Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all 16413 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH.ABDALLAH KIGODA KUWA MGENI RASMI TAMASHA LA HANDENI KWETU

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Viwanda na  Biashara ambaye pia ndio mbunge wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Utamaduni, lililopangwa kufanyika Katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.

Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani hapa, huku likitarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea kushika kasi, ambapo kwenye uwanja huo, Tamasha hilo litaanza saa 2 asubuhi hadi saa 12 za jioni.

Akizungumza jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema maandalizi yamezidi kushika kasi kwa kuangalia mazoezi ya vikundi kadhaa vitakavyotoa burudani katika tukio hilo.

“Tunashukuru Mungu kuona mambo yanazidi kuwa mazuri kwa kuhakikisha kuwa Desemba 14 mwaka huu tunafanya tamasha lenye mguso na kila mmoja wetu kufaidishwa.


“Huu ni wakati wa kila mtu kujipanga ili aje kushiriki kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa juhudi hizi zote zipo kwa ajili ya kujenga ushirikiano kwa watu wote,” alisema Mbwana.

Wadhamini katika tamasha hilo ni pamoja na gazeti la Mwananchi, Clouds Media Group, niPhed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog, PamojaPure Blog na Taifa Letu.com.

LAMBORGHINI SIO KWENYE MAGARI TU SASA YAZINDUA SMARTPHONES ZA KIFAHARI “ANTARES” ZINAUZWA TSHS MILIONI 6.2

$
0
0
 Lamborghini haipo kwenye biashara ya magari ya kifahari tu. Na sasa imetangaza smartphone zake ziitwazo Antares.
 Simu hizi chache zimetengenezwa kwa kufuatisha umbo la gari hizo za kifahari na zinatumia mfumo wa Android 4.3 na zinakuja na 1.5 GHz quad-core processor, RAM yenye ukubwa GB 1, kumbukumbu ya ndani yenye ukubwa wa GB 32 na micro SD yenye ukubwa wa GB 32. Simu hizi zinauzwa $4,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 6.2.







KERO YA LEO:JE HIKI KIFOLENI CHA HAPA KUINGILIA MLIMANI CITY MALL NA KUELEKEA CHUO KIKUU KINASABABISHWA NA NINI?

$
0
0

 Ni mvurugano tuu
 Hapa ni mchanganyiko maana barabara hiyo kuna njia mbili, moja ya kwenda na nyingine ya kurudi lakini cha ajabu unakuta njia tatu yamepanga ynayoelekea njia moja kama picha invyoonesha na kusababisha foleni zisizokuwa na msingi


 Foleni hii inasababisha mpaka magari ya Barabara kuu yasiweze pita vizuri
 Baadhi ya magari mfano Defender hii haijurikani inatokea wapi 
 Foleni tuu hapa
Mbabe ndiye anaweza katiza

YALIYOJIRI LEO KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO(TCRA) JIJINI DAR

$
0
0

 Ndugu Mlaki akiwa anafungua Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John S. Nkoma akifuatilia kwa umakini maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania (TCRA) 



 Baadhi ya wadau mbalimbali katika secta ya Mawasiliano Tanzania wakiwa katika Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
  Waendesha mada wakiwa mezani Kutoka kushoto ni Bi. Elizabeth Nzagi, Ndugu. Haruni Lemanya , Aliyeshika Microphone no Ndugu. Mlaki ambaye ndiye Mwendeshaji wa Mkutano, Injinia James Kilaba na Albert Richard .
 Wadau mbalimbali wa mawasiliano Tanzania pamoja na Secta nyengine mbalimbali wakiwa wanafuatilia kwa umakini mada zinazo endelea
  Bi. Elizabeth Nzagi akizungumzia Mada juu ya sheria na mambo muhimu katika mawasiliano.
  Injinia James Kilaba akizungumzia juu ya mafanikio ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia mwanzo mpaka kufikia Miaka 10.
  Mkurugenzi wa Mambo ya Posta Tanzania Bi.Makubuli akizungumzia jambo juu ya maendeleo ya Posta.
  Ndugu Haruni Lemanya akizungumzia maswala mbalimbali ya Posta ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hali ya juu ambayo yamefanywa na posta, mfano kuanzisha utaratibu wa kuweka sanduku la posta kila nyumba.
Ndugu Albert Richard akizungumzia juu ya nguvu  ya Mabadiliko ya Sayansi na Teknorojia katika kukuza uchumi wa Tanzania ikiwa ni Mijini na Vijijini

Endelea kufuatilia hapa 


WATANZANIA WAWILI WANASWA NA KILO 55 ZA DAWA ZA KULEVYA AFRIKA KUSINI

$
0
0
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa (katikati) akiangalia dawa za kulevya aina ya heroine zilizokamatwa nchini, zikifunguliwa na afisa wa jeshi la polisi Neema Mwakagendi kabla ya kuteketezwa jana, katika tanuri la Kiwanda cha Saruji wazo jijini Dar es Salaam.Dawa aina mbalimbali zilizokamatwa ziliteketezwa. Picha na Juliana Malondo 
Johannesburg/Dar. Watanzania wawili wanahojiwa na Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya.
Watu hao wawili wanatazamiwa kufikishwa mahakamani kesho kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye thamani ya Rand75 milioni (Sh11.7 bilioni).
Maofisa wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Makosa ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks), kiliwakamata watu hao katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la Gauteng.
Msemaji wa Hawks, Paul Ramaloko alisema jana kuwa maofisa hao walivamia nyumba waliyokuwa wanaishi Watanzania hao na kukuta mzigo huo.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watu hao kwa kuhofia kuharibu uchunguzi akisema bado walikuwa wanawasaka watuhumiwa zaidi wakiwamo raia wa Afrika Kusini.
Alisema kikosi chao kimepata mafanikio makubwa kwa kukamata dawa nyingi kiasi hicho... “Tunakaribia kuwakamata vinara wa biashara hiyo, maana tumeelezwa kuna kundi kubwa la watu wazito,” alisema Ramaloko. Hii inakuwa mara ya pili katika kipindi cha miezi minne kwa Watanzania kutuhumiwa kubeba dawa hizo.
Julai mwaka huu, wasanii wawili Agness Gerald `Masogange’ na Melissa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Johannesburg wakiwa na kilo 180 za kemikali aina ya ephedrine zenye thamani ya Sh7 bilioni.
Baada ya kukaa miezi miwili jela, Masogange alipatikana na hatia ya kuingiza kemikali hiyo, ambayo hutumika kutengeneza dawa za kulevya na kutozwa faini ya Rand 15,000 (Sh2.3 milioni).
Melissa aliachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia.
Wasafirishaji sasa watumia samaki
Katika hatua nyingine, wasafirishaji wa dawa za kulevya inasemekana wamebuni mbinu mpya ya kutumia samaki kusafirisha bidhaa hiyo haramu.


Akizungumza jana wakati wa uteketezaji wa dawa za kulevya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema wanatumia samaki kwa kuwa wana harufu kali.
Alisema harufu hiyo huwafanya mbwa waliopewa mafunzo ya kutambua dawa hizo kushindwa kuzigundua.
“Tumebaini kwamba siku hizi wanaweka dawa hizo chini kwenye mizigo yao na kisha kuweka samaki hao juu hata mbwa akinusa vipi hawezi kuambulia kitu,” alisema Nzowa.
Alisema wengine hutumia mboga aina ya kabichi kwa usafirishaji wa bangi. Alisema hutanguliza bangi kwenye magunia na juu yake kuweka kabichi.
Pia alisema changamoto nyingine katika vita hiyo ni baadhi ya wasafirishaji wa dawa hizo kusafirisha malighafi (vibashirifu) ya kutengeneza dawa hizo.
Dawa zilizoteketezwa jana katika tanuri la Kiwanda cha Kutengenezea Saruji cha Twiga, Wazo Hill, Dar es Salaam, zilikuwa kilo 702 za bangi, kilo 12 za heroine, kilo tano za cocaine na kilo 105 za kuberi.
MWANANCHI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZIKO YA MTOTO WA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM, PETER MANGULA MAKABURI YA KINONDONI

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake, Peter Mangula, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.


 Watoto wa marehemu, wakiweka udongo kwenye kaburi ikiwa ni ishara ya kumzika baba yao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, akiwaongoza sehemu ya wanafamilia kuweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wake, (Peter Mangula), wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika makaburi ya Kinondoni Kisutu jijini Dar es Salaam,leo.
 Baadhi ya Vijana wa CCM, wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Peter Mangula, wakati wakiwasili kwenye makaburi ya Kisutu Kinondoni kwa maziko.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Peter Mangula likishushwa kaburini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko ya mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula) zilizofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko ya mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, (Peter Mangula) zilizofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim,akiwaongoza mawaziri wenzake wastaafu, kuweka mashada ya maua.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, wakiweka mashada ya maua.
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbload Slaa, akiweka Shada la maua.
Kingunge Ngambale Mwilu, akiweka shada la maua kwa niaba ya wazee.
Meya wa Ilala, Jerry Slaa,akiweka shada la maua.

