Thamsanqa Jantjie
Mkalimani fake wa hafla ya kumbukumbu ya Mandela iliyofanyika December 10, Thamsanqa Jantjie amelazwa kwenye hospitali ya magonjwa ya akili ya Sterkfontein (Psychiatric Hospital).
Kwa mujibu wa gazeti la The Star, mke wa Jantjie alimpeleka kwenye hospitali hiyo iliyopo Krugersdorp kufanyiwa uchunguzi Jumanne hii ambako ilipendekezwa alazwe. Jantjie alitakiwa kwenda Sterkfontein December 10 kufanyiwa check-up. Hata hivyo kufuatia kupewa ofa ya kufanya ukalimani kwenye hafla hiyo kubwa ya Mandela kwenye uwanja wa mpira wa FNB uliopo Soweto, Jantjie aliwasiliana na hospitali hiyo kupanga upya miadi yake.
Baada ya shughuli hiyo, Jantjie aliviambia vyombo vya habari kuwa alikuwa na matatizo ya akili yaliyomfanya aone malaika uwanjani hapo na kwamba alipaniki baada ya kuona polisi wenye silaha. – SAPA.