Quantcast
Channel: PAMOJA BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

TAZAMA PICHA ZA SIKU MAMA VICKY NSILO SWAI ALIPOMRUDISHIA MZEE MANDELA VIATU VYAKE NA KUPONGEZWA MAZISHINI

$
0
0

 Rais wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.

Mzee Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikononi mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. Viatu hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia)   Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerezani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.


 Rais Kikwete akimtambulisha Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere kwa waombolezaji wakati wa shughuli ya mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu Afrika kusini Desemba 15, 2015



ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya Mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu

Mama Vicky Nsilo Swai akishangiliwa na waombolezaji kwenye mazishi ya Mzee Mandela wakati Rais Kikwete alipomtambulisha na kueleza historia ya jinsi alivyomkaribisha Madiba nyumbani kwake na kumtunzia viatu vyake, simulizi ambayo ilimsisimua kila mtu aliyekuwepo ukumbini hapo na mamilioni waliokuwa wanaangalia tukio hilo live dunia nzima.


Maandishi ya Mzee Mandela kwa Mama Vicky Nsilo Swai aliyoyaandika kwenye kitabu alichompa kama zawadi baada ya kurudishiwa viatu vyake mwaka 1995.

CHANZO: MICHUZI BLOG

Viewing all articles
Browse latest Browse all 16395

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>