Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all 16423 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS NOVEMBER 28, 2013

$
0
0

















POLISI YAPIGA MARUFUKU KUUZA VISU, SIME, MAPANGA BARABARANI

$
0
0
“Kwa mfano, badala ya ofisi kwenda kuchukua kiasi kikubwa cha fedha na kwenda nacho kiwandani au ofisini kwa ajili ya kuwalipa mishahara wafanyakazi, ni vyema kujisajili katika mitandao ya simu au watumiwe katika ATM,”  Kamishna Kova. 

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imepiga marufuku biashara ya kutembeza visu, sime na mapanga barabarani na kusema yeyote atakayekiuka agizo hilo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo lipo katika mchakato wa kupendekeza sheria mpya ya matumizi ya silaha na umiliki ili kudhibiti matumizi mabaya yakiwamo uuzaji wa visu, mapanga na sime kiholela.
Kamishna Kova alisema tatizo kubwa si mtu kumiliki silaha, bali jinsi watu wanavyozitumia vibaya na kusababisha madhara katika jamii na kuongeza kuwa sheria hiyo itajumuisha uuzaji holela wa visu, mapanga na sime barabarani na umiliki wa silaha za  moto.

“Kwa mfano visu, kwa kawaida vinatumiwa nyumbani kukatia nyanya na vitunguu, lakini mtu anaweza kukitumia vibaya kwa kumchoma nacho mtu tumboni au kifuani...hivyo atakayeonekana anauza vitu hivyo, atachukuliwa hatua.
 Hatua hiyo imekuja baada ya mfululizo wa mauaji ya kutumia silaha za moto yanayohusishwa na wivu wa mapenzi kukithiri nchini.
Novemba 19, mwaka huu, Gabriel Munisi aliwaua watu wawili kwa risasi na kumjeruhi mpenzi wake, Christina Newa, mama mzazi wa mpenzi wake, Ellen Eliezer na kisha kujiua, kwa kile kinachoaminika kuwa ni wivu wa mapenzi.
Mapema Oktoba mwaka huu, Mwandishi wa Habari wa Kituo cha ITV, Ufoo Saro alijeruhiwa pia kwa risasi na mpenzi wake, Anthery Mushi. Pia alimuua mama mzazi wa Ufoo na kisha kujiua kwa kujipiga risasi.
Kamishna Kova alisema pia kuwa katika mchakato huo wa kuunda sheria mpya za umiliki wa silaha, hatua kali ikiwamo kunyang’anywa silaha hizo kwa watu wanaozitumia vibaya itachukuliwa.
Hata hivyo, alisema wakati sheria hizo zikisubiriwa, polisi watawachukulia hatua kali wote watakaobainika kuzitumia vibaya. Aliwataka Watanzania kuwa makini na matukio ya uhalifu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka na sikukuu.

MWANANCHI

TAZAMA HAPA MATOKEO YA MECHI ZA EUFA CHAMPIONS LEAGUE ZILIZOCHEZWA JANA JUMATANO NOVEMBER 27, 2013

$
0
0

 







UANACHAMA WA ZITTO ‘MOTO’ CHADEMA',

$
0
0
UANACHAMA wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe umetajwa kuwa ‘kaa la moto’ kwa uongozi wa chama hicho hata kabla ya kiongozi huyo kujibu mashitaka 11 yanayomkabili ili kunusuru uanachama wake.
Duru za siasa ndani ya chama hicho, zinasema Chadema haiko tayari kukabiliana na mtikisiko wa Zitto kuvuliwa uanachama, kwa kuwa hatua ya kuvuliwa madaraka tayari imegharimu umoja na utulivu wa chama hicho.
Taarifa hizo zinasema kwa sasa kuanzia Kamati Kuu mpaka wanachama, kuna mpasuko mkubwa ambao namna pekee ya kuuziba ni kumshawishi Zitto na Mwenyekiti Freeman Mbowe, kupatana.
Hata hivyo, wakati jitihada za kuwapatanisha zikiendelea, duru za siasa zinaeleza kuwa kambi ya Mbowe ina wajumbe wanaoshinikiza kumtosa Zitto na kuwa tayari kukabiliana na gharama zake.
Majimbo
Mtoa habari wetu kutoka ndani ya Chadema anaeleza kuwa hofu kubwa iliyopo kama Zitto atanyang’anywa uanachama, ni ukweli kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wanaweza kupoteza majimbo mengi na kuipa mwanya CCM kupita kirahisi.


