibia – Ihe Ne Me
The Muffinz – Umsebenzi Wendoda
Davido – Gobe
Most Gifted Dance Video
KCEE – Limpopo
MAfikizolo – Khona – Winner
Fuse ODG ft Wyclef Jean – Antenna (Remix)
DJ Malvado ft Petty – Jamaica
DJ Ganyani FT FB – Xigubu
KCEE – Limpopo
MAfikizolo – Khona – Winner
Fuse ODG ft Wyclef Jean – Antenna (Remix)
DJ Malvado ft Petty – Jamaica
DJ Ganyani FT FB – Xigubu
Most Gifted Kwaito Video
L'vovo Derrango ft Professor – Palesa
Professor ft Osikido & Character – Finger Prints. – Winner
EES – Woza December
Kabelo – Impilo
DJ Tira ft Big Nuz & Joocy – Summer Time
L'vovo Derrango ft Professor – Palesa
Professor ft Osikido & Character – Finger Prints. – Winner
EES – Woza December
Kabelo – Impilo
DJ Tira ft Big Nuz & Joocy – Summer Time
Most Gifted African (West) Video
D'Prince – Goody Bag
Ice Prince – Aboki
R2Bees – Life (Walaahi)
Dblack ft Joey – Vera
Chidinma ft Illbliss & Suspect – Emi Ni Ballar
P-Square – Alingo – Winner
D'Prince – Goody Bag
Ice Prince – Aboki
R2Bees – Life (Walaahi)
Dblack ft Joey – Vera
Chidinma ft Illbliss & Suspect – Emi Ni Ballar
P-Square – Alingo – Winner
Most Gifted African (East) Video
AY/Marco Chali – Party Zone
P-Unit ft Collo: You Guy (Dat Dendai) – Winner
Radio & Weasel – Can't Let You Go
Sauti Sol – Money Lover
Navio – Kata
AY/Marco Chali – Party Zone
P-Unit ft Collo: You Guy (Dat Dendai) – Winner
Radio & Weasel – Can't Let You Go
Sauti Sol – Money Lover
Navio – Kata
Most Gifted African (South) Video
Dama Do Bling – My Eish
Oskido – Tsa Mandebele – WinnerBlack Coffee ft Zakes – Take it All Off
Paul G ft Fabulous – Get Control
DJ Dimplez ft L-Tido & ANATii – We Ain't Leaving
Khuli Chana – Hazzadazmove
Dama Do Bling – My Eish
Oskido – Tsa Mandebele – WinnerBlack Coffee ft Zakes – Take it All Off
Paul G ft Fabulous – Get Control
DJ Dimplez ft L-Tido & ANATii – We Ain't Leaving
Khuli Chana – Hazzadazmove
Special Recognition Award – P Square
↧
ZITTO: URAIS, MABILIONI YA USWISI VINANIMALIZA
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.
Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?
Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.
“Matatizo yaliyopo ni mafanikio yangu, …. nadhani hii siyo vita kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, pengine magenge ya watu wanaotaka urais na wale walioficha fedha zao nje wamekaa pamoja wanaona tatizo lao ni Zitto… wanajua siwezi kusemea nje maana sina kinga…, hivyo wanataka kuniondoa bungeni…” alisema.
Aliongeza kuwa kwenye siasa kinachohitajika ni kusimamia misingi, jambo alilosema binafsi amekuwa akilifanya katika kipindi chake chote cha kisiasa.
Zitto alisema kuwa ni vyema wananchi wakawapima wabunge wao kwa kazi wanazozifanya bungeni akibainisha kuwa kati ya mwaka 2011 hadi 2013, yeye amewasilisha hoja nyingi nzuri zilizo na mashiko ikilinganishwa na wabunge wenzake wanaomtuhumu kutumiwa na CCM.
“Je, mbunge anayetumika na Chama Cha Mapinduzi anaweza kupeleka hoja ya kumng’oa Waziri Mkuu na kumshinikiza Rais mpaka akasimamisha kazi mawaziri wanane? Je, mbunge anayetumika anaweza kushikia bango watu wanaotorosha fedha nje ya nchi?” alihoji Zitto.