PICHA NA SOFIANI MAFOTO

RAIS KIKWETE APOKEA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akianza kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza leo jioni. Kombe hilo limerejea jijini Dar es Salaam na kesho wananchi watapata fursa ya kupiganalo picha.



Hapa ni furaha tu

MHE. JANUARY MAKAMBA KUWA MGENI RASMI TANZANIA UHURU NIGHT WASHINGTON, DC,

$
0
0
 MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA KUUNGANA NA RAIS MUSTAAFU ALI HASSAN MWINYI SHEREHE YA UHURU CALIFORNIA
 Tiketi zinapatikana online au Piga simu kwa Dj Luke 301 661 6696,  Dj Seif  202 286 6595 na Baraka Daudi 301 792 8562 


Hawa ndio watakaopendezesha Uhuru  Bar
Kristina                             Sonia                                        Nina
Uhuru Red Carpet

VIJIMAMBO Blog inakuletea TANZANIA UHURU NIGHT siku ya Jumamosi December 7, 2013 Ukumbi wa THE FRIENDSHIP CENTER, 9055C Maier road, Laurel, MD 20723 Balozi Mhe. Liberata Mulamula atakuwa mgeni rasmi
Ni usiku wa Uhuru wa Tanzania, kula, kunywa mpaka unasaza kwa $60 tu na muziki ni mpaka asubuhi nunua tiketi yako mapema nafasi za kukaa ni watu 200 tu na 
Mimi ni mtanzania, natoka Tanzania, nchi yangu Tanzania, MIAKA 52 ya UHURU wa TANZANIA.
TANZANIA UHURU NIGHT Itaanza saa 12 jioni (6pm) kwa COCKTAIL

Tega sikio tutazidi kuwajuza mambo mazuri yakayojiri siku hii ya Tanzania Uhuru Night


ALL YOU CAN EAT AND DRINK ALL NIGHT FOR $60 ONLY

KARIBUNI WOTE

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBER 30, 2013

$
0
0













VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO VYADAIWA KUSABABISHA UPOFU

