Rihanna ni miongoni mwa mastaa duniani walioitikia wito wa kuwasaidia waathirika wa kimbunga kilicholeta madhara makubwa nchini Ufilipino mwanzoni mwa mwezi huu.
Staa huyo ameahidi kuchangia dola $100,000 (zaidi ya shilingi milioni 162) kusaidia maafa hayo. Mchango wake utaenda kwenye shirika la umoja wa mataifa la kusaidia watoto (Unicef).
“Dharura hutengeneza vichwa vya habari, lakini kupona huendelea kwa muda baada ta camera kuondoka. Kutokana na kuwa shabiki na mfuasi wa kazi za Unicef, kwa miaka mingi, najisikia heshima kuungana nao kuwasaidia watoto walioathirika na kimbunga cha Haiyan,” anasema Rihanna kwenye maelezo yake.