Joy Kalemera (wapili toka kulia) akiwa College Park Maryland alipowatembelea darasa la kiswahili DMV siku ya Jumamosi Feb 8, 2014. Wengine katika picha ni waratibu wa Miss Tanzania USA akiwemo mkurugenzi Ma Winny Casey (wa kwanza kushoto)
Wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV wakimsalimia Miss Tanzania USA Pageant na kumwimbia nyimbo mbalimbali za kiswahili ukiwemo wimbo wa Taifa.
Miss Tanzania USA Pageant akijitambulisha na kuwaambia yeye ni mhandisi anayefanyakazi New Jersey na akawauliza kama wanafahamu maana ya neno uhandisi na wao wakajibu hawafahamu ndipo alipowaelewesha maana yake kwa Kingereza.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wanafunzi wa darasa la kiswahili wakimsikiliza Miss Tanzania USA Pageant alipowatembelea shuleni kwao College Park, Maryland.
Mwalimu mpya wa hesabati Cechelela Timo akiwafundisha hesabu kwa kiswahili wanafuzi wa darasa la kiswali DMV.
Mwalimu Asha Nyang'anyi akiwaelekeza jambo wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV.
Mmoja ya wanafunzi Briana akiwasomea kitabu cha hadithi wanafunzi wenzake.
Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akimuelekeza kitu mmoja ya wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV
Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog
Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog