Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kwa mujibu wa gazeti la The Standard la nchini Zimbabwe walinzi 27 wanaomlinda Rais Robert Mugabe wamesimimishwa kazi kwa kudaiwa hawakuwa wamejipanga baada ya rais huyo mzee kuanguka.
Kwa mujibu wa vyanzo, walinzi hao walipewa barua za kusimamishwa kazi Ijumaa iliyopita. Kuna ripoti pia kuwa baadhi ya maofisa wanaweza kufukuzwa kazi.
Sura mpya za walinzi wake zilionekana Ijumaa wakati Mugabe alipokutana na rais mpya wa Zambia Edgar Lungu mjini Harare.
Uchunguzi mkali unaendelea kufuatia tukio hilo lililomuabisha Mugabe.