Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all 16413 articles
Browse latest View live

SIKU YA UKIMWI DUNIANI, WANAUME WILAYANI HANDENI WAASWA KUPIMA AFYA ZAO ILI KUPAMBANA NA UGONJWA UKIMWI

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD Zuberi Chembera, wa pili kulia mwenye koti jeusi akionyesha ujuzi wa kusakata rhumba katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo kiwilaya, yalifanyika Kata ya Kwasunga, ambapoi alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alihudhuria majukumu mengine ya Kitaifa. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Handeni, Mr Mdoe, aliyesimama, akizungumza jambo katika madhimisho ya Ukimwi katika Kata ta Kwasunga, wilayani Handeni mkoani Tanga.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Kamanda wa Polisi wa Handeni, OCD Zuberi Chembera, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, ambapo kiwilaya yalifanyika katika Kata ya Kwasunga wilayani Handeni mkoani Tanga. Chembera alimuwakilisha DC Muhingo Rweyemamu.

WANAUME wametakiwa kujenga tabia ya kucheki afya zao badala ya kuwaachia akina mama peke yao, ikiwa ni njia ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi uliozimishwa leo Dunia nzima, huku kiwilaya ya Handeni, yakifanyika katika Kata ya Kwasunga, wilayani Handeni.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD Zuberi Chembera, akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wilayani hapa.

Akizungumza mbele ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo, OCD Chembera, alisema wanaume wengi hawapendi kupima afya zao, hususan kujua kama wameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi, badala yake wanasubiri matokeo ya wake zao.


 Wanafunzi katika shule ya Sekondari Kwasunga, wakiigiza mbele ya wahudhuriaji katika Maadhimisho ya Ukimwi duniani, katika Kata yao.
 Hapa wanafunzi wakiingia kwa ajili ya kuimba kwaya katika maadhimisho hayo. Hakika yalipendeza kupita kiasi.


OCD Chembera, hapa aliacha kiti na kuwasogelea kwa karibu wananchi kwa ajili ya kuzungumza nao juu ya ugonjwa Ukiwi.


Alisema inapotoke wake zao au wapenzi wao wamepata ujauzito, hugoma kabisa kwenda kupima afya zao, jambo linaloweza kukwamisha harakati za mapambano ya ugonjwa wa Ukimwi ndani nan je ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

"Wanaume tuacheni tabia za kuachia akina mama waende wakapimwe afya zao pale wanapopata ujauzito, maana hiyo si njia nzuri badala yake wote tuwe kitu kimoja na kuyapokea matokeo hayo kwa ajili ya kulinda afya zetu.

"Aidha ni wakati wa kila mmoja wetu kushirikiana kwa dhati katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao unaendelea kuangamiza ndugu zetu, japo kiwilaya maambukizi ya Ukimwi yanaonekana kupungua hadi asilimia 2,” alisema.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kwasunga, wananchi wengi walihuudhuria sambamba na kujionea burudani kutoka katika bendi ya Azimio pamoja na magizo kutoka kwa wanafunzi kwenye kata hiyo ya Kwasunga.

PICHA NA HANDEN YETU

MAMIA WAFURIKA KUSHUHUDIA BONANZA LA WAZI LA MASUMBWI NDANI YA KITUO CHA MABASI CHA MWENGE .

$
0
0

 Hawa ni wazee wa zamani ambao sasa ni walimu wa mchezo wa Ngumi, Wakati wao ndio walikuwa Mabondia Wakubwa
Wapigangoma wa Kikundi cha Ngoma ya Mchiriku cha Jagwa wakitumbuiza katika Bonanza la Masumbwi
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Mwimbaji wa Kundi la Jagwa akitumbuiza vilivyo katika Bonanza hilo la Masumbwi.
 Afisa habari wa Shirikisho la Ngumi Tanzania Salim Mwiduka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa Bonanza la wazi la ngumi.
 Mwenyeji wa Maandalizi ya Bonanza la Ngumi Kessy Juma akiwa anafungua Bonanza hilo.
 Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za ngumi Said Masanga akielezea juu ya Tuzo hizo za ngumi.
 Mjumbe wa Shirikisho la Ngumi wanawake Bi. Aisha George Vaniatis akiwa anafuatilia mpambano

Kulia ni Mwalimu mkongwe wa Mchezo wa ngumi bwana Rashid au anafahamika kwa jina la 
Super D

 Mpambano wa kwanza kati ya Gervas Rogiansion aliyevaa gloves nyekundu akipambana vikali na mpinzani wake John Christian aliyevaa Gloves za rangi ya bluu , ambapo John Christian aliibuka mshindi kwa Makonde mawili kwa moja.
 Umati wa watu waliojitokeza kutazama Bonanza la wazi la Ngumi katika kituo cha mabasi cha Mwenge
 Mashabiki wa Ndondi wakishangilia
 Mpambano wa pili  kati ya Haruna Swanga  aliyevaa gloves nyekundu aliyepambana vikali na na mpinzani wake Kulwa Makenzi  aliyevaa Gloves za rangi ya bluu , ambapo Haruna Swanga aliibuka mshindi kwa kumtandika mpinzani wake makonde matatu kwa sifuli.

 Mpambano wa tatu  kati ya George Costantino   aliyevaa gloves nyekundu aliyepambana vikali na na mpinzani wake Hamadi Furahisha   aliyevaa Gloves za rangi ya bluu , ambapo Hamadi Furahisha  aliibuka mshindi kwa kumtandika mpinzani wake makonde mawili kwa moja.
 Leonard Machichi aliyevaa gloves nyekundu akiwa anajikimu kukwepa ngumi kutoka kwa mpinzani wake Abuu Bakari wakati wa mpambano huo
 Abuu Bakari akipokea kipigo cha nguvu kutoka kwa mpinzani wake Leonard .. ambapo hali ilikuwa mbaya sana kwa Abuu
 Mwamuzi wa Mpambano huo Michael Mwamkenja akisimamisha mpambano huo katika Mzunguko wa pili baada ya Bondia Abuu kunyosha mikono juu ishara ya kushindwa .
 Leonard Machichi akitangazwa mshindi wa pambano hilo kali ambalo wanaliita RDT
 Makamu wa Raisi mpya wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania Lukelo Anderson au Man Power akiwa anatoa Neno la Shukurani Mara baada ya mpambano huo kuisha.
 Kutoka Kushoto ni Bi. Zuena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa Maendeleo ya Vijana na wachezaji katika Shirikisho la ngumi za Ridhaa Tanzania,Mutayoba Rwakatale Katibu wa maandalizi hayo, na Bondia Haruna Swanga. 
Picha zote na Dar es salaam yetu.


TAZAMA HAPA MATOKEO YA MECHI YA LIGI KUU YA UINGEREZA ZILIZOCHEZWA JANA JUMAPILI

$
0
0



ENDELEA KUSOMA MATOKEO ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA CHINI



HII HATARI SANA

$
0
0

UPDATES: MALORI YAGONGANA NA KUZIBA NJIA ENEO LA WAMI, MSAADA

$
0
0
 Malori yaliyogongana yakiwa yameziba njia baada ya kugongana eneo la mto wami.
Ajali mbaya imetokea muda huu eneo la mto wami na kusababisha Foleni kubwa sana kwa magari na mabasi yanayotumia njia hiyo, Blog hii imefanikiwa kupata picha kadhaaa za ajali hiyo, Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli breki kwa malori hayo yakiwa yanateremka kwenye mlima huo.Polisi wanaendelea na jitihada za za kuyatoa ili njia ipatikane kwa ukubwa zaidi ili kuruhusu upitaji mzuri wa magari.
 Foleni ni kubwa sana ya mabasi yaendayo mikoa ya Tanga, Arusha Na Kilimanjaro
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI




HAYA NDIYO MAKOSA 11 ANAYOTUHUMIWA ZITTO KABWE NA CHAMA CHAKE CHA CHADEMA

$
0
0



MASHITAKA 11 dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, yamebainisha kuwa kosa kubwa la kiongozi huyo kijana, ni nia yake ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Chanzo chetu cha habari kilichoona mashitaka hayo kabla ya kutumwa kwa washitakiwa, kimebainisha kuwa makosa saba kati ya makosa 11, yanahusu kugombea uenyekiti Taifa, au kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa.

“Ukiona hayo mashitaka yenyewe ndugu yangu, yanajirudia rudia na kuzunguka katika kosa moja la nia ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa… angalia kosa la kwanza, kosa la tatu, tano, sita nane na tisa, ni kama vile kuwania uenyekiti ndio kosa kubwa.

“Hata hivyo kwa jinsi mgawanyiko ulivyo ndani ya chama sasa, nakuhakikishia hawa jamaa (Zitto, Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba), watarudishwa katika nyadhifa zao na hakuna atakayeadhibiwa,” alisema mtoa taarifa wetu.

Alinukuu kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyehoji kama makosa wanayotuhumiwa akina Zitto ni makubwa kiasi cha kuyeyusha mema aliyoyafanya katika chama. “Si umesikia akina Baregu wakizungumza? Kwa mashitaka yale nakuhakikishia kitakachofanyika ni kufunika kombe mwanaharamu apite,” alisema mtoa habari wetu.

Kosa la kwanza kwa Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, wanadaiwa kuvunja Kanuni ya Chama inayokataza kukashifu chama, kiongozi au mwanachama yeyote. Katika maelezo ya kosa hilo, akina Zitto wanadaiwa kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.

Moja ya madai katika mashitaka hayo, ni kilichoandikwa katika Mkakati wa Mabadiliko 2013, kuwa Mbowe amekuwa akinunua vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambayo haihojiwi popote. Wanadaiwa pia wamemkashifu Dk Slaa kwa kudai ni mdhaifu kwa kumruhusu Mbowe kuingilia shughuli za kiutendaji.

Zitto na wenzake wanadaiwa katika kosa la pili, kutokuwa wawazi na wa kweli wakati wote na kushirikiana na vikundi vya majungu na udanganyifu kinyume na Kanuni za Uendeshaji kipengele cha 10.1 (VIII. 

Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).

Katika kosa la nne, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama, miongoni mwa jamii, kisiasa au kijamii. Katika kosa hilo wanadaiwa kwenda kinyume na kipengele cha 10.1 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.

Akina Zitto katika kosa la tano, wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya kuchonganisha na kuzua migogoro kwa viongozi wa chama au wanachama, kinyume na kifungu cha 10.1 (IX), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.

Katika kosa la sita ambalo mtoa habari wetu alisema ndio kubwa, Zitto na wenzake wanadaiwa kutekeleza mpango wa kusudio la kugombea uenyekiti wa Chama Taifa, bila kutangaza kusudio la kutangaza nafasi hiyo.

Hatua hiyo inadaiwa kuwa ni kinyume na kifungu 2.C cha Muongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi ya Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali wa 2012.

Zitto na wenzake katika kosa la saba, wanadaiwa kutengeneza mitandao ya kuwania uongozi ndani ya chama kwa nia ya kujihakikishia ushindi kinyume na kanuni ya 2 (D), ya Muongozo wa Kuwania Uongozi. 

Katika kosa la nane, Zitto na wenzake wanadaiwa kuwachafua viongozi na wanachama wengine wenye kusudio/nia ya kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti kinyume na kifungu 2 (E) cha Muongozo wa Kuwania Uongozi.

Katika kosa hilo, kumewekwa maelezo ya ziada kuwa kosa hilo linaunganishwa na kosa la kwanza ambalo washitakiwa wanadiwa kuwakashifu Mbowe, Dk Slaa na Lema.

Kosa la tisa, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na upinzani dhidi ya chama na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa chama, kinyume na kifungu cha 10.3 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji.

Kosa la kumi linamhusu Zitto peke yake, ambapo anaidaiwa kukashifu chama na kiongozi wa chama nje ya Bunge kinyume na kifungu 2 C (B), kikisomwa pamoja na kifungu 3 B cha Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Wabunge.

Katika hilo Zitto kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa chama yaani Dk Mkumbo na Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana, wanadaiwa kusambaza waraka uitwao Mkakati wa Mabadiliko 2013.

Mkakati huo, unadaiwa kukashifu chama na/ au viongozi wake wakuu kama ilivyoelezwa katika kosa la kwanza, tatu, nne na nane.

Mwisho katika kosa la 11, Zitto na wenzake wanadaiwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama kinyume na kanuni ya 3 F ya Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Bunge.

CHANZO: HabariLeo

DK. SLAA, MBOWE WAPIGWA MARUFUKU MWANZA

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, wamepigwa marufuku kukanyaga jijini Mwanza.



Pamoja na onyo hilo, pia viongozi hao wametakiwa kufanya kila wanaloweza ili aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka, warudishwe madarakani ndani ya siku nne kuanzia jana.

Kauli hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya CHADEMA, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Gwanchele, yeye na wenzake wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa wanapinga kitendo cha kuvuliwa madaraka kwa viongozi hao kwa kuwa kilifanyika kinyume cha Katiba ya chama hicho.


“Pamoja na kuwapiga marufuku kukanyaga mkoani Mwanza viongozi hao wa kitaifa, kama Zitto, Dk. Mkumbo Kitila pamoja na Samson Mwigamba wasiporejeshwa madarakani, hadi Desemba 4 mwaka huu, vijana Kanda ya Magharibi tutaandaa maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza Dk. Slaa na Mbowe wajiuzuru ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.


“Chadema tumeingiliwa na mdudu aitwae ubinafsi kwani kuna baadhi ya viongozi wa chama ni makuwadi wa viongozi wetu wa ngazi za juu kufanya wanayotaka bila kuchukuliwa hatua.

“Chadema ni chama kinachojali watu wa upande fulani wa nchi, hivi viongozi kama Godbless Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) pamoja na Kileo ambao waliamua kumshambulia Zitto kupitia mitandao ya kijamii wamechukuliwa hatua gani na chama?.

“Tutahakikisha tunawaondoa viongozi wote wa ngazi za juu kwa nguvu ya umma kwani Chadema sio mali ya mtu binafsi, chama hiki nicha wanachama.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Hatutaki kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi, hao wanapaswa kukaa pembeni kwanza kupisha uchunguzi na kama hawataki kupisha nguvu ya umma itawaondoa na ndio maana sisi vijana wa Kanda ya Magharibi, tumeamua kuwapiga marufuku Mbowe na Dk. Slaa wasikanyage Mwanza kwani wao tayari wameamua kujijengea himaya yao isiyoguswa katika mikoa ya kaskazini, sasa Mwanza wanakuja kutafuta nini.

“Mbowe na Dk. Slaa ni watuhumiwa hawapaswi kuendelea kuwa viongozi wa Chadema, hao wanapaswa kujiondoa ili nao wachunguzwe juu ya matumizi mabaya ya fedha za chama,” alisema Gwanchele.

Pamoja na kuwashambulia Mbowe na Dk. Slaa, Gwanchele pia aliwarushia kombora wabunge wa Chadema wanaotoka Mkoa wa Mwanza kwa kile alichosema nao wameshiriki katika kuvuliwa madaraka kwa Zitto, Dk. Kitila na Mwigamba.

Kutokana na hali hiyo, alisema wabunge hao, Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana) na Salvatory Machemli (Ukerewe), wamepoteza uhalali wa kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

“Wabunge wa chadema Mkoa wa Mwanza hivi sasa wanajiona wako juu ya chama na wamekuwa wakitoa matamko ya kuunga mkono kuondolewa kwa Zitto na wenzake wakati sisi wananchi hatukuwatuma kufanya hayo.

“Kwa hiyo, nao wanapaswa kuondolewa madarakani mara moja kwa usaliti wao kwa wapiga kura wao,”alisema.


BAVICHA Arusha

Wakati Mwanza wakisema hayo, Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Mkoa wa Arusha, limewataka Zitto, Dk. Kitila na Mwigamba, kuacha tabia ya kulalamika mitaani, badala yake wawasilishe malalamiko yao ngazi husika.

Akizungumza na Rai Jumatatu jijini hapa jana, Mwenyekiti wa BAVICHA, Mkoa wa Arusha, Efatha Nanyaro, alisema uamuzi wa kuwavua madaraka viongozi hao, ulikuwa sahihi.

“Kwanza sisi tunaunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu japokuwa tangu viongozi hao wavuliwe uongozi, kumekuwa na malalamiko na taarifa nyingi za upotoshaji.

“Tunawaambia wasilalamike mitaani bali wapeleke malalamiko yao Baraza Kuu au wasubiri mkutano mkuu kuliko kulalamika pembeni.

“Pamoja na hayo, naamini kama watapeleka malalamiko yao mbele ya Baraza Kuu, bado siamini kama kikao hicho kinaweza kuja na uamuzi tofauti na ule uliotolewa na Kamati Kuu wa kuwavua uongozi,” alisema Nanyaro.

Nanyaro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi, alisema taasisi yoyote inayoogopa kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wake wanaokiuka taratibu zilizowekwa, itakuwa taasisi dhaifu na haifai kuwapo. 

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, amesema chama hicho hakiwezi kufa hata kama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, atakihama.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo wakati Zitto ameshaweka wazi, kwamba hana mpango wa kukihama chama hicho na kwamba wanaotaka akihame, wamuondoe wao. 

Zitto alitoa msimamo huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Katika mazungumzo yake na Rai Jumatatu yaliyofanyika juzi, Dk. Slaa alisema Chadema ni taasisi yenye watu wengi na hivyo hakiwezi kuathirika kwa namna yoyote ile hata kikiondokewa na kiongozi maarufu.

Dk. Slaa aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza kwa simu na Rai Jumatatu.

“Chadema ni ya Watanzania, hivi Dk. Slaa akifa leo Chadema itakufa?, sasa chama kitaathirika vipi kwa kuondokewa na mtu mmoja wakati kuna mamilioni ya Watanzania wanaokimiliki kuanzia kwenye misingi ya chini?.

“Watanzania wanachopigania ni ukombozi wao, Chadema ndiyo mkombozi wao,” alisema Dk. Slaa kwa kifupi.

Kuhusu mashitaka 11 yanayowakabili Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, alisema barua hizo zilishatoka kwake hivyo hawezi kuzisemea na wenye mamlaka ya kuyasema mashitaka hayo ni wao wenyewe.

Akizungumzia kuhusu Zitto kujitetea mbele ya Kamati Kuu kabla ya kuvuliwa nyadhifa zake, kuhusiana na waraka anaotuhumiwa kuuandaa, alisema ni suala la ndani ya vikao vya chama.

