Aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Emanuel Mteming'ombe. Bw. Mteming'ombe
KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Bw Emanuel Mteming'ombe amefariki dunia katika hospital ya mkoa wa Iringa.
Katibu huyo alikuwa amelazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa kwa zaidi ya siku moja akisumbuliwa kwa ugonjwa athima na leo amefariki dunia.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amethibitisha juu ya taarifa hiyo na kuwa taratibu za mazishi zinafanywa .
CHANZO: FRANCIS GODWIN BLOG