Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

SOMA HABARI HII UBADILI MAISHA YAKO; SABABU 7 ZINAZOKUFANYA USITAJIRIKE

$
0
0
 Ndugu msomaji wetu wa blog hii ya jamii inabidi niwe wa kwanza kukujuza haya, ni vema wangekujuza rafiki zako wa karibu lakini kwasababu hawajaweza kukujuzaa basi hainabudi nikwambie mimi. Kuna tabia fulani zinazokufanya usifikie malengo ambayo unayafikiria muda wote. Sikulaumu, bali tunaelimishana kuhusu mtu kufikia malengo yake aliyojiwekea.  Sasa ni wakati wa mabadiliko kwasababu hivi ndio vitu vinavyozuia mafanikio yako.
 
1. Kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii
Najua si vibaya kucheki "what friends are up to now and then" lakini muda unaotumia kulike status na picha za watu  ambazo hazileti tofauti yoyote katika maisha yako unasababisha upoteaji wa muda mwingi  na hata pesa pia. Hii ni hatari hasa wa vijana ambao utumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufanya mpango mkakati ambao unaweza kubadilisha maisha yako. Unaweza kujiuliza ni kiasi gani cha pesa unachokilipia kwa siku kuingia kwenye mitandao hiyo au hata kwa mwezi na je kama hiyo pesa ingekuwa unaikusanya na kuanzisha biashara nadhani ungekuwa mbali sana hasa kubadili maisha yako.
 2. Unafikiri unafanya kazi kwa bidii lakini si kweli
Ni kweli unatumia siku nzima ofisini lakini mapumziko, kusumbuliwa na kupoteza kusudi la kazi unayofanya vinachangia sana kupoteza muda wako kwa kiasi usichoweza kutegemea. Ushawahi kufikiria biashara ya pembeni itakayokuletea kipato ? Je , unafanya nini muda  wa kazi unapoisha? Je, unatumia muda wako wa jioni kukaa kwenye kochi ukiangalia TV  au laptop ukicheki movies/series ? Huo ndio muda ambao unatakiwa ufikirie business idea uliyonayo, kazi ya nje au kitu chako mwenyewe ambacho kwa siku za baadae kitakua ndio kazi yako ya kudumu.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 3.Hauna Ufanisi
Unaweza kusema unafanya kazi kwa bidii na haupotezi muda wako katika kazi zako lakini nataka nikuambie na sipendi kusema hivi, unaweza kufanya vizuri zaidi. Ndio, unafanya kazi kwa bidii lakini kuna njia ya kufanya kazi hiyo izae matunda.Unajua msemo unaosema” Siyo tu  ufanye kazi kwa bidii, bali  ufanye  kazi nadhifu.” Ukifanya kazi kwa ufanisi naamini unaweza kufika mbali.
 4.Unakata tamaa kirahisi
Labda mambo hayajaenda kama ulivyotarajia au watu hawadhamini mchango wako na hii kukufanya kukosa motisha na msukumo wa kufanya kazi. Hauwezi kufikiria malipo ya miaka ijayo kwa kazi unayoifanya leo kazi utazofanya kwa siku, wiki hata mwezi na kulipwa ni nzuri na ndio ambazo watu wengi hupendelea. Lakini kwa kila mtu aliyefanikiwa anajua kwamba ili uweze kujenga kitu au biashara imara na endelevu  inabidi uwekeze katika muda sasa na matokeo yake hayatajionyesha kwa miaka. Kama hauwezi kukubaliana na jambo hili basi utakua haufikirii kwa upeo zaidi mambo ya  baadae.
5. Hau-take Risks
Ni vizuri zaidi kutoamua kutofanya kitu ambacho kinaweza kukwama baadae. Kuacha ku-take risks ni vizuri lakini hakuna malipo bila kufanya kitu cha hatari kidogo. Kuna vitu vizuri vinaweza kutokea bila mtu ku-take risk lakini ni mara ngapi biashara inajegwa na kukua kwa kutegemea bahati halisi. "Taking risks" inabidi iwe moja ya "job description" yako na japokua ukifeli haujisikii vizuri lakini unajua kipi kitakufanya ujisikie vizuru? kufeli , kufeli, kufeli na ghafla kufaulu na kufanikiwa. Hautajisikia vibaya kuhusu kufeli kwako sababu kupitia kufeli huko ndio kulikufunza njia ya kufaulu.
 6. Hautumii Opportunities
Sio tu kuchukua risks bali hata kuchukua opportunities zinazotokea linaweza likawa jambo gumu. Opportunities zenyewe zinakuja kwa kujificha ukitofautisha na risks, maranyingi mafanikio huja kwa kukubali kuchukua opportunities zinazotisha.Tafuta opportunities kwenye sehemu ulizotegemea na utashangaa vitu utakavyogundua.
 7. Kutopenda kujishughurisha
 Vijana walio wengi hawapendi kujihusisha na shughuri yoyote bali wanakaa vijiweni na kupiga stiri lakini ikumbukwe kuwa umri unakwenda. Na pia kuna vijana wanaobagua kazi kutokana na viwango vya elimu walizonazo lakini cha kujiuliza sijawahi kusikia tumbo linabagua chakula. Elimu ni kuwa na fikra ya pembua mambo kiufanisi na sio kukaa ukasema huwezi kufanya kazi ambayo unaonekana kama unajishusha lakini kwenye maisha ya kila siku kama ukifuatilia kwamba mtu/watu watanionaje kama nikifanya hivi huwezi kufika kwenye mafanikio. Na mafanikio hayaji kwa kupenda njia za mkato ukae ukijua ukitaka njia za mkato kuna uwezekano mkubwa ukapatwa na tatizo baadaye.

Naamini unaweza kufanikiwa,inabidi tu kuangalia hivi vitu 7 nilivyovizungumzia vinaweza kubadili maisha yako ya sasa. Maana naamini changamoto kwatika maisha ndio mafanikio yako.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>