Tahadhari:- Kuna tapeli mwenye asili ya kizungu anadai yeye ni raia wa Africa Kusini. ni mrefu, anaonekana sana mitaa ya Kinondoni kwa Manyanya jijini Dar es Salaam mida ya usiku. Ametapeli watu wengi sana akidai kua ameibiwa hotelini na mwanamke na anadai anaishi Mbezi Kimara. Kwa wenyeji wengi wa Kinondoni wanamfahamu na wengi wameshamsikia na wanadai ni mswahili. Chukueni tahadhari na tuko kwenye harakati za kumkamata kwa sababu amesha tapeli wengi akijifanya kuchukua namba za simu kwa ajili ya kurejesha fedha hizo tunaomba wenye tarifaa zaidi watusaidie kwa ushirikiano na polisi kumtia mbaroni. Imetolewa na mmoja ya waliolizwa |
↧
TAPELI WA KIZUNGU ANASAKWA:-TAARIFAA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
↧