“Alikuwepo kwenye kikao, lakini mambo mengine ya kikao ni mambo ya ndani, Katibu Mkuu ni Katibu wa vikao na Chadema anazungumzia taifa, hazungumzii mtu mmoja mmoja.

“Kuhusu huo waraka, mimi nina nyaraka nzito sana huo waraka mnaouona wa maana ni takataka tu, na ninaona upuuzi kushughulikia mambo ya kipuuzi kama hayo,” alisema Dk. Slaa.

RAI

PAUL WALKER ALIKUWA KIPENZI CHA WENGI, MASTAR MBALIMBALI DUNIANI WAOMBOLEZA KIFO CHAKE NA KUANDIKA UJUMBE KWENYE TWEETER NA INSTAGRAM ZAO ZISOME HAPA

$
0
0
Kifo cha star wa Hollywood Paul Walker kilichotokea Jumamosi iliyopita (Nov 30) kimewagusa watu wengi kutokana na jinsi ambavyo star huyo wa Fast and Furious alivyokuwa akipendwa.

Ukitembelea mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram, Facebook, Twitter na mingine asilimia kubwa ya post za watu mbalimbali wakiwemo maarufu kutoka Tanzania na nje pia kuanzia jana zinahusu jinsi ambavyo wameshtushwa na kifo cha Walker.

Hizi ni baadhi ya tweets, pamoja na post za mastaa mbalimbali wa nje
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI 


Rapper The Game aliweka picha ya Paul Walker Instagram na kuandika:

“Sad news about a dear friend. @PaulWalker, one of the best actors & for damn sure a great friend to me & I’m sure everyone else died today in a fiery car crash. This saddens me & is a definite reminder of how short life is. When I woke up this morning this is definitely not what I thought I’d have to post at some point during the day. My sincerest condolences & prayers are with his entire family…… A TRUE FRIEND was lost today & will be missed. Rest In Peace Paul………….”
Your humble spirit was felt from the start, wherever you blessed your presence you always left a mark,… http://t.co/nUiPPIU9Bb

Aliyekuwa mtu wa karibu wa Walker katika movie ya Fast and Furious, Vin Diesel, pia alipost picha ya swahiba wake Instagram na kuandika:

“Brother I will miss you very much. I am absolutely speechless. Heaven has gained a new Angel. Rest in Peace”.

Rapper T.I pia alipost picha yake na Walker na kuandika:
 

T.I na Paul Walker

“I am shocked & saddened to find that the world has lost such a great spirited person. Paul was not only a passionate, talented, actor, he was also a sincere man with a genuine personality that filled a room immediately upon introduction. My family’s hearts & prayers are extended to his family, especially his daughter. May he rest in peace. Through all his many actions & efforts his legacy lives on. He will never be forgotten”.

Tyrese ambaye ni co-starring wa Walker katika Fast and Furious alishare picha wakiwa pamoja na kuandika:
 

Tyrese & Paul Walker

“My heart is hurting so bad no one can make me believe this is real Father God I pray that you send clarity over this cause I just don’t understand My heart hurts it’s broken no one can convince me that this is real…. Prayer warriors please pray real hard for his only child, his daughter and family… #HeartOfAnAngel13YrsFamilyForeverWeJustCelebreatedYour40thBirthday….. My God… My God… I can’t believe I’m writing this.”

KHAAAH!!! HAMA KWELI TANZANIA KUNA VIPAJI VINGI MTIZAME PUNGO KIPINGE AKONESHA KIPAJI CHAKE

$
0
0
 Huyu ndiye Pungo  Kipinge kijana mwenye kipaji cha hali ya juu 
Sasa kazi imeanza kama unavyojionea hakuna kuigiza hapa huu ndio ukweli wa kudhihirisha kipaji kikubwa alichonacho kijana Pungo  Kipinge na hapo kumbuka yuko juu ya meza.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Pungo  Kipinge akiwa amejikunja kama hana mifupa vile
Wengine wanaweza kusema Pungo  Kipinge anavunjika kumbe yeye hapo yuko vizuri
Sasa kijana Pungo  Kipinge analamba moto hii weka mbali na watoto maana unaweza kuuguza mtoto hositalini mwaka mzima