“Ni kweli huu si mgogoro wa kwanza kwa Chadema na mara zote viongozi walipovuliwa madaraka kulitokea mtikisiko, lakini si kama huu wa Zitto… mbaya zaidi, majimbo ya viongozi tuliowavua madaraka leo hii yamepokwa na CCM, hatuko tayari kupoteza zaidi,” alisema mtoa habari huyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina.
Akitoa mfano, alisema mgogoro kati ya Chadema na Katibu Mkuu wa zamani Dk Aman Kabourou, ndio ulisababisha jimbo la Kigoma Mjini lililokuwa moja ya majimbo ya Chadema, leo hii kukaliwa na CCM.
Mbali na Kigoma Mjini, mtoa habari huyo alikumbushia pia jimbo la Tarime, alikokuwa Makamu Mwenyekiti, Chacha Wangwe, ambalo mbali na kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya kifo chake, leo linashikiliwa na CCM.
“Unajua hata kwa Zitto (Kigoma Kaskazini) ukiangalia kama kweli tukimtosa, sina hakika kama tutarejesha lile jimbo. Na hata kwa Arfi (Said, Makamu Mwenyekiti aliyejiuzulu, Mbunge wa Mpanda Kati), kama yule mzee tukimchezea hatuna chetu,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusu mpasuko huo, alikataa na kuhoji: “Kwani wewe huoni, mbona wenzenu wameandika mpasuko uliotokea katika Kamati Kuu?”
Mbali na mtoa habari huyo, hata katika waraka unaodaiwa kusababisha mtafaruku huo ambao Dk Kitilla Mkumbo alikiri kuuandaa, Chadema imetajwa kuwa na udhaifu wa kushinda majimbo katika uchaguzi mdogo.
“Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika uchaguzi mdogo mara nane, lakini tumeshinda mara mbili tu sawa na asilimia 25,” alisema Dk Mkumbo katika waraka wake.
Usuluhishi
Pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kutangaza kumwandikia Zitto mashitaka yake na kumpa siku 14 za kujibu, tayari kumeripotiwa kuwa nyuma ya pazia chama hicho kimeamua kumwangukia Zitto yaishe, ikiwa ni pamoja na kumwahidi cheo kikubwa kuliko Naibu Katibu Mkuu.
Kwa mujibu wa taarifa hizo katika uchaguzi mkuu wa Chadema Juni mwakani, Zitto atashawishiwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti bila mpinzani au na mpinzani dhaifu na Mbowe ataachiwa kugombea uenyekiti bila mpinzani au na mpinzani dhaifu, lengo likiwa kurejesha umoja wakati wakijiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Pia inadaiwa Zitto ataahidiwa kupewa fursa ya kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Wasira
Akizungumzia mgogoro huo akiwa mkoani Kagera, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira, alisema anajivuna kwamba ndani ya chama chake hakuna ubaguzi kama ilivyo katika vyama vingine vya upinzani ambavyo alidai kiongozi wa ngazi ya juu lazima atoke kabila fulani.
Alidai katika baadhi ya vyama, ikitokea mtu ametoka kabila tofauti akataka kugombea uongozi ngazi ya juu, kunazuka vurugu na kufukuzana kwa visingizio vya kuvunja katiba za vyama hivyo.
“Mara nyingi huwa natumia kauli ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukiishaionja huiachi kwa hiyo wameionja inawatafuna. “CCM hatuna sababu ya kushangilia matatizo yao na hatuwaogopi wala hatutaki upinzani ufe, kwa sababu upinzani ni mfumo ulio ndani ya nchi, ila nasi tuache makundi yanayotokana na uchaguzi, ili tuendelee kushika Dola kama ilivyo ada yetu,” alisema Wasira.
Vyuo vikuu
Baadhi ya wanachama wa Chadema, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu, walikutana Dar es Salaam jana na kutangaza mgogoro wa kiutawala kati ya wapigania demokrasia ndani ya chama hicho na wahafidhina.
Wanachama hao waasi ambao walisema ni wapigania demokrasia ndani ya chama hicho; lakini kwa tafsiri ya viongozi wa Chadema ni ‘wahaini’, wametangaza kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wanachama wa chama hicho wakatae baadhi ya watu waliopandikizwa kwa kukaimishwa nafasi za uenyekiti kwa manufaa ya wahafidhina.
Baadhi ya wanachama hao wakiongozwa na Greyson Nyakarungu, walidai wanatambua kuwa mgogoro ndani ya Chadema umetokana na Mwenyekiti Mbowe kutamani kuendelea kuongoza chama kwa gharama yoyote.
Nyakarungu alidai Mbowe anatamani aendelee kutawala hivyo kuzunguka katika baadhi ya mikoa na kuwaondoa katika nafasi zao viongozi waliochaguliwa kidemokrasia, ambao wanaonekana kutomwunga mkono kwa kisingizio cha kutowajibika.
Nyakarungu ambaye alijiita Brigedia wa Uasi huo, alisema watu wote waliopenyezwa kukaimu nafasi hizo za uongozi mikoani wajiondoe haraka “kabla hatujawaondoa kwa nguvu.
“Sisi tumeamua kama tulivyozunguka nchi nzima na kampeni ya Washa Taa Mchana, tutazunguka nchi nzima kuwaambia wanachama ubovu huu wa wahafidhina. “Tunamwonya Zitto na Dk Mkumbo tabia zao za kusema kuwa wanaheshimu uamuzi wa CC huku wakijua ni nini kitatokea, waache mara moja, kwani unyonge wa aina hii ni kuendelea kuruhusu baadhi ya watu kupora rasilimali za chama,” alidai Nyakarungu.
Nyakarungu, Jeremia Fumbe wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Likapo Bakari ambaye alifukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma, walisema wao ni majeruhi wa kufinyangwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho, na kila hoja ambayo wanatoa wamekuwa wanaitwa masalia ya Zitto.
Nyakarungu alisema watu wote wanaoitwa wasaliti ndani ya chama hicho au ‘wanaotumwa na CCM’ hoja yao imekuwa moja tu ya matumizi ya fedha za chama hicho, hoja ambayo pia walidai imemgharimu Zitto.
“Tunafikia hatua wahafidhina wanasema wazi kuwa ni bora chama kishuke daraja kuliko kupewa mtu wa nje, mtu wa kuja, mtu wasiyemfahamu,” alisema Nyakarungu na kusisitiza kuwa wanachama wa Chadema kutoka Mara na Kigoma ndio wamekuwa wahanga zaidi.
Nyakarungu, ambaye alidai alijiunga na chama hicho mwaka 2005 na kushiriki kujenga, alisema kilichomponza Zitto ndani ya chama hicho ni kuhoji matumizi ya chama hicho kupitia kamati ya Bunge ya PAC, ndio maana alishambuliwa yeye binafsi wakati huo ulikuwa uamuzi wa Kamati ya Bunge.
“Viongozi wetu wa Chadema wanahoji Serikali na matumizi ya fedha za walipa kodi wakitaka uwazi na usawa, leo wanataka kutonywa mapema ili wafanye marekebisho ya kuficha uovu wa matumizi ya pesa? “Zitto kama kiongozi anayejipambanua asingeweza kuwatonya ili wafiche uchafu katika matumizi ya fedha huku akitengeneza nafasi ya kuumiza vyama vingine, hii ni dalili ya udikteta. Na kwa kuwa aligusa mkia wa mfalme nge ni lazima ang’atwe,” alidai Nyakarungu.

HABARI LEO

MKUTANO UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA, KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA MLIMANI CITY.

$
0
0



Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano kutoka Rwanda Ndugu Mutabal akitoa salam zake




Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano kutoka Uganda Ndugu Mwesigwa akitoa salam zake

 
 Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano kutoka Kenya Ndugu Mutua  akitoa salam zake


 Wadau mbalimbali wa mawasiliano kutoka secta mbalimbali wakiwa wanafuatilia kwa umakini mkutano
 Mr. Mlaki Mwendeshaji wa Majadiliano akiendelea kutoa Mwongozo
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John S Nkoma akizungumzia mada juu ya Mabadiliko kutoka Analojia kwenda Dijitali
Muhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndugu Andrew Kisaka akizungumzia mada juu ya mawasiliano .


