Muigizaji aliyehamia kwenye muziki, Snura anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Ushaharibu’ kabla ya kutoa album ya Majanga pamoja na filamu yake.
Snura akiongea na Clouds FM weekend hii, Snura alisema kwenye video ya ‘Nimevurugwa’ kuna chorus ya ‘Ushaharibu’ ambayo imefanya shabiki wake wamuulizie kama anataka kuachia wimbo kama huo.
“Muziki kinachofuata ni ‘Ushaharibu’ kama watu ambavyo wameona video yangu nimevurugwa ina chorus ya ‘Ushaharibu’ watu wamekuwa wakiniulizia sana kuhusiana na hiyo ngoma. Ni ngoma ambayo imependwa kabla hata ijatoka. Kwahiyo sasa hivi najiandaa kuiachia hiyo ngoma lakini mtaani kuna ngoma niliachia kama zawadi kwa wapenzi wa taarab inaitwa ‘Huko Nyuma’ kwahiyo ningependa kuitoa sasa hivi ‘Ushaharibu’ nitakuwa kama napandisha vitu juu yake. Najaribu kuvuta muda kidogo halafunitaiachia,” alisema.
“Natarajia kuachia album ambayo itakuwa na mseto wa kutosha ikiwemo hiyo nyimbo ya taarab ,tutakuwa na mduara,kutakuwa na afro pop na nyimbo ambazo zitakuwa tofauti tofauti yaani ya album ya Majanga itakuwa na nyimbo tofauti tofauti na ndani ya mwaka huu nitaachia album na filamu ya Majanga.”