Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

YANGA YAOMBA RADHI KUJITOA MAPINDUZI

$
0
0
 
UONGOZI wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam umeomba radhi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushindwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea mjini hapa Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo Clement Sanga jana wakati alipokabidhi Sh milioni 10 kwa ajili ya kufanikisha michuano hiyo ambayo kilele chake ni siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Jumapili hii.
Alisema Yanga ni miongoni mwa klabu zenye historia kubwa ya Zanzibar ambapo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Amaan Karume alitoa mchango mkubwa wa kuanzishwa kwa klabu hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo lake.
"Kwa niaba ya uongozi wa Klabu ya Yanga na Mwenyekiti mwenyewe tunaomba radhi kwa kushindwa kuhudhuria mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo sisi ni sehemu ya wadau wakubwa.......tumetingwa na harakati za maandalizi ya mashindano ya klabu Bingwa ya Afrika," alisema.
Alisema klabu hiyo imeshindwa kushiriki katika Kombe la Mapinduzi baada ya Kamati yake ya Ufundi kuvunjwa na hivyo kukosa mwalimu ambaye ataongoza timu hiyo kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi. "Sababu moja kubwa iliyopelekea kushindwa kuhudhuria Kombe la Mapinduzi ni kuvunjwa kwa Kamati ya Ufundi ambapo walimu wote walifukuzwa kwa hivyo ilikuwa vigumu sana kuja Zanzibar bila ya mwalimu,' alisema.


 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mapema akipokea fedha hizo, Makamu wa Pili wa Rais ambaye ni mlezi wa Kombe la Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi alizitaka klabu za soka nchini kuepuka migogoro isiyokuwa na lazima kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka nchini.
Alisema migogoro na mivutano katika soka ni sawa sawa na migogoro katika vyama vya siasa ambayo itavuruga maendeleo ya kuimarisha vyama hivyo katika kuelekea kwenye uchaguzi.
"Naishauri Klabu ya soka ya Yanga kuepuka migogoro katika soka ambayo daima kazi yake kubwa kurudisha nyuma maendeleo ya soka," alisema.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haikufurahishwa na kitendo cha Yanga kukacha michuano hiyo zaidi kutokana na timu hiyo pamoja na Simba kuwa na mashabiki wengi na mvuto katika maendeleo ya soka nchini.
"Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepokea ombi lenu la kuomba radhi kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo migogoro iliyoibuka hivi karibuni,"alisema Balozi Iddi.
Sanga alisema Yanga inaondoka kuelekea Uturuki kwa ajili ya kupiga kambi ya maandalizi ya michuano ya kimataifa. Alisema timu hiyo imekubaliana na uongozi wa Kombe la Mapinduzi kwamba itakuja Zanzibar na kucheza mechi tatu za kirafiki ambapo mapato yatakayoingia yatakwenda moja kwa moja katika mfuko wa Kombe la Mapinduzi.
Wakati timu zikijiandaa na michuano hiyo mwishoni mwa mwaka jana, Yanga kupitia kwa msemaji wake Baraka Kizuguto mara kwa mara alikaririwa na vyombo vya habari kwamba hawajapewa taarifa rasmi ya ushiriki katika michuano hiyo, kauli ambayo ilipingwa na waandaaji.
Lakini siku moja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, Yanga ilitangaza kuvunja benchi lote la ufundi na pia ikatangaza kujitoa kwenye michuano hiyo, kitendo kilichopingwa na wadau wa soka wakidai kuwa Yanga haikufanya uungwana kujitoa.


HABARI LEO

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>