MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Kwezi Seleli (20) mkazi wa kijiji cha Kalama,kata ya Uyogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuwawa kwa kuchinjwa sehemu za shingoni na mume wake akiwa amelala usiku.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo saa kumi alfajiri katika kijiji hicho huku akimtaja mwanamume aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Chalia Samweli (25).
Kwa mujibu wa Kamanda huyoa amesema kuwa mwanaume huyo alitumia panga kumuua mke wake huku naye akifanya jaribio la kujia kwa kunywa sumu aina ya Diazone inayotumika kuogeshea mifugo ambapo hakufa alikuwa mahututi.
Aidha kamanda amesema kuwa katika eneo la tukio kulikutwa panga moja na kwamba chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa wa mauaji hayo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa kupatiwa matibabu.
CHANZO: DUNIA KIGANJANI BLOG