$
0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal, katika Mkutano wa mwaka wa Uzazi wa Mpango, Oktoba mwaka  huu. Katika Mkutano huo Tanzania ilionekana bado ina matumizi ya chini ya dawa za uzazi wa mpango. Picha na Maktaba. 
Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha  ugonjwa wa macho ujulikanao kamaGlaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.
 Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa  Afya na Lishe  uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).
Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen  ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato  huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.
Wanawake zaidi  ya 3,400  wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walifuatiliwa kwa zaidi ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utafiti huo.
Profesa Shan Lin wa Chuo Kikuu cha Carlifonia, San Francisco anasema wanawake wanaotumia vidonge hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatakiwa kupima maradhi ya macho aina ya Glaucoma na afya zao zifuatiliwe kwa uangalifu na wataalamu wa macho.
Utafiti huo umebaini kuwa wanawake waliotumia vidonge hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu walikuwa na hatari kwa asilimia tano ya kupata upofu usababishwao na glaucoma ukilinganisha na wasiotumia vidonge  hivyo.
 Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale  wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen  vina umuhimu katika  seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.
“Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho,” anasema Dk Pasquale.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo  Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema  ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.
“Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge,” anasema
Dk Masawe anasema si vyema watu kuzitumia dawa za Uzazi wa Mpango kwa  mazoea na endapo wataona ni vyema kufanya hivyo, washauriane na wataalamu wa afya.
Anasema  kuwa elimu inahitajika kwa kina kuhusu matumizi ya dawa hizo kwani wapo baadhi ya watu wanaozitumia bila mpangilio wala utaratibu maalum.
“Hizi dawa zinasaidia lakini zisipotumiwa kwa uangalifu, huenda zikasababisha madhara,” anasema Dk Masawe.
Kwa upande wa utafiti huo uliojikita kuangalia madhara ya vidonge hivyo kwa wanawake, watu wanaovitumia wanatakiwa kuwa makini na uhusiano uliopo kati ya afya ya uzazi na maradhi ya macho hasa kama mtumiaji amefunga hedhi mapema.
Matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa katika mkutano wa kila mwaka wa Chuo Kikuu cha Mfumo wa Macho Marekani (USP), yanasema wanawake zaidi ya 3,046 walifanyiwa uchunguzi kuhusu afya ya uzazi na maradhi ya macho.
 Pamoja na sababu nyingine za maradhi ya macho,  wanasayansi waliofanya utafiti huo wanasema kutumia vidonge vya uzazi kwa muda mrefu, ndicho chanzo kikuu cha upofu na kutaja sababu nyingine kuwa ni historia ya familia, shinikizo la ya macho na kisukari.
 Watalaamu wa afya nchini wanasema bado madhara ya dawa hizo yanatofautiana kulingana na aina ya dawa anayotumia mhusika.
Madhara mengine ya dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu, kichwa kuuma, matiti  kuuma, kuongezeka uzito na kupata hedhi bila mpangilio.
Dk Joseph Matiku wa Kituo cha Afya, Mugumu, Serengeti anasema, hatari zaidi ni kwa binti wanaotumia dawa hizo kwa muda mrefu kabla hawajaanza maisha ya ndoa.
“Wapo wanawake ambao wanapata uvimbe kwenye kizazi kutokana na matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi. Ingawa hakuna utafiti uliofanyika kuthibitisha hili, lakini wanawake wengi wanaotumia dawa hizi hapa nchini wanapata uvimbe maarufu wa Fibroids” anasema.
Hata hivyo, Oktoba mwaka huu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi anasema Wizara ya Afya ipo kwenye harakati za kutafuta fedha ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanawake wanaostahili kupanga uzazi wanapata dawa husika.
Mwaka jana wakati wa Mkutano wa Uzazi wa Mpango uliofanyika London Uingereza, Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itafikisha asilimia 60 katika huduma za uzazi wa mpango.
Vilevile katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Uzazi wa Mpango uliofanyika Oktoba mwaka huu, Makamu  wa Rais Dk Gharib Bilal alisema juhudi za ziada zinahitajika kuhakikisha kiwango cha watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango, kinaongezeka ili kutimiza lengo la kimataifa ya kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hiyo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa, kiwango cha matumizi ya huduma za uzazi wa mpango kwa nchi zilizoendelea ni asilimia 72, huku Tanzania iliyo kwenye kundi ya nchi zinazoendelea ikiwa ni asilimia 27 tu.
 Dawa za uzazi wa mpango hufanyaje kazi?
Vidonge vya uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuweka uwiano  katika kiwango cha vichocheo.
Katika hili, kazi kubwa ni kuzuia homoni za estrogen kuongezeka na kufikia kiwango cha kati au cha juu.
 Bila homoni ya estrogen, tezi ya pituitari haiwezi kuifanya mirija ya uzazi kuruhusu mayai yaliyochavushwa kwenda kukutana na mbegu za kiume kwa ajili ya utungishwaji wa mimba.
MWANANCHI

MAGAZETI YA UDAKU YAMUAMKIA TENA BOB JUNIOR, YADAI AMEKIRI NDOA KUMUINGIZA ‘CHAKA

$
0
0

Ni siku nyingine magazeti ya udaku yameamka na nyundo nyingine kwa Bob Junior. Awamu hii yanasema ‘Bob Junior: Nilipotea Maboya kuona, aanika siri za ndani za mkewe’.

Bob Junior ameendelea kulaani na kufuatia habari hiyo ameandika: Unafki mkubwaa huu dooh hii too much jamani hii nimechoka tuta pelekana sasa pabaya kweli daimmm wajinga hawaa”
Swali ambalo wengi wameanza kujiuliza ni kuwa, kweli Bob Junior anaandamwa ama ndio zile style za kutafuta kiki?
“Unayapenda nawe haya hiyo pic yako na wema wameitoa wapi?na kama hujayafanya kibabaiko cha nini si uwaache waseme,” ameandika msichana aitwaye Meymah Ally.



MISHAHARA YA VIGOGO ‘HAILINGANI NA UFANISI’

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa katika kikao cha OGP London akisema mishahara ya viongozi wa umma haiwezi kuwa siri kwani ni sehemu ya bajeti, ingawa leo hii wengi katika serikali yake wanatetea usiri uliokithiri katika suala zima la vipato vya ‘wakubwa.’ PICHA | MAKTABA 
Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida.
Huku ikitaja mapato ya mishahara ya marais wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, imesema kuwa hali hiyo ni kuibebesha jamii mzigo wa kugharimia malipo ya viongozi.
Akizindua ripoti hiyo iliyochunguza gharama za kuwalipa viongozi wa Serikali na wanasiasa, Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa), Dk Theodore Valentine, alisema kuwa viongozi wa Afrika Mashariki ndio wanaoongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa zaidi chini ya Jangwa la Sahara.

