Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAARIFA ISIYO SAHIHI KUHUSU TSUNAMI

$
0
0

Dear wadau, 
Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami. Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji.
Taarifa rasmi ni kama ilivyotumwa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa kama inavyoonesha hapa:
Ujumbe huo unasomeka kama hivi:
TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usikuTsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwakuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka yaHali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwamujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.
Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha mkangamanyo kwa wananchi.
Asante tena kwa ushirikiano wako,
Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,

Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>