Hali ya dereva bingwa wa zamani wa mbio za magari (Formula One), Michael Schumacher imeanza kuimarika kufuatia ajali mbaya aliyoipata December 29 mwaka jana na kumfanya apoteze fahamu kwa kipindi kirefu.
Meneja wa Schumacher, Sabine Kehm ambaye amekuwa akitoa taarifa za afya yake, kwa mara ya kwanza hakutaja neno ‘critical’ wakati akieleza kuhusu maendeleo ya matatibu anayoyapata dereva huyo.
“Familia ya Michael inafurahishwa sana na kazi inayofanywa na timu ya madaktari kumtibu Michael, na wanawaamini moja kwa moja.” Ameandika meneja wa Schumacher kwenye barua pepe. “Michael’s condition is still considered as stable.”
Mshindi huyo wa dunia wa mbio za magari kwa mara saba aligonga kichwa chake kwenye jiwe (mwamba) wakati akiteleza kwenye barafu December 29.