Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAGAZETI YA UFARANSA YAMCHAFUA OBAMA YADAI ANA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA BEYONCE, WAANDISHI WA MAREKANI WAKANUSHA

$
0
0
 Kuna mgongano wa habari kati ya baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa na vile vya Marekani kuhusu uhusiano uliopo kati ya Beyonce Knowles na rais wa Marekani, Barack Obama.
Gazeti la Ufaransa la Le Figaro liliripoti kuwa kuna uhusiano wa siri wa kimapenzi kati ya rais wa Marekani, Barack Obama na mwimbaji ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya Obama, Beyonce Knowles.
Habari hizo zilishindiliwa msumari na mpiga picha Mfaransa Pascal Rostain, ambaye ni rafiki wa mke wa rais wa zamani wa Ufaransa, Carla Bruni, aliyelieleza gazeti hilo kuwa habari hizi hivi karibuni zitaandikwa na waandishi wa habari wa Marekani na inaweza kuwa kama ile scandal iliyomtesa Bill Clinton, kuhusu Monica Lewinsky (1995/1996).
“Kuna kitu kikubwa kinachoendelea kati ya wawili hawa, tusisahau Marilyn (Monroe) au Monica Lewinsky. Unaweza kuwa rais wa nchi ya kwanza yenye nguvu duniani…hiyo haikufanyi usiwe mwanaume kamili.” Rostain aliliambia gazeti hilo.
Hata hivyo, ingawa Rostain alidai kuwa Washington Post lingeandika habari hiyo leo (February 11), Washington Post imeandika habari tofauti kabisa huku baadhi ya waandishi wakikanusha habari hizo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

“Sio kweli hata kidogo”, msemaji wa Post Kris Coratti ameiambia Poynter.com kwa njia ya barua pepe. 
Naye mwandishi wa wa New York Times, Dave Itzkoff ametweet kuhusu tuhuma hizo na kuonesha kutokubaliana kabisa na kilichoandikwa na gazeti la Ufaransa.
“It doesn’t seem plausible to me that the most powerful person in the world would have time for an affair with Barack Obama.”
Ni kama vyombo vya habari vya ufaransa vimeiwashia taa familia ya Obama kuhusu mahusiano ya mapenzi. Wakati gazeti la Le Figaro likiandika hayo, jarida la Gala la nchini humo limeandika kuwa Obama na mkewe Michelle wanaelekea kupeana talaka.
Familia ya Jay Z ni rafiki wa familia ya Obama, ambapo kuna wakati Michelle na Beyonce waliandikiana barua za wazi, huku familia ya Jay Z ikialikwa mara kwa mara katika ikulu ya Marekani.
Mwaka 2012, Beyonce alimuandikia Obama barua kwa mkono wake na kuipost kwenye tovuti yake, kumsapoti katika uchaguzi wa Urais.
“President Obama,
Everyday we see your heart and character, inspiring all of us to give more of ourselves.
You are the leader to take us from where are to where we need to be.
You are the reason my daughter and nephew will grow up knowing that they can truly be ANYTHING they want to be.
All my respect and adoration,
Beyoncé.” Inasomeka barua ya Beyonce kwa Obama.
Wakati hayo yote yanaandikwa, leo rais wa Ufaransa Francois Hollande ambaye amekuwa na matatizo katika ndoa yake, ameitembelea ikulu ya Marekani na kuzungumza na rais Obama.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>