Waandamanaji wakipambana na polisi mjini Kiev
Vifo hivyo ni vya kwanza tangu kuzuka kwa maandamano ya kuipinga serikali miezi miwili iliyopita. Waandamanaji na polisi nchini Ukraine wamepambana tena mapema leo (23.01.2014), baada ya ghasia kuzuka hapo jana Jumatano na kuigeuza sehemu ya katikati ya mji mkuu, Kiev kuwa uwanja wa vita, huku polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Vifo hivyo vimezusha hofu mpya baada ya miezi miwili ya maandamano ya kuipinga serikali yaliyochochewa na hatua ya serikali kutosaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya, kutokana na shinikizo la Urusi.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Moshi mweusi ulifuka kutokana na magurudumu kuteketezwa wakati wa vurugu hizo mjini Kiev, huku picha za magari ya kivita yakitumiwa kupambana na waandamanaji hao.
Makabiliano hayo yanakuja baada ya siku moja ya kubuniwa sheria mpya za kuharamisha maandamano wiki jana. Bunge liliidhinisha sheria hizo wiki jana na kusababisha vurugu mpya
Viongozi wa mashitaka walithibitisha kuwa watu wawili walifariki kutokana na majeraha ya risasi. Ni watu wa kwanza kufariki kutokana na vurugu tangu kuanza Novemba mwaka jana kutokana na mapendekezo ya serikali kujiunga na muungano wa Ulaya
Waandamanaji walianza, kuwatupia mabomu ya petroli na mawe wakati polisi wa kupambana na ghasia nao waliwatupia magurunedi na risasi za mipira