Tuhuma za usaliti
“Sizijui hizo tuhuma 11 kwa sababu nilichoelezwa kwenye kikao cha Kamati Kuu sicho kilichoelezwa na chama kwenye mkutano wake na waandishi wa habari… hivyo sijui kabisa hizo tuhuma zangu ni zipi mpaka sasa,” alisema.
Alisema kuwa kwenye Kamati Kuu alilaumiwa kwa masuala matatu. Akizitaja: “Nililaumiwa kuwa sifanyi kazi za chama, la pili kuwa nimemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali akague vyama kutokana na kuwa na nia mbaya na chama hicho. Tuhuma ya tatu ni ile ya kukataa kupokea posho bungeni ambapo nadaiwa kulenga kuwadhalilisha wabunge wenzangu.”
Zitto alisema kuwa baada ya kuzijibu tuhuma hizo mbele ya wajumbe wa kikao cha Kamati Kuu na katika mkutano wake na waandishi wa habari, akashangazwa na tuhuma alizoziita mpya kuwa anatuhumiwa kutokana na waraka ambao yeye hahusiki nao, licha ya kutajwa kuwa mfaidika tu.
“Mimi sihusiki na waraka wowote, huo unaodaiwa kusambazwa kwenye mitandao wala mwingine wowote… ni wajibu wa chama kueleza mimi nahusikaje na waraka ule,” alisema.
Madai ya Mwanasheria wa Chadema kuvunja Katiba
Zitto alisema jambo linalompa shaka kuwa huenda suala lake limelenga kumdhoofisha kisiasa ni kitendo cha mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu kuamua kuvunja katiba ya chama hicho kwa makusudi.
Alifafanua: “Katiba ya chama (Chadema), inasema kwamba kiongozi wa ngazi fulani ataondolewa kwenye uongozi na ngazi iliyomchagua. Mimi nilichaguliwa na Baraza Kuu la Chama, siyo Kamati Kuu… sasa iweje Kamati Kuu iniondoe?”
Alisema kimsingi Kamati Kuu haina mamlaka ya kumvua uongozi bali ina mamlaka ya kuweza kumsimamisha uongozi kusubiri kikao kilichomchagua kufanya uamuzi wa kumwondoa katika uongozi au kumrejesha.
Zitto alidai kuwa Lissu alisema uongo kuwa hata Dk Wallid Kabourou aliondolewa uongozi na Kamati Kuu na kwamba ukweli ni kuwa Dk Kabourou alijiondoa mwenyewe na kuhamia CCM na kwamba hata Chacha Wangwe hakuondolewa na Kamati Kuu isipokuwa alisimamishwa na kusubiri Baraza Kuu ambapo kabla ya Baraza Kuu kuketi alifikwa na mauti.
Kwa nini hapokei posho?
Alipoulizwa ni kwa nini yeye hapokei posho za wabunge alisema suala la posho siyo lake binafsi bali ni suala la imani na msimamo wa chama hicho, ambao waliuweka wakati wa kampeni na ni miongoni mwa mambo waliyowaahidi wapigakura wakati wa kampeni, hivyo yeye anachofanya ni kutimiza tu ahadi.
Aliongeza kuwa wakati wa kampeni za mwaka 2010, walikuwa wakiwaeleza wananchi kuwa wabunge wanapokea fedha nyingi na kuwa wakichaguliwa watapunguza posho hizo na kwamba Chadema ilipofanikiwa kushinda chama kilikubaliana watekeleze ahadi zile.
Alidokeza kwamba walikubaliana kutekeleza kwa kuanza na mambo mawili moja likiwa kukataa kuchukua posho za vikao, maana ni kinyume cha utaratibu na suala la pili ni kuacha kutumia shangingi la Serikali ambalo linatumika na Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
Alisema katika kutekeleza uamuzi huo Mbowe alitangaza hatua ya kurudisha shangingi na yeye (Zitto) kama Waziri Kivuli wa Fedha akatangaza kuacha kupokea posho.
