Nyumba ya mkazi wa kitongoji cha Lukondo katika kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka, Fikiri Buma ikiwa imebomolewa na kile kilichodaiwa kuwa ni utekelezaji wa amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya Morogoro Vijijini ambapo zaidi ya nyumba 20 zilibomolewa januari 10 mwaka huu tarafa ya Mkuyuni mkoani Morogoro.
Mkazi wa kitongoji cha Lukondo kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka Harouna Chunga (87) akiowaonyesha waandishi wa habari wa kituo cha luninga cha ITV, Sifuni Mshana mwenye kamera na Michael Msillo bendera ya CCM tawi la kitongoji hicho namna ilivyochanwa na watu wanaodaiwa kiutekeleza amri ya kubomoa nyumba katika eneo hilo januari 10 ambapo jumla ya nyumba 25 zilibomolewa mkoani Morogoro.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa kitongoji cha Lukondo kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka Hamdan Chawila kulia na mmiliki wa nyumba iliyobomolewa Amina Said (50) kushoto wakiangalia uhalibifu baada ya nyumba zaidi ya 20 kubomolewa na kile kilichodaiwa kuwa ni utekelezaji wa amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya Morogoro Vijijini ambapo zaidi ya nyumba 20 zilibomolewa januari 10 mwaka huu tarafa ya Mkuyuni mkoani Morogoro.
Na Mtanda Blog, Morogoro.
WANANCHI zaidi ya 3,00 wa kitongoji cha Lukonde kijiji cha Kikundi hawana sehemu ya kuishi baada ya nyumba zao kudaiwa kubomolewa na askari wa jeshi la polisi ikishirikiana na mgambo kwa madai ya kutekeleza amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya wilaya ya Morogoro ili kupisha ujenzi wa majosho ya kuogeshea mifugo ya mwekezaji katika tarafa ya Mkuyuni mkoani hapa.
Katika tukio hilo lililotokea januari 10 kuanzia majira ya mchana jumla ya nyumba 25 za wakazi wa kitongoji hicho zinadaiwa kubomolewa kwa madai ya kupisha ujenzi wa majosho ya kuogeshea mifugo eneo la kitongoji cha Lukonde chenye ukubwa wa zaidi ya ekari 3,000.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Lukonde, Hamdan Chawila alisema kuwa jumla ya nyumba 25 zimebomolewa na askari polisi ikishirikiana na mgambo ili kupisha ujenzi wa josho la kuogeshea mifugo na kusababisha zaidi ya wananchi 3,00 kukosa sehemu ya kuishi.
Chawila alisema kuwa tukio hilo hakuna kiongozi wa kitongoji hicho ambaye ameshirikishwa jambo ambalo wameshangaa kuona askari pamoja na mgambo wakivamia na kubomoa nyumba hizo huku akieleza kuwa eneo hilo anafahamu kuwa lina mgogoro na anayedaiwa kuwa ni mwekezaji aliyefahamika kwa jina la, Profesa Martin Ndabikunze Shem wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) huku kesi ya msingi ikiwa imefunguliwa katika mahakama ya mwanzo Mikese baada ya mgogoro wa muda mrefu.
“Januari 10 mwaka huu majira ya mchana tulivamiwa na askari polisi wakiwa na mgambo na kubomoa nyumba 25 katika kitongoji changu na kusababisha wananchi zaidi ya 3,00 kukosa sehemu ya kuisha na kufanyika kwa uhalibifu wa mali mbalimbali”. Alisema Chawila.
Mmoja wa wahanga wa tukio hilo, Fikiri Mikidadi Buma alisema kuwa tukio hilo la kubomolewa nyumba yake pamoja na wenzake limemrudisha nyuma kimaendeleo ukizingatia tayari alifanikiwa kujenga nyumba iliyoekzwa na mabati.
Buma alisema hakuna taarifa zozote juu ya baada ya kubomolewa nyumba zao katika zoezi la kuwaondoa kwa nguvu lililofanywa na jeshi la polisi, mgambo pamoja na kundi la vijana wanaodaiwa kushiriki katika tukio hilo.
“Ninachojua mimi eneo hili lina mgogoro na mwekezaji na kesi ya msingi ipo mahakama ya mwanzo Mikese lakini nimeshsngazwa kuona askari polisi na mgambo kuvamia nyumba yangu na kuibomoa zikiwemo na nyumba za wenzangu na kupata hasara ya mali na wengine kuibiwa fedha katika tukio hilo la bomoa bomoa”. Alisema Buma.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema kuwa jeshi la polisi halikuhusika katika ubomoaji wa nyumba hizo na badala yake askari wa jeshi hilo walienda katika eneo hilo baada ya kutokea kwa vurugu baina ya wananchi na wanamgambo aliodai walikuwa wanatekeleza amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya wilaya ya Morogoro kubomoa nyumba eneo hilo.
Kwa hisani ya Juma Mtanda Blog