MAMISS WAANZA KUJINOA TAYARI KWA MISS TANZANIA USA PAGEANT JUMAMOSI NOV 30

$
0
0
Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant akiwaasa Mamiss Tanzania USA Pageant leo Jumamtano Novemba kwenye hotel ya Marriott
Pamela Egbe Messy mratibu wa Miss Africa USA Pageant akiwaelimisha walimbwende


MaWinny Casey Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na mratibu wa Miss Tanzania USA Pageant, Asha Nyang'anyi (kulia)
Mamiss Tanzania USA Pageant wakimsikiliza Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant alipokuwa
Lady Kate, Pamela, Ma Winny na Asha katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania USA.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Sham Manka kutoka Massachusetts akijieleza.
Aeesha Kamala kutoka Maryland akijieleza.
Joy Kalemera kutoka New Jersey akijieleza.
Namala Elias kutoka Maryland akijieleza.
Alice Mhina kutoka Maryland akijieleza.
Hellena Nyerere kutoka Maryland akijieleza.
Faith Kaasha kutoka Alabama akijieleza.
Julia Nyerere kutoka Maryland akijieleza.

USAFI WA MITARO ENEO LA MAKUMBUSHO IMEKUWA TATIZO KUBWA, MAGONJWA YA MLIPUKO YANAWEZA KUTOKEA

$
0
0
Huu ni mtaro ambao umeziba na maji hayaendi,na watu kutupa uchafu ndani yake kama unavyoonekana.
Juu ya huo mtaro kuna mgahawa wa chakula,ambao watu wanautumia kwa mahitaji ya chakula.

Kama picha inavyoonesha maji machafu yakiwa yametuama,na uchafu ukiwa umetupwa ndani yake.
Ikifika mchan watu hukaaa hapo juu na kupata chakula hii ni hatari kwa afya ya binadamu.


Ukifika maeneo ya makumbusho nyuma ya Jengo la Tigo maarufu mtaa wa kwa bwela kwa wauza viatu maarufu kwa wakina dada,hali ya usafi katika mitaro ya eneo hili ni ya kutisha ingawa imezungukwa na maofisi makubwa kama kampuni za simu na mabenki mengi.Dj sek blog ilifanya utafiti makini na kujione hali ya mitaro hiyo ikiwa katika hali mbaya kiusafi,Kwanza mitaro hiyo imeziba hivyo kusababisha maji kutuama na kupelekea maji hayo kuvunda na kuwa rangi ya njano.



Kingine cha kushangaza zaidi ndani ya mitaro hiyo watu hutumia kama sehemu ya kutupia uchafu kama mifuko ya rambo,makopo n,k.Jambo lingine ambalo ni la hatari zaidi ni eneo la juu ya mitaro hiyo kuna mgahawa ambao unauza chakula kwa ajili ya matumizi ya binadamu.Jambo la kujiuliza je watoa huduma katika mgahawa huo hawaoni hali hiyo ya uchafu ambao upo kwenye eneo lao?na je hawaoni kwamba ni hatari kwa afya za binadamu wanaokula eneo hilo?Tulipojaribu kuwauliza walikuwa hawana majibu ya kutoa.Tunaomba serikali ya mtaa wa makumbusho walione hili na kulishughulikia na sio kukaa ofisini mpaka magonjwa yatokee ndipo tuanze kuhangaika.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA), DAR ES SALAAM.

$
0
0

 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam
  Wadau wakisikiliza hotuba ya ufunguzi
 Wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi


 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi
  
 Waalikwa katika hafla hiyo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma, wakati alipotembelea katika chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) Sunday Richard, wakati alipotembelea chumba hicho baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa (wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma (kulia) na Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa, nje ya Jengo la Mawasiliano baada ya kutembelea Chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika picha ya pamoja na wadau wa mawasiliano na viongozi wa TCRA baada ya  uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR

RIHANNA KUCHANGIA SHILINGI MILIONI 162 KUSAIDIA WAATHIRIKA WA KIMBUNGA CHA HAIYAN UFILIPINO

$
0
0
Rihanna ni miongoni mwa mastaa duniani walioitikia wito wa kuwasaidia waathirika wa kimbunga kilicholeta madhara makubwa nchini Ufilipino mwanzoni mwa mwezi huu.

Staa huyo ameahidi kuchangia dola $100,000 (zaidi ya shilingi milioni 162) kusaidia maafa hayo. Mchango wake utaenda kwenye shirika la umoja wa mataifa la kusaidia watoto (Unicef).
“Dharura hutengeneza vichwa vya habari, lakini kupona huendelea kwa muda baada ta camera kuondoka. Kutokana na kuwa shabiki na mfuasi wa kazi za Unicef, kwa miaka mingi, najisikia heshima kuungana nao kuwasaidia watoto walioathirika na kimbunga cha Haiyan,” anasema Rihanna kwenye maelezo yake.

TUSIZUNGUMZIE HABARI ZA DIAMOND NA ZITTO HATA HIZI ZINAHUSIKA KATIKA JAMII

$
0
0
 Paka huyu alifuatiliwa mienendo yake na mtadao wa PAMOJA baada ya kuonekana anaweza kuwa na habari tofauti ndani ya wanajamii hasa wale watizamaji

Paka sasa amekaa muda mrefu akiwa ametulia sasa anahisi usingizi na kuanza kulainika polepole


Paka huyo anaanza kulala maana usingizi hauna baunsa
  Hapa usingizi ukamnogea paka huyo na kuamua kujiachia 
 Baada ya kusinzia takribani dakika 15 sasa akaanza kuamka uki bado usingizi haujaisha
 Paka huyu baada ya kulala sasa usingizi unakwisha na kutafakari ni jinsi gani ya kuamka na kuendelea na ratiba yake anayoifikiria
Sasa umefika muda wa kuondoka kwa paka huyo akafanye ya kwake

NA PAMOJA BLOG

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO TAREHE 28/11/2013

$
0
0
WIZARA YA UCHUKUZI

MAMLAKA  YA HALI YA HEWA

S.L.P.3056, DAR-ES-SALAAM

Fax: 2460735. email: met@meteo.go.tz


UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO.
            TAREHE 28/11/2013.

[Mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Tabora]:
[Mikoa ya  Kagera, Mara, Mwanza, Tanga]:
[Visiwa vya Unguja na Pemba]:
[Mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa]:
[Mikoa ya  Ruvuma na Morogoro(kusini)]:





Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
[Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara]:
[Mikoa ya Singida na Morogoro (kaskazini]:
[Mikoa ya Dar-Es-Salaam na Pwani]:  
[Mikoa ya Lindi, na Mtwara]:



Hali ya mawingu kiasi, mvua katika  maeneo machache na vipindi vya jua.

[Mkoa wa Dodoma ]:

Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika  maeneo machache na vipindi vya jua.



VIWANGO VYA JOTO, MAWIO NA MACHWEO YA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI
Kiwango cha juu cha joto
Kiwango cha chini cha joto
Mawio (Saa)
Machweo (Saa)
ARUSHA
26°C               
15°C               
12:12
12:26
D'SALAAM
32°C           
24°C
11:55
12:21
DODOMA
31°C
20°C
12:11
12:33
KIGOMA    
28°C
21°C
12:37
12:55
MBEYA
21°C
14°C
12:16
12:46
MWANZA
27°C
20°C
12:28
12:39
TABORA
27°C
18°C
12:25
12:43
TANGA
32°C
23°C           
12:00
12:18
ZANZIBAR
31°C           
24°C           
11:55
12:21

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa; 
kutokaKusini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutokaMashariki kwa Pwani ya Kusini.
                             
Hali ya bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi Madogo.  
                           
Matazamio kwa siku ya Jumamosi: 30/11/2013: Mabadiliko kidogo    
                                                                       
Utabiri huu umetolewa leo tarehe 28/11/2013.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

CHANZO: TABIANCHI

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBER 29, 2013

$
0
0













TOVUTI KUU YA SERIKALI KUZINDULIWA LEO KWENYE UKUMBI WA MWALIM NYERERE JIJINI DAR

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kesho tarehe 29, Novemba 2013 anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Uzinduzi wa Tovuti Kuu hiyo inayopatikana kwa anuani ya www.tanzania.go.tzutahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wananchi, Wafanyabiashara, Washirika wa Maendeleo, Taasisi zisizo za Serikali na Wawakilishi kutoka vyuo Vikuu.

Tovuti Kuu hiyo ni mojawapo ya juhudi za Serikali katika kuhakikisha kuwa taarifa na huduma zinazotolewa na Serikali zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa urahisi, wakati wowote na mahali popote ndani na nje ya nchi. Tovuti Kuu hiyo pia ni moja ya mafanikio makubwa katika kutimiza dira ya muda mrefu ya kuwa na dirisha moja linalotoa taarifa na huduma zinazotolewa na Taasisi za Serikali kwa urahisi.


Taarifa na huduma katika Tovuti Kuu hiyozimegawanywa katika maeneo makuu sita ya ambayo ni Serikali, Wananchi, Taifa letu, biashara, Sekta na Mambo ya Nje inalenga kutoa huduma mbalimbali kama upatikanaji wa nyaraka zote za Serikali, huduma zinazotolewa na Serikali kwa njia ya simu na mtandao, Viwango vya fedha, Hali ya Hewa, na Soko la Hisa.

Huduma nyingine katika Tovuti Kuu hiyo imetengwa katika ukarasa wa Nifanyeje? ambao unamjengea uwezo mwananchi wa kufahamu taratibu za upatikanaji wa huduma zinazotolewa na taasisi mbali mbali za Serikali kama nifanyeje kupata pasipoti, kibali cha kazi, TIN, Cheti cha kuzaliwa na mikopo ya chuo.

Aidha tovuti hiyo pia inalenga kuziunganisha Tovuti na mifumo ya Taasisi mbali mbali inayotoa taarifa na huduma kwa wananchi na wafanyabiashara katika dirisha moja.

Tovuti Kuu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2009 na kupatikana kwa anuani ya www.egov.go.tz chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Tovuti hiyo iliboreshwa na kuunganishwa na iliyokuwa Tovuti ya Taifa kwa anuani ya www.tanzania.go.tz mwaka 2012 chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.


IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

CHAMELEONE KULITIKISA JIJI LA MWANZA DEC 24 MKESHA WA CHRISTMAS

$
0
0

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika mnamo tarehe 24/12/2013 mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza.

Picha zaidi za Mwanamuziki mkali Afrika akisaini mkataba baina yake na viongozi waandaaji wa Show hiyo. Makubaliano haya ya kuweka mkataba yamefanyika jumatatu ya wiki hii tarehe 25/11/2013 jijini Kampalanchini Uganda.


Mwanamuziki Dr. Jose Chameleone (katikati) akiwa na Mapromota wa show itakayofanyika jijini Mwanza Dennis Mshema (Kushoto) na Mr. Ben Mwangi (kulia) mara baada ya utiaji wa saini wa kupiga show moja kali tena takatifu itakayofanyika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas katika ufukwe wa Charcoal Ribs jijini Mwanza. 

Kwa mujibu wa moja wa Mapromota hao Mr. Ben amesema kuwa ile kiu ya mashabiki wa muziki wa ukweli toka kwa Mwanamuziki Jose Chameleone sasa inakwenda kupata dawa yake, kwani maandalizi mazuri yameanza kufanyika kuhakikisha kila kilichobora kina tukia kwenye jukwaa la burudani siku hiyo ya mkesha wa Christmas.

"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Alisema Ben.

 Ameongeza kuwa bado milango iko wazi kwa makampuni mbalimbali na sekta binafsi kushiriki katika suala zima la udhamini. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0752813212.

Mbali na kuwa na masongi makali kama Bei kali, Kamila na kadhalika ambayo hadi sasa utamu wake uko pale pale Jose Chameleone kwa sasa anatikisa ulimwengu wa burudani ya muziki na ngoma zake kali kama Badilisha, Sumula, Valu valu, Tubonge na nyingine kibao... 

BAREGU AITAHADHARISHA CHADEMA KUHUSU ZITTO

$
0
0
 Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.
“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani  viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.

“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”

Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.

Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.
“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao  ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:
“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”
Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.
“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”
Lwakatare
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare alisema chama hicho kipo imara na hakiwezi kuyumba kwa sababu ya uamuzi huo.
Lwakatale ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema: “Mfumo wa ulinzi ndani ya chama upo imara, yakitolewa maelezo na ngazi za juu kinachofuata baada ya hapo ni utekelezaji.”
Alisema kilichotokea ni kitu cha kawaida na ni mwanzo wa chama kujiimarisha.
Temeke wapinga
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu na Baraza Kuu la Chadema hicho Wilaya ya Temeke wamepinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa viongozi hao.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Temeke, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, Joseph Patrick aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mgogoro huo haulengi kujenga chama, bali unakibomoa.
“Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia uchaguzi wa ndani. Hii inasababisha kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika kwa lengo la kuwadhoofisha mbele ya wanachama,” alisema na kuongheza:
“Tumeona mifano mingi ya namna hii. Wakati Chacha Wangwe akiwa hai alipotangaza kuwania uenyekiti, mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote na hakuwahi kusemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama, bali viongozi wenzake waliotofautiana kimsimamo.”
Alisema hali hiyo ilijitokeza pia kwa Zitto alipotangaza kuwania uenyekiti kama ilivyokuwa wakati wa chaguzi za viti maalumu na mabaraza ya chama.
Alisema ni vyema viongozi wakaitisha mkutano mkuu wa dharura na kuwaeleza wanachama mambo mbalimbali ikiwamo ni kwa nini wameamua kusambaza waraka ambao alisema unakidhalilisha chama badala ya waliouandika.
Katibu Chadema ahojiwa
Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Herry Kilewo amehojiwa na Polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na madai ya Zitto kutishiwa kuuawa.
Katika mahojiano hayo, Kilewo aliongozwa na Mwanasheria wake, Mussa Mfinanga, Mwanasheria wa Chadema John Malya na pia alikuwapo Diwani wa Ubungo, Boniface Jacob. Mfinanga alisema Novemba 11 mwaka huu, chombo kimoja cha habari kiliripoti kuwa Zitto ametishiwa kuuawa na mteja wake Kilewo.
Mfinanga alisema baada ya madai hayo, Jeshi hilo lilimwita Zitto kutoa maelezo yake na kisha kuona haja ya kumhoji Kilewo shutuma hizo. Alisema mteja wake amejidhanini mwenyewe na yupo nje kwa dhamana bila ya masharti yeyote.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alikiri kuhojiwa kwa Kilewo akisema ni kawaida kwa jeshi hilo kumuita mtu na kumhoji kwa mujibu wa taratibu na sheria zake.
Imeandikwa na Fidelis Butahe, Beatrice Moses, Pamela Chilongola na Editha Majura.
MWANANCHI

HUU NI MTAZAMO TU

$
0
0

EAC: JUMUIYA MPYA, CHANGAMOTO ZA ZAMANI

$
0
0
Rais wa Rwanda, Paul Kagame (kushoto) akitembea pamoja na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (katikati) na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete (kulia) Walipowasili kwenye Mkutano wa 14 wa EAC wa Viongozi wa Mataifa ya Ushirikiano huo jijini Nairobi, Novemba 30, 2012
Katika siku za hivi karibuni hali ya wasiwasi imeibuka kuhusu uimara na mshikamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tanzania na Burundi, nchi mbili kati ya nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo, zimetoa malalamiko kuwa zinatengwa na nchi wenzake wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya, Uganda na Rwanda, hasa baada ya marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana mara mbili kwenye mikutano iliyobeba jina la jumuiya.
Wa kwanza ni ule wa Entebbe tarehe 24 na 25 Juni, ambapo marais Uhuru Kenyatta, Yoweri Museveni na Paul Kagame mbali na mambo mengine walifikia makubaliano ya kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa Kenya, kupitia Kampala Uganda hadi Kigali Rwanda. Mwingine ni ule wa tarehe 28 Agosti marais hao watatu walikutana mjini Mombasa nchini Kenya kuendelea na ufuatiliaji wa yale waliyokubaliana mjini Entebbe. Hali hii imeleta maswali kuhusu uimara wa jumuiya ya Afrika, mshikamano kati ya nchi wanachama, mwelekeo wa jumuiya hiyo, na hata kuonesha dosari zilizopo ndani ya jumuiya hiyo zinazotakiwa kushughulikiwa.

Ili tufahamu vizuri undani wa kinachotokea sasa, ni vizuri tukiangalia hali halisi ya kiuchumi katika nchi za jumuiya hiyo, na tuelewe ni kwanini mikutano kadhaa imefanyika bila Tanzania na Burundi kualikwa. Kwanza ni vema tukitambua wazi kuwa, kwa sasa Kenya ni nchi yenye uchumi imara zaidi kati ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika na uchumi wake wa soko umekomaa zaidi kuliko ule wa Tanzania. Kukomaa kwa mfumo wa soko kunahitaji milango ya jumuiya iwe wazi zaidi, ili uchumi inufaike na fursa zinazotokana na matunda ya soko la jumuiya. Kwa Kenya mikutano mwili iliyofanyika bila kuwahusisha marais wa Tanzania na Burundi, kimsingi inalenga hilo. Bila shaka Uganda na Rwanda pia zinajua kuwa zitanufaika, kwa hiyo kimsingi nazo pia zina maslahi ya kiuchumi.
Lakini tukiangalia kwa upande wa Tanzania, ambayo uchumi wake unachukua nafasi ya pili katika jumuiya ambao kwa kiasi fulani unaanza kuonekana kutishia nafasi ya ule wa Kenya, hatua ya Kenya kuamua kwa ghafla kujenga reli kutoka Mombasa kupitia Kampala hadi Kigali, ni jaribio la kujihami kutokana na ushindani utakaoletwa na bandari ya kisasa inayojengwa Bagamoyo. Sio siri kuwa, kama bandari ya Bagamoyo ikikamilika na kuendeshwa kitaalamu bila “uswahili” kama ilivyo kwa bandari ya sasa ya Dar es salaam, bandari ya Mombasa itachukua nafasi ya pili katika jumuiya. Hali hiyo itakuwa ndoto ya jinamizi kwa Kenya, kwa hiyo kwa kutumia jicho la hatua za kujihami, hatua ya Kenya kwa upande fulani inaeleweka.
Hata hivyo, tukiangalia nyuma zaidi tunaweza pia kuona kuwa siku zote uhusiano kwenye mambo ya uchumi kati ya Kenya na Tanzania umekuwa ni mwongozo wa maendeleo ya jumuiya ya Afrika Mashariki, na vizuri tukiwa wakweli kuwa mambo hayo ndio yatakayoimarisha na ndio yaliyoivunja jumuiya. Kama uhusiano kati ya nchi hizo mbili kiuchumi unaendelea vizuri, basi kwa ujumla mambo ya jumuiya yataendelea vizuri, na kama kukiwa na mivutano kati ya nchi hizo mbili kiuchumi, basi jumuiya pia inatetereka. Kwa sasa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kama ilivyokuwa mwaka 1967, wakati jumuiya ilikuwa ni mali ya serikali na marais wa nchi, na uhai wake kutegemea zaidi nia yao, kwa sasa jumuiya ni mali ya watu, na hasa kwa wakenya na watanzania ambao wamekuwa na maingiliano makubwa.
Tanzania imekuwa inashiriki kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jicho la tahadhari kubwa. Kila mara inatafakari kwa makini na hata kuchelewa kusaini au kupitisha mikataba ya ushirikiano, kama inahisi kuwa hatua hiyo italeta matata kwa maslahi ya nchi na wananchi wake. Na uzuri ni kuwa kwa sasa Tanzania ina mibadala mingi ya uchumi, kwa hiyo haiko kwenye mkao wa kuburutwa. Katika miaka iliyopita Kenya imekuwa ikilalamika mara kwa mara kuwa Tanzania inachelewesha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi wanachama, na Tanzania imekuwa ikitoa maelezo mengi ya hali hiyo na kufikia hata kutosaini baadhi ya vipengele vya ushirikiano, kwa kusema inahitaji muda wa kujiandaa na kuwa na uwezo wa kushiriki kwenye vipengele hivyo. Chelewa chelewa hii ya Tanzania imewafanya wajumbe wengine waone kuwa Tanzania inawachelewesha, ndio maana wamekosa uvumilivu na kuamua kutangulia.
Tofauti za kiuchumi kati ya nchi wanachama, ilikuwa ni moja ya sababu kubwa zilizochangia kufa kwa Jumuiya ya Afrika ya kwanza mwaka 1967. Kimsingi muundo wa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki bado haujabadilika sana, kwa hiyo changamoto zilizosababisha jumuiya ya kwanza kufa [Kenya kupiga hatua zaidi kiviwanda vingi na kunufaika zaidi na soko la jumuiya kuliko nchi nyingine, watu wake kuwa na viwango vya juu vya elimu na mafunzo ya kazi kuliko wa nchi nyingine na kunufaika zaidi na soko la ajira, na kutokana na msingi mzuri wa uchumi inapata vitega uchumi vingi kutoka nje kwa kutumia jina la jumuiya kuliko nchi nyingine wanachama, na kutokana na kukusanya mitaji mingi ya ndani inaweza hata kuwekeza katika nchi wanachama], kama hazitashughulikiwa kwa makini huenda zitaendelea kuwa changamoto kubwa kwa jumuiya ya sasa.
Kumekuwa na hali fulani ya kujidanganya kwa sisi watanzania na kwa kudanganywa na wakusanya takwimu za uchumi wa jumuiya kutoka Kenya, kuwa na sisi watanzania sasa tunanufaika na soko la jumuiya kwa kuwa exports zetu zinazokwenda kwenye soko la jumuiya zimeongezeka. Pamoja na kuwa kuna ka-ukweli fulani kwenye takwimu hizo, kimsingi bado Tanzania ni soko la Kenya, kwa mitaji, bidhaa na hata nguvu kazi, na mitaji, bidhaa na nguvu kazi kutoka Tanzania ni kama havionekani nchini Kenya. Kwa hali yoyote ile hali hii haikubaliki na hii si maana ya jumuiya, au sio lengo la jumuiya. Na kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu bila shaka kwa Tanzania jumuiya haitakuwa na maana iliyotarajiwa.
Huna haja ya kuwa Profesa wa uchumi kujua ni vipi Kenya inanufaika na raslimali za Tanzania au za Jumuiya kwa ujumla, na vipi Tanzania inajikongoja au kuinufaisha zaidi jumuiya kuliko kunufaika yenyewe. Katika mkoa wowote, wilaya yoyote na mji wowote wa Tanzania, ukienda supamaketi, dukani, kwenye kioski na hata kwa mama ntilie, huwezi kukosa bidhaa za Kenya. Kuanzia chumvi, mafuta, sabuni, dawa, vyombo vya usafi na vyombo vya kupikia nk, vingi vinatoka Kenya. Ukivuka mpaka na kuingia Kenya huwezi kuona bidhaa yoyote kutoka Tanzania, kama ukiipata labda utapata sigara au pombe, vilivyoingia kwenye sehemu za mpakani za Kenya kwa njia za panya.
Hata hivyo kuna mambo mapya yaliyotokeza kabla ya jumuiya mpya kuanzishwa yanayoifanya Kenya isiwe na furaha, ambayo yanaitaka ifanye juhudi zaidi ya kupanua wigo wake wa ushirikiano ili inufaike zaidi na soko la Jumuiya. Mwaka 2000 wakati jumuiya mpya ya Afrika Mashariki inafufuliwa, Tanzania ilikuwa kwenye jumuiya nyingine ya uchumi (jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC), uanachama wa Tanzania kwenye jumuiya ya SADC hauifurahishi Kenya na mara kwa mara Kenya imekuwa ikiishawishi Tanzania ijitoe SADC. Uanachama Tanzania kwa SADC umeifanya Tanzania iwe wazi kwa bidhaa kutoka Afrika, hali hii inafanya viwanda vya Kenya vikabiliwe na changamoto kubwa zaidi. Hali hii pia inaihimiza Kenya kuchukua hatua za kuhakikisha inakuwa na nguvu ya ushindani kwenye soko la Afrika Mashariki.
Kwenye upande wa siasa, kwa sasa hali kwa ujumla ni nzuri. Nchi zote wanachama zinatambua kuwa jumuiya ni muhimu kwao, na kauli zinazotolewa na pande zote licha ya kuonesha hasira na kejeli. Watanzania na wakenya, wanajua kuwa marais wao wa sasa wataondoka madarakani baada ya vipindi vyao vya miaka 10 kumalizika, kwa hiyo wanachoangalia ni vipi jumuiya iendelee kama taasisi, na sio kama gari linalotegemea watu wawili. Ndio maana msemaji wa Ikulu ya Tanzania hivi karibuni alinukuliwa akisema Tanzania haina wazo la kujitoa kwenye jumuiya hiyo.