“Kama viongozi wakuu watakuwa wanalipwa mishahara mikubwa, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zitaweza kugharimia demokrasia?” alihoji Valentine.
Utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2009 na 2012, umebainisha kuwa Rais wa Tanzania analipwa mshahara dola 172,014 kwa mwaka (Sh275 milioni) sawa na Sh22.9 milioni kwa mwezi, huku Rais wa Kenya, akiongoza kwa kulipwa dola 515,021 kwa mwaka (Sh824 milioni) kwa mwaka sawa na Sh68.6 milioni kwa mwezi.
Rais wa Rwanda analipwa dola 199,000 kwa mwaka (Sh124 milioni) sawa na Sh10 milioni kwa mwezi, wakati rais wa Nigeria akipokea dola 161,902 (Sh259 milioni) ambazo ni sawa na Sh21 milioni kwa mwezi.
Pia umeeleza kuwa Rais wa Kenya analipwa mara 320 zaidi ya pato la mwananchi wa kawaida wa nchi hiyo, wakati rais wa Afrika Kusini anapata mara 46 na Rwanda mara 150 zaidi ya mwananchi wa kawaida.
Ripoti hiyo imeendelea kubainisha kuwa rais wa Tanzania analipwa mara 8.2 ya mshahara wa hakimu, huku rais wa Kenya akipokea mara 13.1 na kumpita rais wa Rwanda anayechukua mara 12 zaidi ya mshahara wa hakimu.
Kwa upande wa wabunge, utafiti huo umeeleza kuwa wabunge wa Tanzania wanalipwa mara 3.0 ya mshahara anaolipwa hakimu, Kenya (5.5) na Rwanda (3.0). Viwango hivyo vimetajwa kuwa vikubwa kuliko vya wabunge wa Nigeria na Afrika Kusini.
Naibu Spika anena
Naye Naibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai alisema kuwa umefika wakati ambapo mishahara ya viongozi wa umma inabidi iwekwe wazi kwa wananchi.
“Ningependa mishahara ifahamike kama ilivyo kwa nchi nyingine, hii itaondoa uongo kwa wabunge,” alisema.
Alisema mishahara wanayolipwa wabunge siyo mikubwa na kwamba inapaswa kuongezwa zaidi kwa kuwa hivi sasa imetofautiana kidogo na ya wakuu wa wilaya.
“Mshahara wangu mimi kama Naibu Spika ni mdogo…, hata wa Waziri Mkuu siyo mkubwa. Siku zote mtu anapoongezewa mshahara inamwongezea motisha ya kufanya kazi,” alisema Ndugai.
Serikali yajibu
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga, alisema viongozi wanalipwa mshahara kutokana na nyadhifa walizonazo, hivyo haoni sababu ya jambo hilo kujadiliwa.
Alisema mshahara ni siri ya mfanyakazi husika, na kwamba iwapo itawekwa wazi baadhi ya watu wataacha kujadili mambo ya maendeleo na badala yake wataanza kuzungumzia malipo hayo.
“Tujadili kuhusu namna ambavyo gesi itatuletea maendeleo kwenye uchumi wa nchi yetu na siyo mishahara,” alisema.
Alipopigiwa simu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, alihoji kuwa anazungumza na nani, mwandishi alipojitambulisha alitaka apewe muda hadi baadaye kwa madai kuwa hakuwa sehemu nzuri.
Rais Kikwete na OGP
Akinukuliwa na gazeti la Serikali, Rais Jakaya Kikwete, ambaye Oktoba 31 hadi Novemba Mosi 2013, alihudhuria Mpango wa Pamoja wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) uliofanyika London, Uingereza, ambapo alizungumzia uwazi kwenye Serikali yake likiwemo suala la mishahara.
Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki 1,000 kutoka nchi 60 wanachama na Rais Kikwete alipata nafasi ya kuuelezea mkutano huo, namna Tanzania ilivyoanza utekelezaji wa masharti ya mpango huo.
Rais Kikwete alisema kuwa mshahara wa mtumishi wa umma hauwezi kuwa siri na ndiyo maana unawekwa katika bajeti ya serikali.
“Mishahara haiwezi kuwa siri. Si ipo kwenye bajeti za Serikali?” Alijibu Rais Kikwete alipoulizwa kama suala la mishahara litaendelea kuwa siri katika utekelezaji wa mpango huo.
Rais Kikwete alisema: “Changamoto iliyopo ni kwamba mpango huu unabadili mazoea yetu ya kufanya kazi. Sisi katika kila Serikali kila kitu kilikuwa siri. Sasa OGP inataka mambo haya yawe wazi, ifike hatua mtu aone kutoa habari ni wajibu.”
TUCTA yatoa kauli
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicolas Mgaya alisema wabunge wanalipwa mishahara mikubwa lakini baadhi yao hawaonekani kwenye vikao.
Alitaka mishahara yao iwekwe wazi kwa wananchi kwa kile alichokieleza kuwa kwa sababu wanalipwa kwa kutumia kodi za wananchi.
Anavyosema Profesa Wangwe
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Profesa Samuel Wangwe alisema kuna haja ya kuangalia gharama za kuwalipia viongozi.
“Tuangalie gharama ya demokrasia, lakini jambo la msingi ni kuwa kama wabunge wanalipwa kiasi kinachotajwa basi wafanye kazi yao wanayostahili na wasisahau kwamba wanawawakilisha wananchi ambao ni maskini,” alisema.
Profesa Lipumba
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi - CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ni mchumi kitaaluma alisema kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa viongozi wakilipwa mishahara mikubwa wanafanya kazi zaidi.
“Hakuna ushahidi wowote kwamba kwa kuwalipa wabunge mishahara mikubwa basi wanafanya kazi vizuri zaidi,” alisema.
Akitolea mfano wabunge wa Kenya alisema: “Katika kipindi cha miaka mitano mbunge wa Kenya analipwa dola za Marekani dola 1milioni (sawa wa Sh1.6 bilioni) kiasi ambacho ni sawa na Sh26 milioni kwa mwezi.”
Aliongeza kuwa mishahara ya wabunge wa Tanzania ni zaidi ya mara 40 ya pato la kawaida la mwananchi.
Alipendekeza kuanzishwa kwa taasisi ambayo itapewa jukumu la kusimamia mapato ya viongozi wa umma, na kwamba ni vyema katiba izungumze kuwa mishahara na marupurupu ya wabunge itapangwa na taasisi ambayo ipo huru itakayozingatia mapato ya nchi yalivyo.
MWANANCHI

