Leo katika katiza katiza zangu za kuhakikisha libeneke la Mtaa kwa Mtaa halilali,nilibahatika kukatiza maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya usoni kabisa mwa Jengo la Mwanamboka pembeni ya mataa ya kuongozea magari (ambayo sikumbuki mara mwisho ililkuwa ni lini yaliwaka na kuyaongoza hayo magari) na kukutana na hali hii katika Moja ya Mitaro ya kupitishia maji.
Kiukweli hali ni mbaya sana katika mtaro huo kama ionekanavyo pichani hapa,yaani mtaro umejaa uchafu wa kila aina huku maji yakiwa yametuama bila kusogea hata hatua moja (eeehhhyataendaje na mauchafu yamejaa hivi??).hapo ndipo nikaliwaza sana lile swala la kutaka jiji letu hili la Dar es Salaam lenye Maraha ya kila aina kuonekana safi siku zote,lakini kwa hali hii inayoonekana hapa na katika baadhi ya maeneo mengine,naona ni swala hilo gumu mno kutekelezeka katika jiji letu hili.sasa sijui ni kitu gani kifanyike ili mambo yaweze kuwa mswano,walau siku moja ukiuona mtaro kama huu utamani hata kuogelea?
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Yaani ni uchafu wa kila aina uliopo ndani ya Mtaro huu.
PICHA NA MTAA KWA MTAA BLOG
PICHA NA MTAA KWA MTAA BLOG