Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

ELIMU YA BURE: TAMBUA KUNDI LA DAMU ULILOPO , SOMA HAPA

$
0
0

Katika pekua yangu nimegundua leo hii kuwa watanzania wengi hatujui tupo
katika kundi gani la damu.

Na mbaya zaidi utakuwa wakina mama wana kundi labda -O, au kundi lenye
Negative huwa wanajifungua mtoto mmoja tu halafu hajifungui tena au
wakijifungua mtoto akifa hawajifungui tena, hii inatokana na kutojua kundi
la damu la mama na kundi la mtoto aliyezaliwa, kama mama hatapimwa na
kujulikana kundi lake la damu basi ataonekana tasa, hazai. 
 Kinachotakiwa kufanyika ni mama kutambua kundi lake la damu, na
atakapojifungua tu mtoto naye achukuliwe damu kwa ajili ya kujua kama
wanafanana kundi au laa. kama hawafanani ni lazima mama achomwe sindano
pale pale inayoitwa Ant-D ili imuwezeshe kupata ujauzito tena na
kujifungua. Bila hivyo mama kupata tena ujauzito ni hadithi na atatembea
sana kwa waganga, hospitali, makanisani akitaka msaada kama hawajagundua
hili.

Nawashauri watanzania wenzangu tupime ili tutambue makundi yetu ya damu.
Imeandaliwa na Buberwa Robert Blog

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>