Kifo cha Paul Walker na rafiki yake Roger Rodas hakikusababishwa na tatizo la kiufundi kwenye gari walililokuwa wakiendesha Porsche Carrera GT, kwa mujibu wa wachunguzi. Badala yake, ajali hiyo iliyosababisha kifo cha muigizaji huyo wa Fast & Furious ilisababishwa na mwendo kasi wa gari hiyo.
Akiongea kwa masharti ya kutotajwa jina lake, afisa mmoja wa polisi amesema dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu kutokana na gari kuwa kwenye mwendo mkali. Uchunguzi mwingine umedai kuna uwezekano pia kuwa chenga za mawe barabarani ziliifanya gari hiyo iteleze na kugonga taa ya barabarani na mti.
Paul Walker alizikwa Jumapili nchini Marekani.