“Tulikubaliana wote tutekeleze hayo… lakini wenzangu wakashindwa kuyatekeleza, na mwenzangu akalirudia gari na analitumia mpaka sasa… kwangu mimi mafunzo niliyofundishwa kisiasa ni kwamba unayoyasema, yatekeleze, wenzangu hiyo ‘principal’ ya kutekeleza wanayoyasema hawana,” alisema.
Kuhusu tuhuma kuwa anakataa posho lakini anapokea rushwa kubwa kubwa, Zitto alisema iwapo kuna mtu aliye na ushahidi na hilo aupeleke vyombo vya dola, wamshtaki na achunguzwe kisha achukuliwe hatua.
Alisema mbali na posho, wabunge wanaongoza kwa kupewa misamaha ya kodi mbalimbali ukiwemo msamaha wa kodi ya uingizaji wa magari.
“Hii nayo tulikubaliana kuikataa… na katika kulitekeleza hili, nilipoagiza gari langu nilikataa msamaha nikalipa kodi hadi nilipoitwa na Kamishna wa Kodi na kuulizwa iweje nilipe kodi wakati nina msamaha wa kodi nikamjibu kuwa ni suala la ‘principal’ tu,” alisema.
Ruzuku
Kuhusu suala la ukaguzi wa ruzuku ya chama, Zitto alisema yeye anapokuwa Mwenyekiti wa PAC anasimamia taifa, hasimamii chama, hivyo kwa nafasi yake ya PAC na kamati nzima waliona siyo halali vyama vya siasa kukaa bila kukaguliwa.
Alisema alipigania suala hilo tangu mwaka 2011 alipomwandikia barua Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kumuuliza kwa nini hakagui hesabu za vyama vya siasa wakati sheria inataka vikaguliwe.
Je, ana shaka kuhusu matumizi ya ruzuku ndani ya Chadema?
“Nitaweza kusema jambo hilo kwa uhakika baada ya ukaguzi kufanyika. Mpaka sasa hakuna chama ambacho kimekaguliwa, hivyo inawezekana matumizi mabaya ya ruzuku yako CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, Chadema au yako katika vyama vyote…
“Haiwezekani kila mwaka sisi (wabunge) tunaipigia kelele Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, haiwezekani kila mwaka tunaipigia kelele Bodi ya Korosho, halafu vyama vya siasa ambavyo vinapokea zaidi ya Sh29 bilioni kila mwaka, tukisema, tuonekane wasaliti,” alisema Zitto.
Chadema yajibu
Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Zitto, jana Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa alisema kuwa hawezi kulumbana na mtu kwa njia ya magazeti na kwamba kazi yake yeye ni kufafanua Katiba, kanuni na miongozo ya Chadema pindi inapohitajika. Anaripoti Ibrahim Yamola.
Alisema endapo kama kuna vifungu katika Katiba, kanuni au miongozo vilivyokiukwa katika kufanya uamuzi hayo vibainishwe na si kuongea katika magazeti bila kueleza makosa yaliyofanyika.
“Mimi kazi yangu si kulumbana katika magazeti, kama anaona (Zitto), kuna mambo yamekiukwa anatakiwa kuyawasilisha sehemu inayohusika ili hatua zaidi zichukuliwe.
Wewe mwandishi umeoa? (Mwandishi; hapana), ungekuwa umeoa ningekuuliza hivi; unaweza kutoa siri za ndani za mke wako kwa watu wengine?,” aliuliza Dk Slaa.
Akizungumzia kuhusu mikutano inayoendelea mikoani, alisema haina lengo la kuwaeleza wananchi juu ya uamuzi wa Kamati Kuu ya kuwavua madaraka Zitto na wenzake, bali ni utekelezaji wa mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho uliofikiwa Junuari mwaka huu.
“Mikutano hiyo imeanza tangu Aprili mwaka huu, iko katika ngazi za vijiji na vitongoji vikikijenga chama na wala si kwa dhana yoyote zaidi ya hiyo,” alisema Dk Slaa.
MWANANCHI
↧
TAZAMA HAPA MECHI ZA LIGI YA UINGEREZA ZITAKAZOCHEZWA LEO DECEMBER 01, 2013
↧
TAMKO LA UMOJA WA MATAWI YA WANACHADEMA MKOA WA MWANZA DHIDI YA UAMUZI HARAMU WA KAMATI KUU YA CHADEMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
UTANGULIZI
Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi wa matawi 189 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30 Nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30 Nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan katika kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki
Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama.
Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
1. Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
2. Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5. Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro
2. Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5. Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro
Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:
• Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama, waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya viongozi kanuni ya 10.
Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.
Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.
Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.
Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.
Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na jambo hili.
Hitimisho
Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.
Hitimisho
Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.
Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo utoke madarakani.
Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.
Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.
Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,
Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA
ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA
0757 084776
↧
↧
MARAIS WA AFRIKA MASHARIKI WASAINI MKATABA WA SARAFU MOJA EAC!
Head EAC signed the Monetary Union Protocol which will provide for a wide scope of co-operation in monetary and financial sectors among the EAC Partner States and will further catalyze trade growth within the region. We are now a people destined for greatness, prosperity and happiness. Our borders are fast becoming mere formalities. As we integrate, we cease to be a group of neighbouring nations, and become one people. Let us think with one mind, speak with one voice and walk on one road to our promised destination, “A better East Africa for all its citizens”. UHURU KENYATTA
SOURCE:JAMII FORUM
↧
PROFESA MWANDOSYA AMJULIA HALI FATHER MWANG'AMBA HOSPITALINI INDIA ALIKOLAZWA NAYE
↧
JOY KALEMERA NDIYE MSHINDI WA MISS TANZANIA USA PAGEANT
Mlimbwende Joy Kalemera akipungia mashabiki baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania USA Pageant yaliyofanyika usiku wa Jumamosi Novemba 30, 2013 kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom uliopo Silver Spring , Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ndiye aliyekua mgeni rasmi. Joy Kalemera alipohojiwa na Vijimambo alikua na haya ya kusema.
Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalamera akipewa maua na aliyekua Miss District of Columbia baada ya kutangazwa mshindi kwenye Miss Tanzania USA Pageant ambapo mashindano haya ya kumtafuta Miss Tanzania USA Pageant ndiyo ya kwanza kufanyika kwenye ardhi ya Marekani.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akiwa mwenye furaha baada ya kutangazwa mshinidi wa Miss Tanzania USA Pageant.
Balozi wa Tnzania nchini Marekani na Mexico akimvisha taji Joy Kalemera baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania Pageant
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa mwenye furaha baada ya shindano hili kufana sana na kuandika historia iliyobeba ukurasa mpya wa kutangaza Tanzania kwenye mashindano haya ya Miss Afrika USA Pageant ambayo Tanzania ilikua na mshiriki wa kwanza mwaka huu ambae ushiriki wake haukupitia ngazi hii.
Joy Kalemera akipongezwa na washiriki wenzake waliokua nae kwenye kinyang'anyiro hiki kilichoanzia miezi miwili iliyopita.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa kwanza katika historia ya Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera kulia ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.
Joy Kalemera katika picha ya pamoja na majaji pamoja na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant, Lady Kate (kulia)
Kutoka kushoto ni Faith Kashaa kutoka Alabama ambaye ndiye mshindi wa tatu, Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania mshindi wa pili, Joy Kalemera kutoka New Jersey Miss Tanzania USA Pageant, Julia Nyerere mshindi wa Tano na Namala Elias mshindi wa nne wakiwa kwenye picha ya pamoja
Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na washiriki wenzake.
↧
WAINGEREZA WA TINDIKALI WALIA NA SERIKALI
Picha za Katie Gee kabla (kushoto) na baada ya kushambuliwa na tindikali Zanzibar. PICHA | AFP
Dar es Salaam. Familia ya Waingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18, waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar, wameiomba Serikali ya Uingereza kuishinikiza Tanzania kuharakisha kuwawajibisha waliohusika na tukio hilo.
Waingereza hao ambao walikuwa walimu wa kujitolea katika shule ya St Monica, Tomondo, Zanzibar, walimwagiwa tindikali na watu wawili wasiojulikana wakati walipokuwa kwenye matembezi ya jioni katika eneo la Mji Mkongwe Agosti 7, mwaka huu.