KAMPUNI YA LG WAJA NA SIMU MPYA ‘G FLEX’ ZENYE UWEZO WA KUJIFUTA MIKWARUZO (SELF-HEALING

$
0
0
Kampuni ya LG ya Korea Kusini imetoa simu mpya LG G Flex zilizotengenezwa kwa material yanayoziwezesha simu hizo kurudi katika hali yake ya upya, hata baada ya kupata mikwaruzo ya kawaida ambayo hufanya simu ionekane kuchakaa. Simu hizo zina uwezo wa kujirudisha katika hali ya kawaida (self-healing) mara baada ya kupata mikwaruzo ya kitu chenye ncha kama funguo, kisu nk, na baada ya muda alama zote za mikwaruzo zinapotea na kurudi ilivyokuwa.

Pia display ya simu hizo za LG G Flex imetengenezwa kwa plastic badala ya kioo kama zilivyo simu zingine, na pia muundo wake wa kujikunja (curve) unairuhusu simu kunyooka pindi inapokandamizwa kwa nguvu na kurudi katika hali yake bila kuvunjika.


Kwa simu hizi za G Flex, mtumiaji hatapata yale maumivu ambayo huwakuta watumiaji wengi ya kuvunjika kwa kioo, au simu kupata mikwaruzo mingi inayosababisha kuifanya ichakae haraka.
GG Flex ambazo kwa sasa zinapatikana Korea peke yake zitazinduliwa kwa soko la kimataifa Jumanne ijayo (December 3) huko Hong Kong. Bei ya simu hizo kwa Korea ni 999,990KRW sawa na Tsh milioni moja na nusu.
Tazama video kujionea majaribio ya G Flex



SOURCE: YAHOO

HUKUMU UJENZI WA GHOROFA JIRANI NA IKULU JANUARI 15

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema itatoa hukumu ya kesi ya  ujenzi wa jengo la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu lililopo mtaa wa Chimala Kitalu cha 45 na 46, jijini Dar es Salaam inayomkabili aliyekuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na mwenzake Januari 15, mwaka 2014.


Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao.

Hakimu Fimbo alisema baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao, mahakama hiyo itatoa hukumu Januari, mwakani.

Kabla ya uamuzi huo, mshtakiwa wa pili aliyekuwa Msanifu Mkuu wake, Richard Maliyaga (55), alidai kuwa alipitisha kibali cha jengo baada ya kupata maelekezo ya serikali.

