Mwanaume raia wa China ambaye alipata ajali ya kukatwa kabisa mkono wake wa kulia na mashine ya kiwandani, alilazimika kuunganishwa mkono huo na kifundo cha cha mguu wake (ankle) kwa muda wa mwezi mzima ili uendelee kuwa hai wakati akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kurudishiwa mkono huo sehemu yake.
Madaktari waliomhudumia Xiao mara baada ya kupata ajali hiyo Novemba 10, walimwambia hawataweza kuuokoa mkono wake, lakini alipohamishiwa katika hospitali kubwa masaa saba baada ya ajali ndipo alipoambiwa bado kuna uwezekano wa mkono huo uliotengana kabisa kuwa hai.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Xiao aliambiwa zoezi la kuurudisha mkono wake sehemu yake linaweza kufanikiwa, lakini mpaka mkono wake wa kulia utakapopona kabisa. Na ili kuendelea kuufanya mkono uliokatika uwe hai wakati huo wa kusubiri, madaktari walisema hawana njia nyingine zaidi ya kuunganisha na ‘ankle’ ya mguu wake.
Desemba 10 ndipo madaktari waliamua kuurudisha mkono wa Xiao sehemu yake, na wamesema kuwa zoezi la upasuaji huo lilienda vizuri japo kuwa atahitajika kufanyiwa operations nyingi za ziada ili kuufanya mkono upone kabisa.
Source: The Independent