Hata hivyo jinamizi la tofauti binafsi kati ya waliokuwa marais wa nchi wanachama wa jumuiya ya kwanza (Jomo Kenyatta, Idd Amini na Julius Nyerere) zilichangia sana kuifanya jumuiya ivunjike. Na sasa kuna tofauti za wazi kabisa kati ya Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Rais wa Rwanda Paul Kagame, hasa baada ya Rais wa Tanzania kuishauri Rwanda kufanya mazungumzo na waasi wa kundi la FDLR walioko nchini DRC wanaoipinga serikali ya nchi hiyo, na Rais wa Rwanda kukataa kufanya mazungumzo na waasi wa kundi la FLDR. Tofauti hizo zilianza kujionesha kwenye mambo ya uchumi, baada ya Rwanda kuamua kuyatoza ushuru mkubwa malori yanayoingia katika nchi hiyo kutoka Tanzania, na baadaye kuacha kutumia bandari ya Tanzania na kuanza kutumia bandari ya Mombasa. Jambo hili ambalo nchi tatu waanzilishi wa jumuiya zilisema halitatokea tena, sasa linaonekana kuleta kivuli cha yaliyotokea mwaka 1967.     
Mbali na changamoto kubwa ya uchumi na tofauti za kisiasa, tatizo kubwa linaloisumbua jumuiya kwa sasa ni kuwa imefikia kwenye hatua ya utekelezaji wa vipengele ambavyo ni changamoto kubwa kwa maslahi makuu ya nchi (prerogatives of states). Pamoja na kuwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanajua kuwa siasa za umoja na ushirikiano ni nzuri na zina manufaa, ukweli ni kwamba umoja na ushirikiano ukihimizwa kwa kasi unakuwa na madhara ya muda mfupi ambayo baadhi ya watu hasa wale wasiojua undani wake hawakutarajia. Matokeo yake ni kuwa wakati wa kupiga hatua za utekelezaji wa mambo ya kuelekea shirikisho la kisiasa, baadhi wanaanza kushtuka na kusema, kama Jumuiya ina maana kuwa hatutapata import tax toka kwa nchi inayouza bidhaa nyingi Tanzania basi kuna dosari, kama jumuiya ina maana matajiri kutoka nchi nyingine ya jumuiya watakuja kuvamia ardhi yetu kwa kisingizio cha jumuiya basi kuna dosari, kama jumuiya ina maana watu kutoka nchi nyingine watakuja kuchukua ajira zetu na sisi hatuwezi kupata ajira kwao basi hatutaki, kama jumuiya ina maana jina la nchi yetu litatumiwa kuomba fedha kwa ajili ya miradi ya kuzinufaisha nchi nyingine basi hatutaki, kama jumuiya ina maana wahalifu kutoka nchi moja wataingia kwa urahisi katika nchi nyingine basi ni tatizo, kama jumuiya ina maana kuna wakati tutakuwa na wanachama ambao tuna tofauti za kisiasa, basi haifai.
Haya ni mambo ambayo yalitokea na bado yanatokea hata kwenye jumuiya kubwa kama Umoja wa Ulaya na hata shirikisho la Marekani, kwa hiyo ni mambo ambayo yalitakiwa kuzingatiwa na kupatiwa majibu kabla ya kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini inaonekana kuwa hadi sasa baadhi ya watu hawajui, ndio maana sauti za manung’uniko zimeanza kusikika. Labda tunaweza kusema tuliingia kwenye jumuiya kutokana na kushawishiwa, kuiga mkumbo lakini sio baada ya kutafakari kwa makini na kuangalia pande zote za shilingi. 
Ukweli ni kuwa, kutokana na kutojiandaa vya kutosha changamoto hizo zitaendelea kuwepo na zitazidi kuwa kubwa kadiri maingiliano ya kiuchumi yanavyozidi kuongezeka. Lakini ikilinganishwa na manufaa ya kiuchumi kwa nchi zote wanachama, bado jumuiya ni muhimu sana kuliko changamoto hizo zinazoweza kuondolewa moja baada ya moja na hatua baada ya hatua. Pamoja na kuwa rais Jakaya Kikwete alisema bungeni kuwa Tanzania haifikirii kujitoa, kauli za kutishia kujitoa kwenye jumuiya zilizotolewa na baadhi ya wanasiasa ni dalili ya woga, kutokuwa wawajibikaji na kukwepa ukweli. 
Pia ni kuchafua sura ya Tanzania na hata sifa ndogo ya Tanzania iliyobaki kwa sasa, na kuonekana kuwa sisi ni “quitters” na sio “fighters”. Tanzania inatakiwa ipigane ndani ya jumuiya, na kuifanya iwe mwanachama wa kweli. Wanasiasa wetu wafanye kazi ya kujenga uchumi wenye nguvu ya kushindana, wafanye kazi ya kuweka yanayohitajika ili Tanzania iweze kuwa mwanachama wa kweli.
Kibaya zaidi ni pale unaposikia kauli kuwa kama kutakuwa na haja ya kujitoa swala hili litajadiliwa na wabunge. Tatizo ni kuwa mwamko, uelewa na elimu kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa watanzania bado viko chini sana. Kila mara nikipata bahati ya kuongea na wakenya wa kawaida na watanzania wa kawaida kuhusu jumuiya, ninachogundua ni kuwa wakenya wengi hata wale wa mitaani wenye elimu ndogo kabisa, wana mwamko mkubwa kuhusu jumuiya ya Afrika mashariki na wanajua ni vipi jumuiya itawanufaisha, na wanaiunga mkono serikali yao kwa hatua inazochukua kuhusu jumuiya. 
Wanaelewa maana ya soko huria (duty free trade on member states) na maana yake kiuchumi kwa uchumi wa nchi yao, hata ukiwauliza maana ya rules of origin na manufaa yake kwa Kenya wanaweza kukueleza ni nini, kwa ujumla unaweza kuona hata wana uchangamfu (enthusiasm) na jumuiya. Lakini ukiwauliza watanzania walio wengi (bahati mbaya sana hata baadhi ya tuliowachagua kuwa wawakilishi wetu, na wale walioteuliwa kuongoza idara mbalimbali) hawajui jumuiya ya Afrika Mashariki ni nini zaidi ya kujua jina.
 Hawajui inaweza kuwa na hatari gani na manufaa gani kwa usalama wa kiuchumi wa Tanzania, wengine hata hawajui kama wanaiunga mkono serikali au kuipinga inapofanya maamuzi kuhusu jumuiya ya Afrika Mashariki, na wengine wanafanya hivyo kwa ushabiki tu. Kwa hiyo wakati tunafufua jumuiya tukawa tunasikia tu hiki kimepitishwa kile kimepitishwa, na tumekuwa ndani ya jumuiya. Lakini kilichokuwa kinaonekana wazi ni kuwa, hata wanasiasa wetu waliokuwa wanashiriki kwenye vikao, ni kama walikuwa wanalazimika kuridhia, lakini economic realities za Tanzania zilikuwa zinawasuta.
Lakini jambo la muhimu ambalo sisi watanzania tunatakiwa kujiangalia na kulipatia ufumbuzi, ni “uswahili” na siasa za “uswahili”. Siasa za uswahili zinaendelea kuitafuna nchi yetu, na ushahidi upo kwenye taasisi, idara, makampuni, familia, vikundi na vyama na mashirika mengi tunayoyaendesha. Pamoja na kuwa tunatumia maneno “urasimu” na “ukiritimba”, lakini kikubwa zaidi ya hayo ni “uswahili” na “ushkaji”. 
Inaweza kuonekana kuwa hatuna tafsiri sahihi ya maneno “uswahili” na “ushkaji”, na hakuna utafiti uliofanyika hadi sasa kuhusu  mambo haya na madhara yake kwa siasa, uchumi na jamii ya Tanzania, lakini watanzania wengine wanaofuatilia uongozi na uendeshaji wa taasisi zetu hapa Tanzania wanajua mambo haya ni nini. Kwa sasa elimu, uzoefu, ujuzi, uchapaji kazi, sio tena misingi wa uongozi Tanzania, badala yake mambo ambayo kwa ujumla wake tunaweza kuyaita uswahili ndio yanatawala mambo hapa Tanzania. Kwa wakenya kukataa uswahili, si jambo baya, sidhani kama ni busara kwa wao kukumbatia hasa kutokana na kuona jinsi unavyoitafuna Tanzania.
CHANZO: FIKRA PEVU