Alidai kuwa alishiriki mchakato wa ujenzi wa jengo hilo kama Mwenyekiti wa kamati ya kutoa vibali vya ujenzi iliyokuwa na watu sita akiwamo yeye.


“Kamati ilinitaka nitoe kibali cha ujenzi huo baada ya kupokea maelekezo ya serikali …kabla ya kutoa vibali kamati yetu ilikuwa inapitia michoro na kama haina mapungufu tulikuwa tunaridhia kibali kutolewa kwa ajili ya ujenzi kufanyika,” alidai Maliyaga.

Alidai kuwa watu wote waliohusika kwenye mchakato wa ujenzi wa jengo hilo, hawajaburuzwa mahakamani na kwamba kesi hiyo inawakabili watu wawili huku wenzao wakipeta mtaani.

“Mimi naona nimeonewa tu kwenye kesi hii, sijanufaika na chochote katika mradi wa ujenzi wa jengo hilo na kwamba sikutumia madaraka yangu vibaya,” alidai mshtakiwa huyo wakati akifunga utetezi wake.

Katika kesi ya msingi, Kimweri na Maliyaga wanakabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.

Ilidaiwa kuwa Kimweri alikuwa na wadhifa huo TBA kuanzia mwaka 2002 hadi 2010 na Maliyaga aliajiriwa mwaka 2002 akiwa Msanifu Mkuu.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alidai kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na TBA, ambako hadi mwaka 2006 kilikuwa hakijaendelezwa.

Aidha,TBA kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma, iliwaalika wanaotaka kuwekeza kuwasilisha andiko la awali kwa ajili ya uendelezaji.
CHANZO: NIPASHE

HUU NI MTAZAMO TU: SOMA HAPA SABABU KUMI(10) ZINAZOSABABISHA WASICHANA KUTOINGIA KWENYE NDOA

$
0
0

Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.

 Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi kukana na shamra shamra anazokuwa nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.
Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)

1.      Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)

Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake.Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.  
Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo, kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. 
Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.


2.     Kutaka mwanaume tajiri

Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.
Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida, hata ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari.
Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.

3.     Kutompata Mwanaume Ampendae

Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia.  
 Wengi katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
Yeye kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati.  Huyu mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.  

4.     Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)

Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka. 

Akija wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo. 

Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.

 Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.

5.     Kujiona ni mzuri sana

Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani.

 Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana. 

Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.

6.     Kujiona ana Umri mdogo

Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.

 Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.

 Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa. 

Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.

 Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.

7.     Maradhi hasa UKIMWI

Hili kama lilivyo kwa wanaume -  Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto. 

 Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi

8.    Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)

Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.

Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.  

Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.

9.     Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:

·         Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.

·         Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.

·         Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona kama ni utumwa.

10.Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi

Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi. 

Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.  

 Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.



WALIMBWENDE WA MISS TANZANIA USA PAGEANT WAJINOA KWA MARA YA MWISHO

$
0
0
 Joy Kalemera kutoka New Jersey
 Faith Kashaa kutoka Alabama


 Julia Nyerere kutoka Maryland.
 Hellena Nyerere kutoka Maryland.
 Sham Manka kutoka Massachusetts.
 Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania.
Walimbwende wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kujinoa kwa ajili ya kumtafuta Miss Tanzania USA Pageant itayofanyika Hollywood Ballroom anuani ni 2126 Industrial Pkwy, Silver Spring, MD 20904 kati mstari wa mbele ni Miss Pageant wa kesho akifuarahia ukodak moment na washiriki. 

Walimbwende wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na waratibu wakiwemo mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Afrika USA Pageant Lady Kate (wa pili toka kulia mstari wa mbele), mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey (wanne toka kushoto mstari wa mbele).

Mbunge viti maalum Chadema Mhe. Leticia Nyerere katika picha ya pamoja na Hidaya Mahita (kushoto) na Hellena Nyerere ambaye ni mwanae anayeshiriki kwenye kinyang'anyiro cha miss Tanzania USA Pageant.
 Mwanahabari wa VOA Sunday Shomari(kushoto) akimdodosa mawili matatu mlimbwende Sham Manka kutoka Massachusetts.

BALOZI WA COCA COLA DAVID CORREY ATUA DAR NA KOMBE LA DUNIA, MAMIA WAFURIKA KULIONA

$
0
0

 Balozi wa FIFA Coca-Cola David Correy kutoka Marekani aliyeimba wimbo rasmi wa Brazil World Cup 2014  akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ambapo maelfu ya Watanzania wamepata fursa ya kushuhudia kombe halisi la FIFA la Dunia na kupiga nalo picha kwa karibu.
 Balozi wa FIFA Coca-Cola David Correy kutoka Marekani aliyeimba wimbo rasmi wa Brazil World Cup 2014  akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo


Watanzania wamepata fursa ya kushuhudia kombe halisi la FIFA la Dunia na kupiga nalo picha kwa karibu.


