Kuzima smartphone saa 3 usiku kunaweza kukufanya ufanye kazi vizuri siku inayofuata, watafiti wamesema
Tunafahamu usiku unaweza kuwa muda mzuri wa kupitia status za washkaji Facebook, kutazama picha mbalimbali Instagram ama kufuatilia mijadala kwenye Twitter lakini hicho kinaweza kuwa kikwazo kikubwa cha nia yako ya kutaka kupata usingizi wa kutosha ama kuwa na utendaji mzuri kazini.
Watafiti hao wanasema kujiondoa kabisa na matumizi ya simu usiku ni njia ya kupata usingizi mzuri usiku. Wamewaomba waajiri kusubiri kutuma email hadi asubuhi
Timu katika chuo kikuu cha Washington imesema matumizi ya simu usiku sana yanaweza kuharibu kabisa usingizi wako na namna utakavyofanya kazi siku inayofuata. Wameshauri wafanyakazi wawe na tabia ya kuzima simu ama lasivyo watajikuta wakishindwa kufurahia kazi kesho yake.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Sababu ya hii kama tutakavyoelezea, ni kwamba smartphones ni mbaya kwa usingizi, na usingizi ni muhimu kwa uchapakazi wa mwajiriwa,” alisema Christopher Barnes, Profesa Msaidizi katika chuo kikuu cha Washington (Foster School of Business) aliyeongoza utafiti huo utakaochapishwa kwenye jarida la , Organizational Behavior and Human Decision Processes baadaye mwaka huu.
“Bahati mbaya smartphones zimetengenezwa mahsusi kuharibu usingizi. Sababu zinatufanya kiakili kuendelea na kazi hadi usiku, zinafanya kuwepo ugumu wa kujiondoa kisaikolojia kutoka kwenye masuala muhimu ya siku ili tupumzike na kulala. Pengine suala gumu kuliepuka kutoka kwenye smartphones ni kwamba zinatuweka kwenye mwanga, ukiwemo mwanga wa blue. Hata kiwango kidogo cha mwanga wa blue hupunguza uzalishaji wa kemikali ya usingizi, melatonin, ikimaanisha kuwa muonekano (display) unaweza kutengeneza madhara haya.”