Hiki ndicho kitu cha kwanza kwenye orodha ya mambo yanayowaangusha wengi. Wakati unaandiaka CV yako au barua ya kuomba kazi hakikisha tena na tena kama ulichoandika ni sahihi na hakuna makosa ndani yake. Vile vile unaweza kumpa mtu mwingine aiangalie kabla hujaituma, ili kukusaidia kuangalia makosa ambayo labda wewe hujaweza kuyaona. Hakuna mwajiri ambaye anataka kuchukua jukumu la kurekebisha makosa uliyofanya wakati wa kuandika.
2. Kutokuwa na ujuzi mzuri wa Usaili
Katika usaili wowote, kama ni ana kwa ana au kwenye simu kujua kuongea lugha vizuri na matamshi yake ni jambo la muhimu sana.Lugha za mtaani na vifupisho vya maneno vinawezekana katika maisha ya kawaida na inakubalika kwa jamii ya watu wanaokuzunguka lakini hayaleti picha nzuri kwa mwajiri hasa unapoyatumia kwenye Usaili. Hakikisa siku ya kwenda kwenye Usaili , ulale vizuri na kama ni mtu wa kwenda kwenye starehe siku hiyo upunguze kwani mtu ni rahisi kukugundua kama ulichelewa kulala.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
3. Jumbe zisizoeleweka kwenye mitandao ya Jamii
Hili ni jambo la kizamani, lakini lisikushangaze. Uwe makini kwenye mitandao ya jamii wewe unaweka vitu gani, jumbe gani. Kama wakati wote unaonesha picha za wewe ukistarehe, kunywa pombe na tabia zingine za ajabu ajabu unapoomba kazi zafisha anuani zako za mitandao ya kijamii kabla ya kuomba kazi.
4. Kutokuonekana kwenye Mtandao
Hii haimaanishi ni kigezo cha kila kazi, ni baadhi ya kazi tu. Ila kama unatafuta kazi kwenye Masoko, Uhusiano na jamii, Matangazo ,burudani na Nyanja zingize za habari waajiri wengi wanapenda kuona mtu ambaye ana taswira nzuri na yenye nguvu kwenye mitandao. Kama haujui kitu gani kinaendelea kwenye teknolojia ya habari tafsiri yake ni kwamba uko nyuma sana katika kujua mambo yanavyotakiwa kwenda.
5. Kuwa mfuatiliaji Sana
Watu wengi hufikiri kwamba waajiri wanafanya kazi ya kuwatafutia wao kazi. Ukweli ni kwamba taasisi zote za kuajiri zinataka kujaza nafasi za kazi zilizowazi kwa wateja wao. Na wanashughulikia wateja wengi kwa wakati mmoja na kujaza nafasi nyingi kwa wakati mmoja. Kwahiyo kumtumia mwajiri email au kumpigia simu yule amabye hakukujibu usifikirie kuwa utaonekana kwamba unastahiki ya kazi, ila watakuona unawachosha hivyo hawatahitaji kushughulika na wewe.
6. Wewe si Mvumilivu Sana
Kwa upande mwingine, kuna waajiri wengine watakupigia kupata habari zaidi kuhusu wewe, hakikisha unajibu kwa haraka na ufasaha wakati wote unapopigiwa simu. Kama kila wakati mwajiri anakupigia na kukufuatilia sana kuhusu habari zako inamaanisha hujamshawishi vyakutosha kwa kazi ile uliyoomba na vinginevyo inaweza kuwa sahihi.
7. Umekuwa Ukijilinda ili watu wasiwasiliane na wewe.
Kila mwajiri anakutana na jambo hili. Mtu anaweka tangazo la kutafuta kazi kwenye tovuti na anasahau kwamba litakuwepo hata baada ya kupata kazi. Kama hujawahi kuwa na anwani kwenye linkedin au mtandao mwingine usifikiri ni rahisi mtu kuwasiliana na wewe kuhusu kazi. Hata kama hupendi kazi iliyotangazwa, usiondoe anwani yako au CVhuwezi jua kwamba utapata fulsa nyingine.
8. Huna vigezo vya kupata kazi hiyo
Wakati umekata tamaa unafanya maamuzi ya kukatisha tamaa. Hata kama huna kazi na huna hela ya kutosha , hivyo unaomba kazi sehemu nyingi hata kama vigezo vyako havikubaliki haitakusaidia na hutapata nafasi ya kuajiriwa. Kama kitu ambacho mwajiri atakujua kwa sababu mbaya ni wewe siku zote kutokuwa na vigezo vya kazi.
Unapotafuta kazi hasa kwa makampuni yanayoajiri inabidi uwe mkweli, nenda na wakati na mwenye maelezo ya kutosha, kwakuwa mwajiri ni daraja la wewe kutokuajiriwa au kufanikiwa kitaaluma.