Kuna aliyebanwa hapa zinafanyika jitihada za kuchimba kumwokoa. Inasikitisha na kutia matumaini kumwona aliyebanwa kuanzia kiuno kwenda miguuni naye anajitahidi kuchimba kwa mikono
Basi la Kampuni ya Hood Limited lenye namba za usajili T 159 AXM lililokuwa linatoka Mbeya kuelekea Arusha limepinduka eneo la Melela- Mlandizi, Mvomero mkoani Morogoro na kujeruhi watu kadhaa na kuua mtu mmoja. Basi hilo lilikuwa likijaribu kulikwepa gari lingine.
PICHA NA MAGGID MJENGWA