TAMKO LA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI NA KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETI KUHUSU KUJIUZURU

$
0
0



MSAFARA WA MWENYEKITI UVCCM WAWEKEWA MAGOGO

$
0
0
Polisi mkoani Pwani inachunguza kundi la watu linalodaiwa kuweka magogo barabarani kuzuia msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) taifa, Sadifa Juma Khamis (MB) katika eneo la Tondoroni, wilayani Kisarawe, mkoani humo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema atazungumzia suala hilo baada ya  kupata  taarifa kamili.

Kwa mujibu  wa watu walioshuhudia tukio hilo, kundi hilo liliweka magogo hayo jana usiku katika barabara ya kati ya eneo la Mpuyani katika njia panda ya barabara iendayo vijijini kuingia barabara kuu ya Morogoro.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema katika nyakati tofauti kundi hilo lilianza kuzuia msafara huo kwa kutaka kushinikiza dai la mgogoro wa mipaka kati ya eneo la Jeshi la Wananchi wa Ulinzi Tanzania (JWTZ) na makazi ya watu katika eneo la Tondoroni, wilayani humo.

Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika walidaiwa kutishia kuchoma moto magari ya msafara huo wa mwenyekiti wakati alipotaka kushuka na kuzungumza nao na kuamua kujisalimisha kwa kuingia ndani ya gari  na kurudi Kisarawe.


Mwenyekiti  huyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Tanzania Visiwani mapema akiwahutubia  wananchi wa Kisarawe aliwataka kudumisha amani kwa  kukiweka Chama Cha Mapinduzi madarakani. “Amani ikivurugika hakuna atakayekuwa salama, hata askari  nao  hawatokuwa salama”.

Akiongea na viongozi wa CCM na UVCCM  katika jengo la ofisi za CCM wilaya, aliwataka wanachama hao kuvunja makundi ya kampeni kwa kuwa hayana tija kwa sasa, isipokuwa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Alisema kuwa Muungano wa Tanzania ni muhimu hivyo changamoto zilizomo ndani yake zitafutiwe muafaka kwa njia ya amani.

Alisema kuna  baadhi ya watu wakorofi ambao wanadai muungano uvunjwe hasa kutoka Pemba wakidai kuwa kisiwa hicho ni chao wakati  visiwa hivyo vya Pemba na Zanzibar havina wenyewe na watu walioko huko wametokana  na  biashara ya utumwa na wengi wao walitoka upande wa Tanzania Bara wa makabila mbalimbali.

Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alimsimika mwandishi wa siku nyingi, Abubakar Mlawa kuwa kamanda wa UVCCM wilayani humo na wengine 15  wakiwamo madiwani  kuwa makamanda wa UVCCM wa kata zao.
 
CHANZO: NIPASHE

MWANAMUZIKI MKONGWE WA CONGO, TABU LEY ROCHEREAU AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mwanamuziki mkongwe wa Congo, Pascal Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa katika hospitali ya nchini Ubelgiji.

Kwa mujibu wa mwanae Charles Tabu, aliyeongea na Radio Okapi, Tabu Ley amefariki kwa kiharusi na Kisukari.
Naye Nyboma Mwandido, mwanamuziki mwenzie aishiye jijini Paris, Ufaransa amethibitisha kifo cha msanii huyo kilichotokea leo Jumamosi saa 2 asubuhi Brussels. Tabu Ley alikuwa mgonjwa mahututi kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa na kiharusi alichokipata mwaka 2008.
Kiharusi (stroke) kilimfanya awe kwenye kiti cha walemavu tangu muda huo. Pamoja na muziki, Tabu Ley aliwahi kuteuliwa kuwa waziri na Rais Laurent Kabila mwaka 1997 na baadaye kuwa mbunge.


Awali, msanii huyo wa Rhumba aliyekataa kuwa mshairi wa Rais Mobutu Sese Seko alilazimika kuikimbia nchi hiyo.
Miaka ya mwishoni alikuwa akiishi Paris, Ufaransa akipata matibabu kabla ya hivi karibuni kupelekwa Ubelgiji kupata matibabu maalum.
Katika miaka 46 ya muziki, Tabu Ley ameshaandika zaidi ya nyimbo 3,000 na kuuza maelefu ya nyimbo.
Viewing all 16413 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>