Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUANZA KURINDIMA FEBRUARI 13 MJINI NGOME KONGWE,ZANZIBAR.

$
0
0


 Picha wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara   la 11 katika kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16 katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
 Pichani ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.
Jumla ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico.

Kutoka Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu Mandingo,Segere Original na Kazimoto.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>