Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

MAITI YA KICHANGA YAOKOTWA DAR

$
0
0

Dar es Salaam. Watu wawili wamefariki dunia akiwemo mtoto mwenye umri wa siku moja  ambaye maiti yake imekutwa kwenye  nyumba ambayo haijakamilika ujenzi (pagale), katika matukio yaliyoripotiwa  juzi jijini Dar es Salaam.
Katika tukio la pili, mwanamume mmoja amefariki dunia baada ya kuanguka wakati akijaribu kuangua nazi kwa kutumia fimbo na kusababisha kichwa chake kupasuka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema katika tukio la kwanza, maiti ya  mtoto wa kike mwenye umri wa siku moja iliokotwa  kwenye nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake.
Minagi alisema tukio hilo lilitokea Novemba  24, mwaka huu ambapo maiti hiyo ilikutwa imetupwa katika nyumba hiyo, huku ikiwa haina jeraha. Hata hivyo hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo na polisi wanaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo na maiti yamehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Katika tukio la pili, Mkazi wa Mjimwema Songambele Shija (60) amekutwa amekufa huku kichwa chake kikiwa kimepasuliwa na matofali yaliyodondoka kutoka kwenye nyumba ambayo haijakamilika ujenzi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engilbert Kiondo alisema tukio hilo limetokea Novemba 21 mwaka huu saa 7:00 mchana katika eneo la Ungindoni Jangwani Wilaya ya Temeke.  Kiondo alisema chanzo cha kifo chake inasadikiwa kuwa marehemu enzi za uhai wake alipanda juu ya pagala hilo kwa kutumia stuli ili aweze kuangua nazi kwenye mnazi uliopo karibu na nyumba hiyo.
Alisema alitumia fimbo ndefu yenye ndoano kuangulia nazi hizo huku akiwa amepanda juu ya ukuta huo ambapo ulishindwa kuhimili uzito huo na kuporomoka na kusababisha kifo chake.

MWANANCHI



Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>