Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameuvunja utawala wa miaka minne wa Lionel Messi wa Argentina anayechezea klabu pinzani ya Barcelona baada ya kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Fifa ya mwaka 2013 hapo jana ambapo sherehe hizi zilifanyika Zurich nchuni Uswisi.
Mchezaji wa zamani wa Brazili, Pele akionesha jina la mshini ambaye ni Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo ya kuonesha yeye ndiye wanasoka bora wa FIFA MWAKA 2013, wa kwanza kulia ni Rais wa FIFA, Sepp Blatter na wapili kutoka kushoto ni Rais wa shirikisho la Mpira la Ufaransa(FFA), Francois Moriniere na wa kwanza kushoto ni Rais wa EUFA, Michel Platini
Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo, akimkumbatia mwanae Cristiano Ronaldo Junior baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa FIFA wa mwaka 2013
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kutokana na furaha machozi yalimtoka Cristiano Ronaldo
Rais wa FIFA, Joseph S. Blatter akimkabidhi tuzo ya mwanasoka bora wa FIFA wa mwaka 2013 Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa na furaha baada ya kutwaa tuzo hiyo
Kwa upande wa wanawake, kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Nadine Angerer ameibuka kinara mbele ya Marta (Brazil) na Abby Wambach (Marekani). Mdada huyo aliisaidia Ujerumani kutwaa taji ya Euro 2013 kwa wanawake akiokoa penati katika mechi yao ya fainali dhidi ya Norway waliyoshinda 1-0
Nadine Angerer akizungumza jambo baada ya kuchuku tuzo ya mwanasoka bora wa kike
Picha ya Pamoja
Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa na mke wake, Irina Shayk pamoja na mtoto wao Cristiano Ronaldo Juniorkwenye sherehe zilifanyika Zurich nchuni Uswisi
Mchezaji wa tumu ya taifa ya Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa kwenye picha ya pamoja na Nadine Angerer ambaye ni mchezaji wa timu ya wanawake ya Ujerumani na timu ya Brisbane Roar baada ya kupewa tuzo zao za uchezaji bora wa mwaka 2013