TAZAMA HAPA RATIBA YA MECHI YA LIGI YA UINGEREZA ZITAKAZOCHEZWA KESHO JUMAMOSI NOVEMBER 30, 2013

$
0
0










TAPELI WA KIZUNGU ANASAKWA:-​TAARIFAA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

$
0
0
Tahadhari:- Kuna tapeli mwenye asili ya kizungu anadai yeye ni raia wa Africa Kusini. ni mrefu, anaonekana sana mitaa ya Kinondoni kwa Manyanya jijini Dar es Salaam mida ya usiku. Ametapeli watu wengi sana akidai kua ameibiwa hotelini na mwanamke na anadai anaishi Mbezi Kimara. Kwa wenyeji wengi wa Kinondoni wanamfahamu na wengi wameshamsikia na wanadai ni mswahili. Chukueni tahadhari na tuko kwenye harakati za kumkamata kwa sababu amesha tapeli wengi akijifanya kuchukua namba za simu kwa ajili ya kurejesha fedha hizo tunaomba wenye tarifaa zaidi watusaidie kwa ushirikiano na polisi kumtia mbaroni. Imetolewa na mmoja ya waliolizwa



TAZAMA HAPA TUKIO LA KUSIKITISHA :BAADA YA FAMILIA YAKE KUNYANYASWA , KUTESWA , KUBAKWA KISHA KUUAWA KIKATILI MIAKA SITA ILIYOPITA,WILLIAM PETIT AFUNGA NDOA NA KUPATA MTOTO

$
0
0
 Baada ya maumivu ya muda mrefu Dr.William Petit amepata mtoto huyu mwezi huu tarehe 23, 2013.
Dr.William Petit  alishikwa na mshituko baada ya  tukio ambalo kwa hakika hatokuja kulisahau maishani mwake ni baada ya Familia yake kutekwa na kuuawa kikatili.

 Dr.William Petit akiwa na mkewake mpya baada ya maumivu ya miaka 6 akiendelea kuumia na kuwaza juu ya mke wake na watoto wake.
Mnamo mwaka 2007, tukio  la kusikitisha na kuhuzunisha lilimpata
Dr.William Petit ambapo alipoteza mke na watoto wawili ambao walitekwa , wakanyanyaswa, wakaumizwa, wakabakwa na mwisho wakauawa kwa kifo cha kikatili.




Dr.William Petit na mke wake mwezi wa nane mwaka huu wakitangaza kwamba wanatarajia mtoto.
Gazeti la Daily mail online , limeandika kuwa baada ya kufanyiwa vitendo vyote hivyo nyumba hiyo ilichomwa kwa kutumia Gesi huku mke wa Dr.William Petit na watoto wake wawili wakiwa wamefungiwa kitandani na kuzibwa vichwa na mito.

 Hizi zilikuwa picha za kwanza walizo weka mtandaoni Dr.William Petit na mkewake kuwa wanatarajiwa kupata mtoto.

 Ni huzuni sana kwa kweli Dr.William Petit akiwa na familia yake walio uwawa kikatili mwaka 2007
 Dr.William Petit  akiwa na furaha pamoja na mke wake mpya Christine Paluf

 Ni huzuni sana Mke wa Dr.William Petit pamoja na watoto wake wawili baada ya kubakwa na kuteswa wakiwa katika hili jumba walifungwa kitandani na kuunguza nyumba hii kwa kutumia gesi.

 Mbaya zaidi wakati jengo linawaka moto watoto walikuwa wanamaumivu makali ya kubakwa na kuteswa huku kichwani wamefunikwa na mito.

 Inasikitisha na kuuma sana Hiki ndicho kitanda ambacho Mke wa Dr.William Petit pamoja na watoto wake wawili waliishia hapa kwa kuungua moto.

SOURCE: DAILYMAIL ONLINE


Viewing all 16423 articles
Browse latest View live