- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam
Wadau wakisikiliza hotuba ya ufunguzi
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi
Waalikwa katika hafla hiyo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma, wakati alipotembelea katika chumba cha Mtambo wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika picha ya pamoja na wadau wa mawasiliano na viongozi wa TCRA baada ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR