Mwanamuziki Kamanda Ras makunja (katikati) akiwa na wadau nchini Ethopia, kwa ajili ya kuipeperusha CD mpya ya Bongo Tambarare
Addis Ababa,Ethopia,
Kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU aka Anunnaki Alien Kamanda Ras Makunja amewasili nchini Ethopia kwa ziara ya siku tatu ya kikazi,kwa ajili ya kuiporomoti CD mpya "Bongo Tambarare" ,baada ya wadau wa muziki nchini humo kuomba CD hiyo iweze kupigwa katika vituo vya redio nchini humo.wadau wa Ethopia wamevutiwa sana na mdundo uliomo ndani ya CD ya "Bongo Tambarare" yenye nyimbo tatu ambayo inasikika at www.ngoma-africa.com ,habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo pia itaenda nchini urusi kwa mwaliko
maalumu katika maonyesho michezo ya olympiki ya msimu wa baridi mjini
Sochi. Kuwepo kwa hali ya baridi kali na barafu nyingi huko ulaya ! bado
kunaleta maswali mengi juu ya ziara ya wakali hao wa muziki wa dansi FFU !
kama watasafiri na kupiga mzigo ? kama kawaida yao.