TEKNOLOJIA YA MIWANI KWA WASIOONA YAVUMBULIWA

$
0
0
NOOR SHIJA 
Kwa miaka mingi, watu wenye ulemavu wa kuona, wasioona kabisa na wale wenye uono hafifu, wengi wao wamekuwa wakitumia fimbo maalumu (white cane) kwa ajili ya kutambua vitu vilivyo mbele yao.
Hata hivyo, mwanasayansi Dk Stephen Hicks wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza, amegundua teknolojia mpya ya miwani inayowawezesha watu wenye ulemavu wa kuona kutambua vitu vilivyo mbele yao, maandishi kwenye mabango na majina ya mitaa kupitia miwani maalumu iliyopewa jina la ‘Smart Glasses.’
Kwa mujibu wa Dk Hicks, teknolojia hiyo mpya inafuatia teknolojia nyingine ya miwani, ambayo humwezesha mtu mwenye ulemavu wa kuona, kupata picha ya vivuli ya vitu vilivyo jirani naye, ikiwemo binadamu.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Hata hivyo, Dk Hicks amekuja na uvumbuzi mwingine wa ‘Smart Glasses’ inayomsaidia mtumiaji kujiongoza mwenyewe katika maeneo ambayo hayafahamu kwa kusoma vibao vya maelekezo, kama vile majina ya mitaa na vituo vya basi.
Dk Hicks anasema kuwa miwani hiyo inamfanya mtu mwenye ulemavu wa kuona kuweza kujitegemea kwa kiwango kikubwa, ikiwemo kufahamu maneno yaliyoandikwa kwenye mabango ya matangazo, mitaa na orodha ya vyakula hotelini.
Kwa mujibu wa teknolojia hiyo ya Dk Hicks, miwani hiyo imetengenezwa kwa kuwekwa kamera ambazo zinarekodi picha, yakiwemo maandishi na kuyatambulisha kwa sauti kwa mtumiaji. Mfano, orodha ya vyakula hoteli, miwani hiyo inarekodi maneno na kuyatamka kwa sauti kwa mtumiaji.
Dk Hicks anasema kuwa miwani hiyo itasaidia maelfu ya watu wenye ulemavu wa kuona kuweza kumudu kufanya shughuli zao bila utegemezi wa watu wengine, ikiwemo kufahamu maelekezo yanayotokana na mabango ya barabarani, hasa majina ya mitaa na vituo vya mabasi.
Zaidi ya miaka mitatu, Dk Hicks amekuwa akitengeneza miwani hiyo ali yoweka kamera na programu inayomsaidia mtumiaji kubaini kitu na miwani hiyo inamtamkia kwa maneno.
Ulemavu wa macho ni hali ya kukosa kuona kutokana sababu zinazohusiana na mishipa, kuna viwango mbalimbali vimetengenezwa ili kuelezea kiwango cha kukosa kuona, ambapo upofu kamili ni ukosefu kamili wa kuona maumbo na mwanga na hurekodi kliniki kama NLP, kifupishi cha “No Light Perception” au kukosa kuona mwanga.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa macho, watu wenye ulemavu huo ambao macho yao bado hayajaharibika, wanaweza kutambua kukiwa na mwanga ingawa hawaoni kwa ukamilifu. Ishara za mwanga za lengo hili husafiri kupitia njia ya ‘retinohaipothalamia,’ kwa hivyo mishipa ya jicho iliyoharibika kupita mahali ambapo njia ya ‘retinohaipothalamia’ hutokea kwenye jicho siyo kizuizi.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaeleza kuwa visababishi vya upofu wa kawaida duniani kote katika mwaka 2002 vilikuwa mtoto wa jicho asilimia 47.9, glakoma asilimia 12.3, kuzorota kwa seli kunakohusiana na umri asilimia 8.7, konea kutopitisha nuru asilimia 5.1 na kuharibika kwa retina kunakosababishwa na ugonjwa wa kisukari asilimia 4.8, pia upofu tangu utotoni asilimia 3.9, trakoma asilimia 3.6 na onkoseresiasisi asilimia (0.8).
Kulingana na suala la maambukizi ya upofu duniani, idadi kubwa ya watu katika nchi zinazoendelea na uwezekano mkuu wao kuathiriwa unamaanisha kuwa visababishi vya upofu katika maeneo hayo ni muhimu zaidi kiidadi.
Mtoto wa jicho husababisha zaidi ya kesi 22,000,000 za upofu na glakoma kesi 6,000,000, wakati ukoma na onkoseresiasisi husabaisha kupofuka kwa takriban watu 1,000,000 duniani kote.
Idadi ya watu, wanaokuwa vipofu kutokana na trakoma imeshuka kwa kasi katika kipindi cha miaka 10 kutoka milioni sita hadi milioni 1.3, hivyo basi kuiweka katika nafasi ya saba kwenye orodha ya visababishi vya upofu duniani kote.
Xerophthalmia (ukavu wa macho), inakadiriwa kuathiri watoto milioni tano kila mwaka; 500,000 hupata konea inayofanya kazi, na nusu yao huwa vipofu. Vidonda vya konea pia ni kisababishi kikubwa cha upofu wa jicho moja duniani kote na uhusishwa na kesi zinazokadiriwa 850,000 za upofu wa konea kila mwaka katika eneo la nchi ya India peke yake. Kutokana na hayo, kuharibika kwa konea kutokana na sababu zote sasa ndiyo sababu ya nne kuu ya upofu kimataifa (Vaughan & Asbury’s General Ophthalmology).
Watu katika nchi zinazoendelea wanaweza kuathiriwa zaidi na upofu kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiwa au kutibiwa wakilinganishwa na wenzao katika mataifa yaliyoendelea.
Ingawa kuharibika kwa macho huwaathiri sana watu waliozidisha miaka 60 katika maeneo yote, watoto walio katika jamii maskini wanaweza kuathiriwa sana na magonjwa yanayosababisha upofu wakilinganishwa na wenzao kutoka jamii tajiri.
MWANANCHI

PICHA YA LEO: WEKA KICHWA CHA HABARI KWENYE PICHA HII

$
0
0

TAMKO LA KIKAO CHA MKOA – CHADEMA - KIGOMA

$
0
0
PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  1. Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013
 
-      Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama.
 
-      Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa
 
-      Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
 
-      Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
 
-      Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 
i.             Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. 

Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
 
ii.            Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
 
iii.           Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.
 
iv.          Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
 
v.            HOFU/TAHADHARI -   Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.

Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu. Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.
   
LENGO KUU:  NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
 
Asanteni
  
                                               
ALHAJ. JAFARI KASISIKO                                           MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA                        01/DEC.2013                KATIBU MKOA
0756439200                                                                0786448443
0714439200                                                               0756448442
 
  
CHADEMA MKOA KIGOMA
 
 


WAZIRI MKUU THAILAND AKATAA MADAI YA WAANDAMANAJI KUJIUZULU

$
0
0

Mabomu ya machozi yakiwa yanapigwa katika mitaa ya Bangkok. 
 Raia huyu akirusha bomu la machozi kwa askari lililorushwa upande wao 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



Wapinzani wakijaribu kuvamia ofisi ya waziri mkuu. 
Vikosi vya tiba vikiwasaidia waliojeruhiwa katika maandamano.

WAZIRI Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amekataa madai ya waandamanaji wanaomtaka ajiuzulu akisema hilo haliwezekani chini ya katiba ya sasa nchini humo, lakini akasema yuko tayari kwa mazungumzo.
Maandamano makubwa leo yalifanywa na wananchi ambapo walijaribu kuivamia ofisi ya waziri mkuu huyo katika mapambano ambayo tangu yaanze watu wane wamekufa katika machafuko hayo ya kisiasa.
Waandamanaji wanaoipinga serikali wamemtaka Bi Yingluck kujiuzulu, ambapo mpinzani wake, Suthep Thaugsuban, amempa siku mbili kufanya hivyo.  Waandamanaji wanataka serikali ichukuliwa na “Baraza la Umma” wakidai serikali ya Yingluck inaongozwa na kaka yake ambaye aliangushwa, Thaksin Shinawatra.
CHANZO BBC NEWS

UAMUZI WA SHTAKA LA SHEIKH ISSA PONDA KUTOLEWA DESEMBA 11, 2013

$
0
0




MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imesema itatoa uamuzi wa kuliondoa shitaka la kukaidi amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam au la dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda Desemba 11, mwaka huu.
Umuzi huo ulitolewa leo na Jaji  Rose Teemba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhusu maombi ya marejeo ya kupinga kuondolewa shitaka hilo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Sheikh Ponda.
Kabla ya uamuzi huo kutolewa upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Benard ess Zakaria, walidai kuwa wanapinga maombi hayo kusikilizwa kwa sababu kiapo kilichoambatana nayo kinamapungufu ya kisheria.
Kongola alidai kuwa kiapo kinabeba hoja za maneno ya maombi hayo na kwamba kama kimekosewa yatakuwa batili hayafai kusikilizwa na mahakama yatupwe.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


“Katika hati ya kiapo hicho hakuna baadhi ya vipengele ikiwemo tarehe ya kuwasilisha kiapo na muapaji aliapa kwa mtu anayemfahamu au alitambulishwa na nani… kosa hilo haliwezi kurekebishika kwa hiyo maombi yaliyopo mbele yako Mtukufu Jaji ni batili” alidai Kongola wakati akitoa hoja za kupinga maombi ya Ponda yasisikilizwe.
 Akifafanua zaidi wakili huyo alidai kuwa Jamhuri inapinga maombi hayo kusikilizwa kwa sababu yamekiuka kifungu namba 8 cha sheria inayosimamia viapo.
 Akijibu hoja za Jamhuri, wakili wa utetezi Juma Nassoro alidai kuwa pingamizi la Jamhuri halina misingi ya kisheria na kwamba kiapo kinaonyesha maombi yaliwasilishwa Oktoba 10, mwaka 2013.
Juma alidai kuwa aliyekula kiapo hicho ni Obadia G. Hamidu na mtoa kiapo aliyetajwa kwa jina moja, Kifunda ni wakili anayemfahamu muapaji vizuri na kwamba hoja za utetezi ni sahihi kwa mujibu wa kifungu namba 8 cha sheria inayosimamia viapo.
Baada ya mabishano hayo ya kisheria Jaji Teemba alisema uamuzi wake utatolewa Desemba 11, mwaka huu.

CHANZO: MICHUZI BLOG

MJUE MNYAMA NGIRI NA MAISHA YAKE

$
0
0


Ngiri ni Mnyamapori mtukutu huwasumbua wakulima wa mihogo na viazi vitamu hivyo hulazimika kuwindwa lakini huweza kukimbia kwa kasi kati ya kilometa 48 kwa saa kwa urefu wa  mita 200 mwendo ambao ni wa kasi zaidi kuliko wanariadha yeyote duniani.
Ngiri ana pua kubwa,macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi uliopinda au ulionyooka.Huwa  ana mwili mkubwa,miguu mifupi na nywele zilizojiviringisha.Ana kwato nne kwa kila mguu,mbili ni kubwa za mbele zikitumika kutembelea.

Ngiri huweza kuzaa msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropic,lakini hasa misimu ya mvua.Ngiri jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18 kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba.Ngiri dume huweza kushiriki maswala ya uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka 10.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Kwa uzao mmoja,wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12waitwao vibwagala kasha kuachishwa kunyonya,familia mbili au tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana

Kitaalamu Ngiri wanaopatikana  hapa  nchini  wanaitwa Phacochoerus africanus massaicus ambao.

Ngiri wana umbo lenye manyoya machache na urefu wa mita 1.5,wanasimama kwa urefu wa kwenda juu kwa kati ya sentimita 63.5 na 85 hadi mabegani pia wanawastani wa uzito wa kilo 45 hadi 75 kwa majike na kilo 60 hadi 150 kwa madume.
Miguu ya Ngili ina mifupa migumu iliyounganishwa na misuli yenye  nguvu ambayo hufanya kazi ya kuchimba,kuruka na kukimbia kwa mlipuko kutokana na uwezo wa kukunjika na kunyooka haraka.
Ili kupata mwendo kasi wa juu Ngili hunyoosha kichwa mbele na mkia juu ili kuweza kuuweka mwili sawa na kuimarisha mwendo asianguke.
Ngiri hawana tezi za jasho hivyo hujipoza kwa kutumia maji au matope wakati wa joto kali.Pia hutumia matope  kama njia ya kujikinga na kuunguzwa na jua.Zaidi matope huzuia wasiathiriwe na inzi na wadudu.


Utalii hususani wa wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.

CHANZO: MALIASILI ZETU

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DECEMBER 03, 2013

$
0
0





ENDELEA KUSOMA MAGAZETI KWA KUBOFYA HAPA CHINI














TRAIN ILIYOUA WATU 4 NA KUJERUHI 60 NEW YORK SIKU YA JUMAPILI NDIYO HII HAPA

$
0
0

Train iliyoua watu wa nne na kuacha majeruhi 60 na change NY katika eneo la Bronx NY,  Chanzo cha ajali hii inasemekani ni speed na mbaya zaidi ilikuwa kwenye corner. Ni mtihani wa kwanza kwa Mayor mpya wa New York Bill de Blasio. Train hii ni moja ya train zinazojulikana kwa jina la Metro North, Metro North ni tofauti na zile  train za ndani ya Jiji zinazofanya kazi 24/7 maarufu kwa jina la subway zinazopita chini ya ardhi. Train za Metro North utumiwa zaidi na watu wanaoishi nje ya NY lakini ufanya kazi zao ndani ya NY. Tunashukuru hadi sasa hatujasikia kama kuna mtanzania yeyote alikuwa ndani ya train hii kwani wapo ndugu zetu pia wanaotumia usafiri wa train hizo za Metro North kuingia na kutoka ndani ya jiji la NY.
Wafanyakazi wa zima moto wakiwakazini 

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Mayor mpya wa New York  Bill de Blasio baada ya Mayor Bloomberg.
Blizzard: Travelers carry their luggage through a snow bank on 7th Avenue in front of Penn Station after a snow storm in New York December 27, 2010 - the storm wreaked havoc across the city and Mayor Bloomberg was vacationing in Bermuda at the time
Kati ya vitu atakavyo kumbana navyo Mayor mpya ni kama hivi snow ikianguka kuhakikisha inaondolewa ontime na kupunguza kero za wakazi wa jiji la wasiolala New York City. Hii ilikuwa kali ya mwaka ilitokea 2010 na kusababisha watu kutokwenda kazini kwa 2 days kwasababu ya snow kumwagika na kusababisha kutokuwa na shughuri zozote ndani ya jiji la NY.

MABADILIKO UPINZANI BUNGENI, MAWAZIRI VIVULI MIZIGO KUTOSWA

$
0
0

Dodoma, Rukwa, Kigoma. Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.
Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe iliagiza kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitilla Mkumbo kwa kile kilichodaiwa ni kukisaliti chama.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwa mujibu wa habari hizo, katika Mkutano wa 14 wa Bunge unaoanza leo, kambi rasmi ya upinzani imepanga kumvua rasmi Zitto nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha.
Jana, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alithibitisha kuwapo kwa mpango wa mabadiliko hayo na kwamba yanatarajiwa kufanyika kati ya mwishoni mwa wiki hii na mwanzoni mwa wiki ijayo.
“Tutakaa mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo kwa sababu Kiongozi wa Kambi (Freeman Mbowe), atafika bungeni Desemba 6, mwaka huu na ndiye Mwenyekiti wa Baraza Kivuli,” alisema Lissu na kuongeza:
“Mbali ya Zitto kuna Said Arfi (Mbunge wa Mpanda Mjini) ambaye amejiuzulu nafasi zake zote ikiwa ni pamoja na Waziri Kivuli wa Uchukuzi na tutaangalia ufanisi wa mawaziri wengine kivuli”.
Baraza kivuli linaundwa na mawaziri 18 wakiongozwa na Mbowe na Zitto aliyekuwa Naibu wake na Manaibu saba.
Kujitoa kwa wanachama
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, alisema angeogopa kama kungekuwa na wimbi la wanachama zaidi ya 1,000 kuondoka katika chama kupinga misingi ya chama.
“Lakini kama walimfuata Zitto ndani ya chama ni ruksa sisi hatuna shida lakini kama ni chama hapo kuna la kuangalia… Sisi tunaamini wanachama wetu hawafuati mtu, bali misingi,” alisema.
Kuhusu suala la Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi, Ally Omary Chitanda, aliyejiondoa Chadema, Lissu alisema kiongozi huyo aliondoka katika chama hicho baada ya kuona anapoteza masilahi yake.
“Huyu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Lindi, wakati huohuo alikuwa ni ofisa anayetumikia makao makuu jambo ambalo lilileta mgogoro kwa wanachama,” alisema Lissu.
Aliongeza: “Yeye alitakiwa kuachia nafasi ya ofisa wa chama Makao Makuu kwa sababu wanachama walikuwa wakilalamika kwamba anakaa Dar es Salaam wakati yeye ni Mwenyekiti Lindi”.
Dk Slaa kutua jimbo la Zitto
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema atafanya ziara ya kukijenga chama mkoani Kigoma licha ya kuwapo taarifa inayomzuia kwa madai kwamba hali ya usalama kwa viongozi wa kitaifa kwenda huko kwa sasa si nzuri.
Hatua ya Dk Slaa imekuja wakati kukiwa na taarifa kwamba wafuasi wa Chadema mkoani humo wamekasirishwa na kuvuliwa madaraka kwa Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Jafar Kasisiko alisema uchunguzi wao unaonyesha kuwa watu wengi mkoani humo wamejenga uhasama na uongozi wa juu kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutoridhika na uamuzi wa Kamati Kuu dhidi ya Zitto.
Hata hivyo, Dk Slaa alisema jana kwamba hana wasiwasi na atatua keshokutwa katika mkoa huo kuanza ziara wiki moja kuanzia Desemba 5 hadi 13 kwa lengo la kuimarisha chama.
“Mimi sijapewa taarifa hizo… wanachama wengi wananipigia wanasema wananisubiri kwa hamu na hakuna taarifa zozote mbaya,” alisema Dk Slaa akiashiria kwamba chama hicho mkoani humo kiko bega kwa bega na uongozi wa juu.
Juu Kusini waunga mkono
Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imeunga mkono hatua ya Kamati Kuu ya chama hicho kuwavua nyadhifa zote za uongozi Zitto, Dk Kitila na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Mratibu wa Chadema Kanda hiyo, Frank Mwaisumbe alisema uongozi na wanachama cha Chadema Nyanda za Juu Kusini wanaunga mkono uamuzi uliochukuliwa na wana imani kubwa na viongozi wa juu wa Chadema.
Taarifa za nyongeza na Anthony Kayanda, Kigoma na Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

WATU WANA KIPAJI CHA MAAJABU: MTAZAME MZEE HUYU MWENYE UMRI WA MIAKA 79 ANAVYOISHI NA MBWA MWITU NA KUWALISHA NYAMA KUTOKA MDOMONI KWAKE.

$
0
0
Mzee Werner Freund ambaye ni mtafiti wa zamani wa wanyama hao nae sasa amekuwa kama mnyama tuu mtazame hapa anakula bila wasiwasi
Inajulikana kabisa kuwa Mzee Warner Freund mwenye umri wa miaka 79 ndiye mzee kinara katika kuishi na wanyama wakali na hatari nchini Ujerumani akiwa na zaidi ya Mbwa mwitu 28 nyumbani kwake . Mzee huyu amekuwa na wanyama hawa wakali sana kwa muda wa miaka 40, jambo lililomfanya kuzoeana nao moja kwa moja  

Werner Freund akikalisha ka Mbwa mwitu kadogo chakula kutokea mdomoni mwake

Mbwa mwitu hawa wanafurahia chakula kutoka kwa mzee Werner Freund


ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFA HAPA CHINI



 Ukishangaa ya Mussa utaumia sasa tazama nini kinatokea hapa chini


 Werner Freund kama Mbwa mwitu wake nae anakomaa kula moja ya mnnyama aliyekutwa amekufa.

 Nyama inazidi kuliwa
Wanatafuna balaa

Hii Balaa sana

Werner Freund ndivyo anavyokula kila siku

Werner Freund, 79, 




Walisha shiba hawa

Sasa na yeye ameshiba

Werner Freund akiwa amemaliza kuchinja viumbe hawa tayali kwa kuliwa


Picha na Daily Mail.

MADIWANI CCM,CHADEMA WAPIGANA NGUMI KAVUKAVU

$
0
0

Wawili wajeruhiwa,walazwa
Kisa kuhoji matumizi ya Milioni 95/-

Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamejeruhiwaA vibaya hadi kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa kile kinachodaiwa kupigwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo la ukumbi wa halmashauri wa Mkapa wakati kikao.

Diwani wa Kata ya Mwakibete ambaye pia ni Katibu wa Mwenezi Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, jana aliwaeleza wandishi wa habari kuwa tukio hilo lilutokea Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mkapa ambao unamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mwampiki aliwataja madiwani waliojeruhiwa na kulazwa kuwa ni wa Kata ya Sinde, Fanuel Kyanula na wa Kata ya Ilemi, Furaha Mwandalima.

Mwampiki alisema kabla ya kutokea kwa vurugu hizo, madiwani wa vyama vya upinzani walikuwa wakihoji uhalali wa ziara ya baadhi ya maofisa wa Halmashauri ya Jiji wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, kwenda China kwa kutumia fedha za halmashauri bila kufuata utaratibu.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Alisema katika ziara hiyo, Meya Kapunga aiongozana na maofisa watano ambao ni Mkurugenzi wa Jiji, Mchumi, Afisa Mipango na diwani mmoja wa CCM ambayo iliigharimu halmashauri hiyo zaidi ya Sh. milioni 95 ambazo hazikuwa kwenye bajeti wala kuidhinishwa na kikao chochote.

Alisema madiwani wa Chadema na NCCR-Mageuzi walifuata taratibu zote za kuhoji suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuorodhesha majina yao na kusaini ili mkutano wa madiwani uitishwe na hoja hiyo ijadiliwe.

Kwa mujibu wa Mwampiki, kikao cha Madiwani kilichoketi Ijumaa waliamini kuwa ajenda hiyo itaingizwa, lakini wakashangaa kuona haimo kwenye orodha ya ajenda zilizopaswa kujadiliwa.

Alisema madiwani wa upinzani walipohoji juu ya kuondolewa kwa ajenda hiyo, Meya Kapungu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alikuja juu na kuamuru mlango ufungwe ili madiwani wapigane.

“Tulishangaa kusikia Meya akisema kuwa kila siku madiwani wa Chadema tunawafanya wasiishi kwa raha mjini na kutamka kuwa inabidi milango ifungwe ili zipigwe,” alisema Mwampiki.

Alisema madiwani wa Chadema kuona hivyo waliamua kutoka haraka nje ya ukumbi wa mkutano, huku wakirushiwa chupa za maji na baadhi ya madiwani wa CCM.

Mwampiki alidai kuwa hata baada ya madiwani wa Chadema kuwa wametoka nje ya ukumbi wa mkutano, madiwani wa CCM waliwafuata na kuanza kuwashambulia kwa kipigo mpaka walipoachanishwa na polisi waliokuwepo eneo hilo.

Alisema katika vurugu hizo, madiwani wawili wa Chadema walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa kwa matibabu na walilazwa.

Asema Diwani wa Ilemi, Mwandaliwa alijeruhiwa sehemu za shingo kiasi cha shingo yake kutogeuka kila upande huku Diwani wa Sinde, Fanuel akiwa amejeruhiwa kwenye shavu kutokana na ngumi walizokuwa wakipigwa.

Akizungumza baada ya kutoka hospitali, Mwandalima alisema alikuwa miongoni mwa madiwani wa mwisho kutoka ukumbini na kuwa alipofika nje ya ukumbi alijikuta akivamiwa na kundi la madiwani wa CCM ambao walianza kumshushia kipigo huku wengine wakimkaba na kumuumiza vibaya maeneo ya shingoni.

Meya wa Kapunga alikanusha kuhusika na ugomvi huo huku akisema kuwa hakuna diwani aliyepigana ndani ya ukumbi wa mkutano.

Alisema anachokumbuka ni kwamba madiwani wa upinzani walikuwa na hoja ya kutaka kujua juu ya ziara ya watumishi wa Halmashauri nchini China, lakini hawakufuata utaratibu na kanuni  walizojiwekea katika kuhoji masuala mbalimbali ya halmashauri.

Alisema baada ya kupitia orodha ya majina ya madiwani waliokuwa wakihoji suala hilo, walibaini kuwa kuna baadhi ya saini za madiwani zimeghushiwa, jambo ambalo alisema ni kinyume cha taratibu za halmashauri na sheria za nchi.

Alisema miongoni mwa saini zilizobainika kughushiwa ni za baaadhi ya madiwani ambao hawapo jijini Mbeya kwa muda mrefu.

Alisema baada ya hoja ya madiwani hao kukataliwa, ndipo walipoinuka kutoka ndani ya ukumbi wa mikutano huku wakiwatolea matusi ya nguoni madiwani wenzao wa CCM.

“Ninachokumbuka ni kwamba wakati madiwani wa Chadema wakitoka nje walikuwa wakitukana matusi ya nguoni inawezekana matusi hayo yaliwauma wenzao wa CCM ambao waliwafuata huko nje, hivyo kama walipigwa nje ya mkutano mimi sina taarifa,” alisema Kapunga.

Akizungumzia ziara ya watumishi wa halmashauri ya akiwamo yeye nchini China, Kapunga alisema ziara hiyo ilitokana na agizo la serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (Tamisemi).

Alisema kabla ya kufanya ziara hiyo alifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kulijulisha Baraza la Mdiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ofisi ya Katibu Tawala ya Mkoa wa Mbeya, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, alipinga kiwango cha fedha cha Sh. milioni 95 kinachodaiwa na madiwani wa Chadema kuwa kilitumika kwenye ziara hiyo, badala yake alisema zilitumika Sh. milioni 54.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema yuko nje ya Mkoa wa Mbeya kikazi, hiyo hakuwa na taarifa zozote.

Pamoja na Kamanda Diwani kusema hana taarifa, lakini Mwandalima alisema walipewa fomu za polisi PF 3 kabla ya kupatiwa matibabu hospitali.
CHANZO: NIPASHE
Viewing all 16413 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>