Baada ya tukio hilo lililowajeruhi kiasi kikubwa katika maeneo ya kifua na mikononi, walipewa matibabu katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, kisha wakarudishwa kwao kwa matibabu zaidi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Alipowatembea wasichana hao hospitalini, Rais Jakaya Kikwete alisema tukio hilo limetia aibu kwa mataifa ya nje na kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika.
Taarifa iliyosambazwa kwenye mtandao wa habari wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) Kanda ya Tanzania, inaeleza kuwa familia ya wasichana hao hairidhishwi na namna Serikali ya Tanzania inavyolishughulikia suala hilo kwa kuwa hadi sasa imeshindwa kuwatambua wahusika.
Mtandao huo umemnukuu baba yake Trup, Marc alipokuwa akizungumza na Redio 4 ya BBC, kuwa kuna wingu zito lililotanda kuhusu kesi hiyo, kwa kuwa hadi sasa Serikali ya Zanzibar imeshindwa kuonyesha picha za wahusika ili zitambuliwe na wasichana hao, ingawa imekwisha kuwahoji watu kadhaa.
“Picha haziwezi kutumwa katika muundo bora unaokubaliwa na Interpol au Mamlaka za Uingereza, kutokana na sababu hizo hakuna hata mmoja ameshaziona hizo picha,” alisema Marc.
Naye baba mlezi wa Gee, Doug Morris, alisema: “Kama Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Jumuiya ya Madola wako makini kusaidia watu hao kufikishwa mbele ya sheria kwa niaba ya raia wa Uingereza, tulitegemea wafanye kila linalowezekana, lakini hakuna dalili zozote zinazoonekana za kutaka kuharakisha jambo hili.”
Aliongeza:“Kama wanamaanisha wanachokisema na ni muhimu kwao kuwatafuta waliotekeleza kitendo hicho ili wawafikishe kwenye vyombo vya sheria, basi watusaidie kwa kila njia ambayo wanaweza.
“Kila mtu ameanza kufikiri kuwa wanatuchezea, kila wiki tunakatishwa tamaa. Huu ni uharibifu ambao hauwezi kupita tu bila mtu kuadhibiwa kwa manufaa ya wasichana wale au mtu mwingine yeyote.
“Aina gani ya ujumbe unaoletwa, kwamba unaweza kufanya jambo baya halafu usifanywe kitu chochote?”
Alisema kuwa wangependa suala hilo lifike mwisho haraka iwezekanavyo ili haki itendeke.
Familia hiyo inasema kuwa hadi sasa haijafahamu sababu ya wasichana hao kushambuliwa kwa tindikali, kwa kuwa muda wote walipokuwa Zanzibar walionyesha tabia njema na kuvaa mavazi ya heshima.
Mzazi huyo wa Trup aliongeza kuwa: “Ninadhani mamlaka za Tanzania haziyachukulii masuala ya mambo ya nje ya nchi kwa umakini unaotakiwa, tunataka ifanye kazi.
“Wasichana wanataka kujua kama tukio lile lilitokana na rangi yao au dini kwasababu hawajui ni kwa nini lilitokea.”
Akizungumzia maendeleo ya afya ya binti yake, alisema kuwa Kirstie anaendelea vizuri na kwamba amesharudi chuoni kuendelea na masomo yake, ingawa bado anakwenda hospitali kupata matibabu.
“Anavaa vazi maalumu la kufunika makovu aliyoyapata, atafanya hivyo saa 23 kwa mwaka mzima. Ingawa anaendelea vizuri kimwili na kiakili, bado anapita katika kipindi kigumu,” alisema.
Akielezea maendeleo ya kiafya ya Katie, Morris alisema kuwa naye anaendelea na matibabu na kwamba hali yake inaendelea kuimarika.
Danadana za Polisi
Alipoulizwa maendeleo ya kesi hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alisema kuwa jalada la tukio hilo lipo Zanzibar, hivyo mwandishi awasiliane na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar kupata ufafanuzi.
Hata hivyo, alipopigiwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Mussa Ali Mussa simu zake zote mbili ziliita bila kupokewa. Alipotafutwa Ofisa Habari Mkuu Jeshi la Polisi Zanzibar, INSP Mohammed Mhina alisema kuwa kuna kesi nyingi za matukio ya watu kumwagiwa tindikali yaliyotokea Zanzibar ambayo yatatolewa ufafanuzi yote kwa wakati mmoja.
“Matukio ya kumwagiwa tindikali yapo mengi, hata hilo unalolizungumzia ninalikumbuka, ni vyema hayo yote yakazungumzwa kwa wakati mmoja,” alisema na kuongeza kuwa apigiwe simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, kwa kuwa ndiye anayelijua vizuri jambo hilo.
Kwa upande wake, Mkadam alisema suala hilo halipo tena mikononi mwake kwa kuwa lilishapelekwa kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Mwananchi lilimtafuta Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Yusuf Ilembo, lakini simu zake ziliita bila majibu.
Kauli ya Dk Shein
Akihutubia Baraza la Idd Fitr mwaka huu mjini Zanzibar, Rais wa visiwa hivyo, Dk. Ali Mohamed Shein, alisema serikali yake itahakikisha inawasaka na kuwafikisha mahakamani waliopanga na kufanya shambulio hilo.
↧
↧
MKAGUZI WA HESABU AKUTWA AMEKUFA
Mkaguzi wa hesabu katika Shirika la COASCO, Sabas Mlengela (54), amekutwa amekufa maji ndani ya mto, mjini hapa.
Walioshuhudia wamesema tukio hilo lilitokea jana asubuhi ambapo mwili wa mkaguzi huyo ulikutwa ukielea kwenye maji.
"Tulipofika katika eneo hili tuliona sikio la mtu ndani ya maji na baadaye tukabaini kuwa mtu amekufa akiwa na baiskeli yake na simu yake ilikutwa nje," alisema shuhuda mmoja.
Alisema simu hiyo ndiyo iliyotumika kuwapigia ndugu zake kuwajulisha tukio hilo.
Aliongeza kuwa kifo hicho kina utata huenda kilisababishwa na utelezi uliomfanya atumbukie kwenye daraja au watu wabaya walimsukuma.
"Kwa kweli tunashindwa kuelewa nini hasa chanzo cha kifo hiki, nadhani marehemu atakuwa ameuawa na kutupiwa kwenye maji na watu wabaya kwani haiwezekani mwili uwe majini halafu simu yake isiwe majini, na hawa waliomuua nadhani siyo vibaka kutakuwa na fitina fulani tu," alieleza shuhuda mwingine alijitambulisha kwa jina moja la John.
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Kihenya Kihenya, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulikutwa umezama kwenye mto huo pamoja na baiskeli yake, ingawa simu yake na kalamu vilikuwa vimeanguka pembeni mwa mto huo huku mwili wake ukiwa hauna majeraha yoyote.
Kamanda Kihenya alisema kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu, siku moja kabla ya tukio walikuwa pamoja na Sabas kwenye kikao cha kuvunja kamati, aliondoka saa 3 usiku na hakuonekana mpaka walipopata taarifa za kukutwa akiwa amekufa.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
↧
UPDATES:DK KITILA AVULIWA UONGOZI CHUO KIKUU
Dar es Salaam, Tanzania. Taarifa zilizotufikia, zimeeleza kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umemvua madaraka kwa muda, Dk Kitila Mkumbo kuongoza Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).
LEO imefahamika kwamba Dk Kitila amevuliwa madaraka hayo kwa muda usiojulikana baada ya uongozi wa chuo hicho kupata taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa ni kiongozi wa Chadema huku akiwa mtumishi wa umma.
Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, ni kinyume cha sheria cha nchi mfanyakazi wa umma kuwa kiongozi katika chama cha siasa.
Kutokana na uamuzi wa chuo hicho wiki iliyopita Dk Kitila alipewa barua ya kusimamishwa.
Baada ya uamuzi huo Dk Kitila ataendelea kuwa mhadhiri mwandamizi kwenye kitivo hicho.
Hivi karibuni Dk Kitila Mkumbo alivuliwa nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushiriki kuandika waraka wa badiliko ndani ya Chadema.
↧
MAGAZETI YA LEO JUMATATU DECEMBER 02, 2013
↧