Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

IFAHAMU SABABU YA BALOTELLI KULIA KAMA MTOTO KWENYE MECHI YA JUMAMOSI YA AC MILAN NA NAPOLI

$
0
0
Sio mara ya kwanza kwa Mario Balotelli kulia kama mtoto uwanjani. Jumamosi hii baada ya kupumzishwa kwenye mechi ya AC Milan na Napoli ambapo Milan ilitandikwa bao 3 kwa 1, mshambuliaji huyo alionekana akilia kwa uchungu akiwa kwenye benchi.
Swali muhimu kwa wengi ni kwanini alikuwa analia?
Sababu ya kwanza inayosemwa ni kwamba ni kutokana na matusi ya kibaguzi aliyokuwa akiyapata kutoka kwa mashabiki wa Napoli, japo yeye hajazungumzia bado.
Sababu ya pili ni kuwa huenda ni kujiona hakucheza vizuri na kupoteza fursa za kufunga magoli na kushindwa kwenye mechi hiyo muhimu.
Sababu ya tatu huenda ni kutokana na kufahamu ukweli wiki iliyopita kuwa kumbe kweli ni baba wa mtoto wa mpenzi wake wa zamani, Raffaella Fico aitwaye, Pia. Mshambuliaji huyo alikuwa amekataa kuwa baba wa mtoto huyo lakini vipimo vya DNA vilithibitisha ukweli huo na yeye mwenyewe Balotelli kuthibitisha kwenye Twitter kwa kuandika: ‘Finally the TRUTH :-) ??…PIA… Sweet child of mine !!! your Dad.’
Kaka yake Balotelli, Enock Baruwah, alidai kuwa machozi hayo yalitokana na kuthibitishwa kuwa ni baba yake na Pia.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles