Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa Marekani, siri ya ndoa/uhusiano wenye furaha ni busu na kusema ‘Nakupenda’ mara 10 kwa wiki pamoja na kwenda ‘out’ au date mara tatu kwa mwezi.
Utafiti huo uliofanywa kwa wanandoa 1000, uligundua pia kuwa surprise 10 za kimapenzi na mazungumzo ya kina na ya kueleweka 10 kila mwezi ni chanzo cha uhusiano thabiti. Kuwa na hobby tatu au interest zinazofanana na kwenda likizo mara mbili kwa mwaka ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kwenye uhusiano.
Kwenye utafiti huo pia imebainika kuwa siri ya ndoa kamilifu ni kukubaliana udhaifu wa kila mmoja, kuaminiana na muhimu zaidi kuwa tayari kusema samahani. Kuwa na muda mwingi wa pamoja, kuwa marafiki wa dhati na kuweza kufurahia pamoja ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa pia kwenye orodha hiyo.
Msemaji wa mtandao wa OnePoll.com, uliofanya utafiti huo alisema: Kila mtu anaweza kuoa/kuolewa lakini inahitaji kujitoa sana ili kufanya ndoa iwe kamilifu.”
Utafiti huo pia ulibaini kuwa ndoa kamilifu huwahitaji wapenzi kufanya mapenzi mara tatu kwa wiki. Pia kuwa na mabishano mara tatu kwa mwezi kumetajwa kama siri moja wapo.