Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

JINSI UAMINIFU UNAVYOTUMIKA KAMA KIGEZO MUHIMU KAZINI

$
0
0
 PICHA: Gavin Gosbert
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini kwamba kazi hazipo ama hazitoshi, ila ninachoweza kugundua kila siku ni kwamba kazi zipo nyingi ila kuna tatizo kwa wafanyakazi wenyewe. Sasa hivi imekuwa ngumu kumtafutia kazi mtu kutokana na maadili kupungua au kukosekana kabisa, kama huongei na waajiri hutoweza kunielewa bali kama ni mwajiri anaelewa vizuri kitu gani wanachohitaji.
Kwasababu ya kukosekana uaminifu hasa kwa wahasibu, mameneja na maafisa ununuzi makampuni ya kuajiri watu yataendelea kukosa hizo nafasi kwani waajiri wengi wanaanza kutafuta wenyewe wapi wanaweza kupata watu waaminifu.
Mambo niliyoyagungua;

Uaminifu unajengwa na maadili
Je umekulia katika maadili yapi, wapi na ninani ambaye anakufahamu vizuri kimaadili ili aweze kumshawishi mwajiri akuamini katika nyadhifa kubwa? Wengi wetu tumekulia katika maeneo ambayo kila kitu tunataka kucheza dili, kuongeza bei, kutengeneza nyaraka zisizo sahihi na kuidhinisha malipo hewa. Mwajiri anajua ndo maana wanaanza kubadili mwelekeo katika kuajiri, je una vigezo vya uaminifu?


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Marafiki zako ni wakina nani? na unatumia muda mwingi wapi?
Amini usiamini “Bad company of friends, corrupt good behaviour” je unahitaji mwelekeo wa taaluma yako? Ondokana na marafiki wabaya ambao wanaweza kukushawishi kufanya vitu kwa mkumbo ili upate mali haraka, ujenge uwe na gari zuri n.k. Jitahidi kuwa na watu na marafiki salama ambao wanaweza kukusaidia kujenga maadili yako kikazi na hata kimaisha.


Elimu yako si kigezo pekee
Zamani walikuwa wanaangalia nani mwenye shahada ya kitu fulani, leo Shahada hizo zimekuwa ni nyingi na mtizamo umeendelea kubadirika. Mambo ya hulka, tabia na maadili mazuri ndivyo vitu kwa sasa vinaendelea kufanya watu wengine waendelee kushikilia nyadhifa na kazi zao na wengine kulazimika kuacha kazi. Je unaweza kumpa mwajiri matarajio yake? kama huwezi shahada yako haina kazi ila tu ni karatasi kama makaratasi mengine unayoyajua.


Je wewe ni mtu wa kutegemewa?
Hakuna mtu anayeajiri watu ili wawe mzigo kwake, ila anaajiri ili kuongeza ufanisi na uzalishaji wa huduma au bidhaa yake. Mwajiri anahitaji mfanyakazi atakayeweza kufanya kazi ambayo italeta matokeo ya kuridhisha kufikia malengo ya taasisi hiyo au kampuni hivyo. Unachotakiwa kujua ni kwamba hiyo kampuni ni ya watu ambao wameweka mitaji yao ili izalishe na kampuni hiyo iendelee, hawahitaji watu watakaoleta hasara.

Hivyo kwa kumalizia usiseme kazi hakuna, jiulize je unaweza kufanya kazi? au wewe ni mzigo?

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>